Mchoma chapati anahitajika

Mchoma chapati anahitajika

RingaRinga

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2015
Posts
1,047
Reaction score
521
Ndugu habarini.

Nina kamgahawa kangu.

Nahitaji kijana wa kike au kiume kwa kazi ya mgahawa. Mwenye uwezo wa kuchoma chapati zilizochambuka (zisizo na mafuta mengi), mwaminifu, itapendeza zaidi kama anaweza pia kupika wali mzuri sufuria kubwa kuanzia kilo kumi na mapishi mengine.

Malipo kuanzia laki moja kwa mwezi, Makazi bora bure, Kula bure mgahawani.

Please nipatieni connection hiyo bandugu nimpate huyo mtu, tufaane ktk utafutaji.

Eneo ni Bwisya Ukerewe.

Mawasiliano 0787597951.
 
Ndugu zangu, mambo yanazidi kufunguka sana. Mara baada ya jamaa mmoja kutoa nafasi ya kazi kwa muuza uji, sasa ametokea mwingine anayo ya kukaanga chapati.
 
Nipo, chapati za kuchambuka, za kumimina, wali, pilao, ugali, mboga mboga vyote naandaa,

Nitakuwa na kijana wangu wa kazi,

Usiku saa 3 unilipe elfu 10 , tukutane asubuhi saa 11.
 
Acha unyonyaji wewe...yaani laki moja kwa mwezi ni sawa na shilingi 3300 kwa siku.Wewe upo tayari uajiriwe halafu mshaharà wako kwa siku uwe shilingi elfu tatu?
Zingatia
  • Makazi bure
  • Chakula Bure
  • Eneo/Mkoa husika
pia amesema kuanzia kiasi fulani, nadhani kutakuwa na makubariano zaidi ya kiwango halisi.
 
Nipo, chapati za kuchambuka, za kumimina
1662464165654.png

1662464186735.jpeg
 
Yes hizi ndizo kazi ambazo napenda kuona zikiwekwa humu

Mkuu hongera sana
Ukimpata usisahau kutuletea mrejesho mkuu


Mungu awe pamoja nawe 🙏🙏
 
Nipo, chapati za kuchambuka, za kumimina, wali, pilao, ugali, mboga mboga vyote naandaa,

Nitakuwa na kijana wangu wa kazi,

Usiku saa 3 unilipe elfu 10 , tukutane asubuhi saa 11.
@mamdenyi kumbe upo,
Tuanze na 7000 kwa siku kwa nyote wawili, hali tutaiona pamoja kama tunaweza ongeza,
Nyama choma na chips pia unaweza?
 
Back
Top Bottom