Mchome akanusha kauli ya Mnyika kuwa wanalipwa milioni 2 ili kumchafua John Heche

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mwanga na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa, Lembrus Mchome, amesema wanachama wa chama hicho hawataki kuona ufisadi ukitokea ndani ya chama chao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mchome amedai kuwa kuna fedha za wafanyabiashara zinazopelekwa kwa viongozi wa juu lakini hazisimamiwi ipasavyo na hazifiki kwenye shughuli za chama ngazi za chini.

Mchome amepinga vikali madai ya Katibu Mkuu John Mnyika kuwa wale wanaopigania katiba ya chama wanalipwa na CCM."Hilo ni uzushi na uongo mkubwa, Kama Lissu na Heche waliposema kuna fedha chafu hawakushutumiwa, kwa nini sisi sasa tunashutumiwa?

Katibu Mkuu asichafue watu," amesema.Ameongeza kuwa dalili ya mgogoro ni pamoja na kutokuwepo kwa Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ wakati wa ziara ya Makamu Mwenyekiti, jambo analosema linaonyesha uongozi umegawanyika.

Amehitimisha kwa kudai ana ushahidi wa mfanyabiashara aliyetoa shilingi milioni 256 kwa kiongozi wa chama Lubumbashi mwaka jana lakini fedha hizo hazikufika hazina ya chama."Tunaomba wafanyabiashara wasitishe kutoa fedha kwa sasa, Turejee kwenye uhalisia wa CHADEMA wa miaka 30, Kukosoa si dhambi, ni uhuru wa kikatiba," amesisitiza Mchome.

Pia soma: Mnyika afafanua tuhuma za Heche na matumizi ya fedha za ToneTone
 
maskini ka J.Mnyika dah:CouldYouNot:
 
Binafsi sio muumini wa siasa za maji taka! Lakini hata kama ukitaka kuzifanya, basi zifanye kwa hesabu kali ili uaminike.

Huyu Mchome ndiye aliyeishtaki CHADEMA kwa msajili, akasababisha sekretarieti yote ya CHADEMA ikafungiwa. Leo anajitokeza kama kiongozi wa propaganda za kumtuhumu Heche, ataamika kweli?

Mchome, kama walivyo Said Issa Mohamed na Ahmed Rashid Khamis mpaka sasa, kwenye macho ya walio wengi huku mtaani wanaaminika ni maadui wa CHADEMA na wasaliti wa chama chao.

Katika mazingira ambayo marehemu Sulemani Bungara na Maulida Anna Komu wote kabla hawajafa walitoa tuhuma ambazo mpaka leo hazijakanushwa, kuwa msajili wa vyama vya siasa ndiye anayewatumia wanachama wa upinzani kuvuruga vyama vyao, mfano ukitajwa kuwa ni hiyo kesi ya CHADEMA ya mgawanyo wa mali; kama kweli mtu unapanga kuichafua CHADEMA kimkakati, huwezi watumia watuhumiwa!

Nadhani ifike mahali turejee kwenye siasa za maswala kuliko hizi sarakasi za maji taka. Mpaka sasa siamini kama CCM inashindwa kuwakabili wapinzani wake kwa hoja nzito zitakazowaletea wananchi matumaini badala ya hizi hoja nyepesi.
 
Apambane na chama chake cha ubwabwa.
GrdjneFX0AAnofj.jpg
 
Lembrus Mchome ana hoja nzito inayostahili kujibiwa kitaalamu na kamati kuu ya CHADEMA. Ila Mnyika kabebeshwa mzigo mzito wa kuwa katibu mkuu wa chama ambacho makamu mwenyekiti ni fisadi wa michango ya matajiri. Mnyika ni mwanasiasa ambaye ana siasa za kistaarabu na hajawahi kutajwa kutafuna pesa za chama kama kina Heche, Lema na Sugu. Kitu pekee cha kipuuzi ninachokumbuka kuhusu Mnyika ni pale aliposema Rais Jakaya ni dhaifu bungeni. Lilikuwa tusi baya sana.
 
1. Kuna utaratibu wa kuchangia chama, ambao unajulikana na michango yote huingizwa kwenye account ya chama.
2. Pamoja na kuchangia chama mtu binafsi anaweza kumpa hela kiongozi au mwanachama yoyote kwa matumizi ambayo wamekubaliana wao wawili. Ikitokea fedha hizo hazijatumika ipasavyo anaye paswa kulalamika ni aliye toa.
3. Hata viongozi wa CCM, wagombea mbalimbali wa CCM huchangiwa fedha na wafanyabiashara ambazo hawazifilkishi kwenye account ya chama. Huzitumia wao kama wao kwenye kampeni na mambo mengi.
4.Mchome kutokana na historia yake ya kusema uongo dhidi ya CHADEMA kwa malengo ya kuofifisha hawezi kuaminika katika hili.
 
Lembrus Mchome ana hoja nzito inayostahili kujibiwa kitaalamu na kamati kuu ya CHADEMA. Ila Mnyika kabebeshwa mzigo mzito wa kuwa katibu mkuu wa chama ambacho makamu mwenyekiti ni fisadi wa michango ya matajiri. Mnyika ni mwanasiasa ambaye ana siasa za kistaarabu na hajawahi kutajwa kutafuna pesa za chama kama kina Heche, Lema na Sugu. Kitu pekee cha kipuuzi ninachokumbuka kuhusu Mnyika ni pale aliposema Rais Jakaya ni dhaifu bungeni. Lilikuwa tusi baya sana.
Aliwahi kukanusha kupangishiwa Nyumba masaki na Francis Mutungi?
 
Huyu mchome alishindwa nini kuwasilisha malalamiko yake kupitia utaratibu maalum uliopo ndani ya chama?
 
Mchome kama mbabe kweli aikosoe ccm, hapo nitajua kweli halipwi kuchafua watu
Gentleman,
huyo kijana ana detailed information za chadema pekee.

Halafu anawezeja kukikosoa chama kisichomuhusu na asichokua na detailed information kukihusu?

muulize malaya wa kisiasa mchungaji Msigwa atakwambia hicho chama kipoje 🤣
 
Back
Top Bottom