Binafsi sio muumini wa siasa za maji taka! Lakini hata kama ukitaka kuzifanya, basi zifanye kwa hesabu kali ili uaminike.
Huyu Mchome ndiye aliyeishtaki CHADEMA kwa msajili, akasababisha sekretarieti yote ya CHADEMA ikafungiwa. Leo anajitokeza kama kiongozi wa propaganda za kumtuhumu Heche, ataamika kweli?
Mchome, kama walivyo Said Issa Mohamed na Ahmed Rashid Khamis mpaka sasa, kwenye macho ya walio wengi huku mtaani wanaaminika ni maadui wa CHADEMA na wasaliti wa chama chao.
Katika mazingira ambayo marehemu Sulemani Bungara na Maulida Anna Komu wote kabla hawajafa walitoa tuhuma ambazo mpaka leo hazijakanushwa, kuwa msajili wa vyama vya siasa ndiye anayewatumia wanachama wa upinzani kuvuruga vyama vyao, mfano ukitajwa kuwa ni hiyo kesi ya CHADEMA ya mgawanyo wa mali; kama kweli mtu unapanga kuichafua CHADEMA kimkakati, huwezi watumia watuhumiwa!
Nadhani ifike mahali turejee kwenye siasa za maswala kuliko hizi sarakasi za maji taka. Mpaka sasa siamini kama CCM inashindwa kuwakabili wapinzani wake kwa hoja nzito zitakazowaletea wananchi matumaini badala ya hizi hoja nyepesi.