Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Mwanga, Mchome Lemburus, ameiomba Serikali na mamlaka husika kumuachia Mwenyekiti wa CHADEMA,, akidai kuwa chama hicho kinamhitaji ili kurejea kuongoza shughuli zake na kusaidia kutatua changamoto zinazokikabili.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mchome alisema anaamini kuwepo kwa Lissu nje ya gereza kutasaidia kurejesha utulivu na mshikamano ndani ya CHADEMA, akieleza kuwa migogoro na mivutano inayojitokeza kwa sasa isingekuwepo kama mwenyekiti huyo angekuwa huru.
Alidai kuwa kesi inayomkabili Lissu haina msingi, hivyo akaishauri Serikali kuona umuhimu wa kumwachia ili arejee kwa familia yake pamoja na kuendelea na majukumu yake ya kisiasa ndani ya chama.
"Hivyo naiomba Serikali na mamlaka husika zione busara ya kumuachia Mheshimiwa Tundu Lissu. Tunamhitaji atuongoze katika mapambano ya kisiasa na kuendelea kujenga chama," alisema.