Mchome: Serikali imwachie Tundu Lissu, amekaa gerezani mwaka mmoja na nusu kwa kesi ya mchongo

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Mwanga, Mchome Lemburus, ameiomba Serikali na mamlaka husika kumuachia Mwenyekiti wa CHADEMA,, akidai kuwa chama hicho kinamhitaji ili kurejea kuongoza shughuli zake na kusaidia kutatua changamoto zinazokikabili.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mchome alisema anaamini kuwepo kwa Lissu nje ya gereza kutasaidia kurejesha utulivu na mshikamano ndani ya CHADEMA, akieleza kuwa migogoro na mivutano inayojitokeza kwa sasa isingekuwepo kama mwenyekiti huyo angekuwa huru.

Alidai kuwa kesi inayomkabili Lissu haina msingi, hivyo akaishauri Serikali kuona umuhimu wa kumwachia ili arejee kwa familia yake pamoja na kuendelea na majukumu yake ya kisiasa ndani ya chama.

"Hivyo naiomba Serikali na mamlaka husika zione busara ya kumuachia Mheshimiwa Tundu Lissu. Tunamhitaji atuongoze katika mapambano ya kisiasa na kuendelea kujenga chama," alisema.

Your browser is not able to display this video.
 
Hivi huyu ndio alipiga picha gari la dgi tiss Msuya kisha akapotezwa Kwa muda?
 
Gentleman,
hakuna muhalifu au mtuhumiwa wa uhaini atakae achiwa huru kutoka korokoroni hata kwa sekunde moja tu, bali mahakama huru za Tanzania zitatoa haki kulingana na makosa ya mtuhumiwa au muhalifu husika.

hakuna haja ya kumbwelambwela vitu useless kuhusu wahalifu wanaosota korokoroni na wenye kesi za kujibu mahakamani πŸ’
 
Huyu aliyepangishiwa apartment na Msajili wa vyama ili atumike kuihujumu Chadema anafikiri tumesahau unafiki wake?
 
Siyo CHADE
SIYO CHADEMA tu,Lissu TANGANYIKA NA WATANGANYIKA WENYE AKILI TIMAMU WOOOOTE TUNAMUHITAJI.
 
nenda basi ukawasaidie akina KATUGA maana hawajui hata cha kuongea mahakamani!
TAL anawakata na kuwafunua kila kukicha hadi wanalazimishwa kuja mahakamani!
 
nenda basi ukawasaidie akina KATUGA maana hawajui hata cha kuonge amahakamani!
TAL anawakata na kuwafunua kila kukicha hadi wanalazimishwa kuja mahakamani!
hawapigi mayowe na kurusha ngumi kama yule muhalifu mtibua minywele kama wendawazimu mahakamani?🀣
 
Punga lao kwenye ubora wako tingisha kiuno tukuone msemaji wa WACHAWI.tanzania
 
Huyu ni mnafiki mkubwa. Mchome mwenye akili ni Mchome Mapovu tu
Kesho beba bango lenye maandishi yafuatayo.

Hatuna Nchi nyingine zaidi ya Tanzania.
Tuilinde amani ni mtaji wetu,
Tuitunze,
Tusikilizane,
Tuheshimiane,
Tushikamane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…