PreGE2025 Mchome wa Chadema atangaza kugombea Ubunge bila kujali harakati za "no reforms, no election"

PreGE2025 Mchome wa Chadema atangaza kugombea Ubunge bila kujali harakati za "no reforms, no election"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mwenyekiti mstaafu BAVICHA mkoa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa wilaya ya Mwanga Lembrus Mchome ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge bila kujali harakati za Chama chake, CHADEMA za kuzuia Uchaguzi kama hakutakua na Mabadikiliko.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X, Mchome mwanachama wa CHADEMA kupitia mtandaowa X (Twitter) ameandika

"Maridhiano yalikua ni maamuzi ya chama na yalipitishwa na baraza kuu la chama na watu walitoka hadharani na kupinga kwa uhuru kabisa. No reform No election ni maamuzi ya chama na yalipitishwa na baraza kuu kwanini iwe haramu kupinga?. Binafsi ntagombe ubunge Mwanga mwaka huu."


Pia, Soma
Lissu ni dikteta wa waziwazi
 
Wilaya ya Mwanga hakuna mtu wa kuiangusha CCM .
Angalau kidogo Hendry Kileo aliisumbua CCM mwaka 2015 .
Lakini aliishia kuangukia pua .

Mwanga Bila vyama vya upinzani kuungana hawana ubavu wa kuishinda CCM .
Huyo mchome anatafuta jina tu ili CCM wamnunue .
Jambo la kusikitisha ni kwamba No reform no Election ni Tamko la Chama wakati Mbowe alipokua Mwenyekiti .
Ila Mbowe naye anatakiwa ajitokeze hadharani kumuunga mkono Mwenzake .
Wakati Mbowe alipokua Mwenyekiti Lisu alimuunga mkono kwa nguvu zote mpaka akapigwa risasi tena akiwa tu mjumbe wa halmashauri kuu . Leo Mbowe anashindwa hata kushirikiana na Mwenzake katika harakati za kutafuta tume huru ili kutimiza kile alichokianzisha mwenyewe?

Kundi la Mbowe kukubali tu kuwa wakati wa Siasa za kilaghai umekwisha .
Mwaka 2020 walimtoa chambo Lisu ili agombee maana waliogopa siasa za JPM .
Lisu alampeleka JPM mchakamchaka wa kufa mtu . Ikabidi wizi wa kura ufanyike ili kuinusuru CCM pamoja na kwamba JPM alikua mzalendo lakini bado uchaguzi ulikua ni mgumu kwa CCM .
Mwaka huu Mbowe anaona wivu kuwa Lisu anaungwa mkono na wananchi wote bila kujali vyama vyao. Lakini kinachomshtua Mbowe zaidi ni Dr.Slaa kurudi na ACT kuikubali mikakati ya kudai marekebisho ya sheria za uchaguzi lakini pia Viongozi wa dini kuonekana kutaka uchaguzi ufanyike kwa haki.
Badala ya Mbowe kumuunga mkono Lisu kwa maana kwamba mefanikiwa kushawishi umma yeye anafanya mgomo baridi.
Lisu angeachia siasa baada ya kupigwa risasi leo Chadema ingeku dhaifu sana maana kuna wakati Mbowe alikua anatumia tukio la Lisu kupigwa risasi kama kiki ya kisiasa.
Point sn
 
Mwenyekiti mstaafu BAVICHA mkoa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa wilaya ya Mwanga Lembrus Mchome ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge bila kujali harakati za Chama chake, CHADEMA za kuzuia Uchaguzi kama hakutakua na Mabadikiliko.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X, Mchome mwanachama wa CHADEMA kupitia mtandaowa X (Twitter) ameandika

"Maridhiano yalikua ni maamuzi ya chama na yalipitishwa na baraza kuu la chama na watu walitoka hadharani na kupinga kwa uhuru kabisa. No reform No election ni maamuzi ya chama na yalipitishwa na baraza kuu kwanini iwe haramu kupinga?. Binafsi ntagombe ubunge Mwanga mwaka huu."


Pia, Soma
Kwamba anatangaza kugombea ubunge si kwa nia ya kuupata bali kuonesha umwamba wa kupinga No reforms No election. Wanazidi kujianika.
 
Kama haeshimu msimamo wa chama basi avuliwe.uanacha/ afukuzwe kabisa.
 
Back
Top Bottom