Paukwa pakawa.
Hicho sicho kibuyu cha kwanza kushindanishwa na FUNDI aliye kichonga,kuna vibuyu vingine vitatu vilichongwa na mafundi wengine,ili wamshushe huyo FUNDI lkn mwisho wa siku FUNDI aliwazidi kila kitu.
Sasa hivi hao mafundi wameamua kukipa sapoti hicho kibuyu kilicho chongwa na FUNDI ili wajaribu kumtetemesha FUNDI lkn bado hicho kibuyu hata robo ya mafanikio na number alizokuwa akizipata FUNDI ndani na nje ya nchi hajawahi kufikia.
Hata hicho kibuyu ukikipima na vibuyu vingine in terms of numbers still vibuyu hivyo vya huyo FUNDI bado vipo juu.Ndipo unagundua ni maneno matupu kwani hicho kibuyu na hao mafundi wanao msapoti wamebaki na maneno na chuki kwa FUNDI.
Hao mafundi wanakipa promo hiko kibuyu wakizani watamkomoa FUNDI kumbe wanaviumiza vibuyu vingine kabisa,kwani FUNDI anajitosheleza kwa kila kitu yeye na vibuyu vyake alivyo vichonga.
Hicho kibuyu kinalalamika kinabaniwa,cha ajabu anapata promo ktk maeneo matatu yanayo milikiwa na mafundi,ambayo alikuwa hayapati kipindi yupo chini ya FUNDI wakati yy FUNDI na vibuyu vyake wanapata promo ktk eneo moja still wanafanya vizuri.