Hii picha ina tafsiri kubwa sana. Naomba tutafakari hapa kwa pamoja.
1. Dishi lina bendera ya Tanzania na lina maji. Hapa anawakilisha nchi ya Tanzania na watu wake.
2. Mwenye nguo nyeusi ni mzazi na mwenye kilemba ni mtoto. Huyo mtoto anachezea maji ndani ya dishi. Hapa inaeleweka zaidi.
3. Maji yanakanyagwa na mtoto mwenye kilemba pamoja na mtu wa nguo nyeusi. Yaani hapa sheria za nchi zinasiginywa/kukanyagwa.
4. Mtu wa nguo nyeusi anawaambia wananchi watulie nchi inaongozwa vizuri. Hapa anawatoa hofu wananchi ya kuwa kila kitu kipo pouwa kabisa, hivyo waondoe maulizo na mishangao..
5. Wananchi wameshika vichwa vyao. Inaonekana wananchi hawamuelewi kabisa huyo mtu, yaani wanashangaa na kujiuliza bila ya majibu yoyote.