Mchumba 'angu amemegwa halafu ka confess

Mchumba 'angu amemegwa halafu ka confess

two wrongs do not make a right hata siku moja,,kama ukiwaza na kuwazaua unaona hauwezi kumwamini tena anza mapema usipoteze muda zaidi
 
Kama unampenda endelea nae tu maana haya masuala ya kuanzisha relationship ndani ya relationship ni vijimambo vya kawaida tu sasa utaacha wangapi wakati almost wote ndio zao hizo??

Tena wewe uchumba, hata kwenye ndoa ukisikia nyumba ndogo unadhani ni nini? ndio relationship mpya ndani ya ndoa na unamfumania unatake eazy mnaendelea na maisha, take easy msamehe endelea na maisha yako ukitaka msafi utampata wapi ndugu yangu wote ndio wale wale!

Lakini kiukweli mambo ya confession tuwaachie wazungu, sie huku kwetu uki-confess umejichongea ndio tiketi ya kuhukumiwa!!!! hata hivyo pole sana

Confession is not our culture....Huku kwetu hata mtu ukamatwe ''red-handed'' akikosea tu ukakurupuka toka kwenye eneo la tukio, kesho yake unakataa ''it wasn't me''.
 
Sijui hata nianzie wapi..... Ni takribani mwaka wa pili sasa nipo nae, na ni mwezi wa pili mwaka huu nilimtambulisha kwa wazazi wangu na ndugu kadhaa kuwa huyu ni "mchumba wangu mpendwa niliyependezwa nae".

Baada ya hapo maisha yakatuweka mbali takribani miezi mitano, lakini tulikuwa tukiwasiliana mara kwa mara... Chako ni chako tu, nilianza kuhisi mabadiliko kwenye mawaasiliano yetu na hiyo iliniumiza kichwa sana, Mungu si athumani siku isiyokuwa na jina nikapata kalikizo, nikaamua ku pay a suprise visit huko kwao...mengi yakatokea lakini la muhimu niligundua kuwa mwenzangu alianzisha mahusiano yasiyo rasmi kama mawili, akakiri kuwa ni kweli amemegwa na hao washkaji kwa muda tofauti...

Iliniuma sana zaidi aliponiambia kuwa mmoja kati ya hao jamaa alikuwa anafahamu kuwa yeye ni mchumba wa mtu na wakala njama kuwa mimi nisijue, kumbe hata nilivyokuwa napiga simu au kutuma msg alikuwa na jamaa yake tena anaipumulia...

Amejuta sana na anadai haelewi kwa nini ali kwenda astray, nimepima moyo wangu nimeamua kumsamehe kwani bado nampenda lakini nashidwa kuishi na fact kwamba jamaa kadhaa baada yangu wamepita... Na nikifikilia zile promises alizokuwa ananipa kuwa ananipenda na kamwe hawezi kuni hurt, zinanifanya nimuone Muongo kwa kila kitu....

Nisaidieni wajameni...

Anza maisha mpya tu, mwanamke wa kumegwa na wanaume wawili ndani ya miezi mitano mliyokaa mbalimbali, si ajabu huwa ana tabia ya kumegwa hata ukiwa naye, ila tu inakuwa rahisi kwake kupangilia mambo yake! Halafu wanawake sio watu wa kuwaaamini kwa 100%..Ukifanya hivyo utakuja kufa kwa presha!

There are lots of fish in the pond, achana naye!
 
duh jamaa wawili katika miezi mitano mmh mkuuu fikiria mara mbili please angekuwa kamegwa na jamaa mmoja ningesema bahati mbaya duh wawili mmmmh
 
halua haina kipolo

kwa nini upashe kipolo wakati vya kupikwa vipo??
 
Achana na huyo mchumba chichi! Heri ya mchawi kuliko mwongo.. Hakupendi huyo. Na ukienda mbali, utasikia kamegwa halafu ataconfess tena. POLE Baba!
 
Pole sana . jua ya kuwa kama alivyokueleza kuwa akupende ndivo alivyowaeleza hao wengine. basi huo ni unafiki kama sio usaliti. Wewe unaweza kuamua kuendelea nae au la. Ikiwa unaamini kuwa atabadilika is okay maana imani huzaa imani na mwishowe matendo.
 
Si imeandikwa kuwa... samehe si mara saba tu, bali saba mara sabini! Basi msamehe nawe akusamehe...!
 
Du!pole sana mshkaji, lakini naomba kuuliza, je ulimkuta bikra au alishamegwa na wengine kabla yako? Kama alivyosema jamaa hapo juu, fimbo ya mbali haiui nyoka. Haya mambo hutokea sana na hata kwenye ndoa. Wewe hujawahi kuchapa pembeni? Kama mmesamehana na mnapendana, unaweza kumuoa tu, hamna shida, si kweli kwamba wote wanaooana hawajawahi kupatwa vikwazo, kwani kuna wengine huwa wanafumaniana kabisa kitandani, sembuse wewe wa kuambiwa na ku-confess tu. Isikupe taabu baba, Haya ni ya akina kurumbizi, changanya na yako. Dunia ya sasa huwezi kumpata wa peke yako. Habari ndiyo hiyo!
 
Iliniuma sana zaidi aliponiambia kuwa mmoja kati ya hao jamaa alikuwa anafahamu kuwa yeye ni mchumba wa mtu na wakala njama kuwa mimi nisijue, kumbe hata nilivyokuwa napiga simu au kutuma msg alikuwa na jamaa yake tena anaipumulia...
Kaka,
Hapo unapoteza muda wako. Msamehe lakini najua hata ukimuoa kidonda hicho hakiponi. Utakuwa unahisi kama atakusaliti tu muda wowote.

Ushauri: piga moyo konde, achana nae! Huyo siyo wa tabia yako.

Jipe moyo, vumilia...ni mapito tu hayo!
 
piga chini usihofu wanawake wapo wengi ni sawa ulimpenda sana
lakini kwa ayo aliyokutendea huna jinsi uyo ni mtu wa tamaa na isitoshe
miezi 5 ni midogo sana kwa yeye kutovumilia
 
Msamehe kisha chukuwa hatua, peleka posa kwao ili uhalalishe kabisa kuwa ni wako peke yako.
 
kama UMEMUA KUSAMEHE! NI LAZIMA UJIFUNZE KUSAMEHE KUTOKA MOYONI; Kutosahau ni kawaida lakini usichukulie kutosahau kama fimbo; yaani akila atakachokosea wewe inakuwa kazi yako Kukumbushia tuuuu!
Pili kumwamini kwako inategemea na yeye mwnyewe kwa kiasi kukubwa ameupokeajae nafanyaje kuahakikisha she wins you back yaani ziwepo juhudi zenu nyote wawili!

Wewe unayo haki ya kuumia lakini pia utafakari kama kunyoa ama kusuka kama wadau walivyokushauri hapo ; lakini pia uwe mkweli weye huja duumisha mila kidogo huko uliko?
 
Kama utafuata ushauri wa hili jamvi ndg Chichi huyo m/mke mpige Chini.........
 
mtu akimmega demu wako na wewe tafuta mnyonge mmegee.hiyo haipunguzi maumivu ila inarudisha hadhi ya kiume.habari ndiyo hiyo.
 
...Chichi mwenyewe kaingia mitini. Nachelea kuwaza kuwa amepata scholarship ya miaka miwili USA na mamaa kabaki Bongo....!:whistle:
 
Wahenga walisema kuwa... Embe mbivu yaliwa kwa uvumilivu
 
Sijui hata nianzie wapi..... Ni takribani mwaka wa pili sasa nipo nae, na ni mwezi wa pili mwaka huu nilimtambulisha kwa wazazi wangu na ndugu kadhaa kuwa huyu ni "mchumba wangu mpendwa niliyependezwa nae".

Baada ya hapo maisha yakatuweka mbali takribani miezi mitano, lakini tulikuwa tukiwasiliana mara kwa mara... Chako ni chako tu, nilianza kuhisi mabadiliko kwenye mawaasiliano yetu na hiyo iliniumiza kichwa sana, Mungu si athumani siku isiyokuwa na jina nikapata kalikizo, nikaamua ku pay a suprise visit huko kwao...mengi yakatokea lakini la muhimu niligundua kuwa mwenzangu alianzisha mahusiano yasiyo rasmi kama mawili, akakiri kuwa ni kweli amemegwa na hao washkaji kwa muda tofauti...

Iliniuma sana zaidi aliponiambia kuwa mmoja kati ya hao jamaa alikuwa anafahamu kuwa yeye ni mchumba wa mtu na wakala njama kuwa mimi nisijue, kumbe hata nilivyokuwa napiga simu au kutuma msg alikuwa na jamaa yake tena anaipumulia...

Amejuta sana na anadai haelewi kwa nini ali kwenda astray, nimepima moyo wangu nimeamua kumsamehe kwani bado nampenda lakini nashidwa kuishi na fact kwamba jamaa kadhaa baada yangu wamepita... Na nikifikilia zile promises alizokuwa ananipa kuwa ananipenda na kamwe hawezi kuni hurt, zinanifanya nimuone Muongo kwa kila kitu....

Nisaidieni wajameni...
hapo ndio tunapokosea,utakufa wewe anza mbele achana nae,nampenda,nampenda mapenzi bongo yaliisha siku nyiiiingi.
 
Back
Top Bottom