Mchumba 'angu amemegwa halafu ka confess

Mchumba 'angu amemegwa halafu ka confess

Nataka kuuliza swali wenzangu. Hivi katika kipindi hicho mchumbake hayupo na yeye aliwamega wangapi?
 
Chichi, nakushauri uachane na mchumba huyo. Katika wakati wa mahusiano ambapo kila mmoja huchunga mambo yasiharibike ni wakati wa UCHUMBA. Kama mtu wako kamegwa wakati wa UCHUMBa wakati wa NDOA ndipo atazaa nao kabisa!!! Achana naye, usilee ugonjwa; asiyesikia la Mkuu huvunjika guu.......
 
Yani mshkaji mpenzi wako amemegwa wakati wa u-boyfriend na u-girlfriend alafu umeamua kumsamehe mbona hiyo haijakaa vizuri? kwa kuwa si mkeo mimi nakushauri uachane nae kwani atakupa ugonjwa wa moyo bure. Kwa mtu anae kupenda ni vigumu sana kufanya mapenzi na mtu mwingine ndani ya uhusiano wenu.

Kisha Petro akamwendea, akamwuliza, "Bwana je, ndugu yangu akinikosea, nimsamehe mara ngapi? Mara saba?"
Then came Peter to him, and said, Lord, how oft shall my brother sin against me, and I forgive him? till seven times?

Yesu akamjibu, "Sisemi mara saba tu, bali sabini mara saba.
Jesus saith unto him, I say not unto thee, Until seven times: but, Until seventy times seven.

Math 18:21-22

Mtenda na mtendewa wana haki ya kusameheana... as long as hawaja'oana..kwa maana wote wapo kwenye matendo hayo hayo ya kumegana kabla ya ndoa... kwa ujumla wote ni wakosa.
 
ACHANA NAYE..
Utakuwa unafukiria kila siku jinsui alivyorambwa na hao jamaa
 
Miezi mitano kamegwa na wawili, mbona balaa? Nakushauri hivi mkubwa, KIMBIA, msala huo!
 
Kama na wewe una uhakika hukumega huko ulikokuwa then wewe ni mwaminifu na huna budi kuachana na huyo kicheche, tena haraka sana. Lakini naona habari hii ni ya muda mrefu, pengine atakuwa ameshaachana naye, Vinginevyo, tunakuomba utupe update ya mahusianao yenu kwa sasa!!!!
 
inaonekana unampenda sana mchmba wako na ameshajua hilo. Atakutesa sana. achana nae ndg yangu
 
sijui hata nianzie wapi..... Ni takribani mwaka wa pili sasa nipo nae, na ni mwezi wa pili mwaka huu nilimtambulisha kwa wazazi wangu na ndugu kadhaa kuwa huyu ni "mchumba wangu mpendwa niliyependezwa nae". Baada ya hapo maisha yakatuweka mbali takribani miezi mitano, lakini tulikuwa tukiwasiliana mara kwa mara... Chako ni chako tu, nilianza kuhisi mabadiliko kwenye mawaasiliano yetu na hiyo iliniumiza kichwa sana, mungu si athumani siku isiyokuwa na jina nikapata kalikizo, nikaamua ku pay a suprise visit huko kwao...mengi yakatokea lakini la muhimu niligundua kuwa mwenzangu alianzisha mahusiano yasiyo rasmi kama mawili, akakiri kuwa ni kweli amemegwa na hao washkaji kwa muda tofauti... Iliniuma sana zaidi aliponiambia kuwa mmoja kati ya hao jamaa alikuwa anafahamu kuwa yeye ni mchumba wa mtu na wakala njama kuwa mimi nisijue, kumbe hata nilivyokuwa napiga simu au kutuma msg alikuwa na jamaa yake tena anaipumulia... Amejuta sana na anadai haelewi kwa nini ali kwenda astray, nimepima moyo wangu nimeamua kumsamehe kwani bado nampenda lakini nashidwa kuishi na fact kwamba jamaa kadhaa baada yangu wamepita... Na nikifikilia zile promises alizokuwa ananipa kuwa ananipenda na kamwe hawezi kuni hurt, zinanifanya nimuone muongo kwa kila kitu.... Nisaidieni wajameni...

watu wakikumegea demu wako na wewe tafuta mnyonge wako ummegee
 
naomba nisiwe mnafiki wala mwenye chembe chembe ya double standards. Maana wengi humu tunaongea kwa nadharia sana.

Nikigundua kwamba mke/demu wangu kamegwa na jamaa mwingine: from the bottom of my heart that will be the end of our relationship. Hata kama ni mke nimekaa naye kwa miaka mingapi.

Ofcourse ni tofauti kama alimegwa hajaanza mahusiano na mimi.

Wengine watauliza: Na yeye je akigundua kama wewe umecheat? Well, hilo namwachia yeye. Kama nikimuomba msamaha akakubali au nika-mconvince kunisamehe akakubali, thats good. Ila ana haki ya kuchukua uamuzi aupendao.

Hili kwangu kwa kweli halina mjadala. Nitamwambia: Mama/dada naomba kwa leo safari yetu ya uhusiano/ndoa iishie hapa.
 
naomba nisiwe mnafiki wala mwenye chembe chembe ya double standards. Maana wengi humu tunaongea kwa nadharia sana.

Nikigundua kwamba mke/demu wangu kamegwa na jamaa mwingine: from the bottom of my heart that will be the end of our relationship. Hata kama ni mke nimekaa naye kwa miaka mingapi.

Ofcourse ni tofauti kama alimegwa hajaanza mahusiano na mimi.

Wengine watauliza: Na yeye je akigundua kama wewe umecheat? Well, hilo namwachia yeye. Kama nikimuomba msamaha akakubali au nika-mconvince kunisamehe akakubali, thats good. Ila ana haki ya kuchukua uamuzi aupendao.

Hili kwangu kwa kweli halina mjadala. Nitamwambia: Mama/dada naoMBa kwa leo safari yetu ya uhusiano/ndoa iishie hapa.

hujui kupenda wewe.
kajifunze kwa wazazi wako au aged couples wakusimulie mauzauza yao ndipo utakapogundua kuwa kumega mego kavu halizuii utafunaji
 
hujui kupenda wewe.
kajifunze kwa wazazi wako au aged couples wakusimulie mauzauza yao ndipo utakapogundua kuwa kumega mego kavu halizuii utafunaji

Mkuu wewe sasa unaleta utani.

Anayekwambia hivyo ni mimi Masanja, sasa kama una definition ya kupenda unayoijua wewe. Its you.

Just do you, I do me.

Masanja,
 
Mkuu wewe sasa unaleta utani.

Anayekwambia hivyo ni mimi Masanja, sasa kama una definition ya kupenda unayoijua wewe. Its you.

Just do you, I do me.

Masanja,

huna mapenzi zaidi ya WIZI MTUPU.
mke akimegwa inauma sana ila shida huwezi kumuacha kijinga hivyo. kama umeoa unamega mara ngapi nje??
wizi mtupu
 
kaka chichiii..pole sana kijana..kwani angekuwa ni mkeo ungefanyaje?....na padre ashasema kifo ndicho kitawatenganisha??....sasa kwa taarifa yako hata kama padre kasema ...kitendo cha kumfumania and worse enough amekiri wazi kuwa aliliwa uroda basi huna budi kumwaga...huyo ni mke...kwa hoja yako ya MCHUMBA....wala hata huitaji kujiumiza kichwa fastaaaa...mwambie achape mwendo wapo mademu kama millioni 25 hivi wanalia mingo wanaume kama wewe. kwann uumize kichwa kijana wangu...vaa maamuzi ya kiume mwageee...ila ukiendekeza mambo ya kitozi ukaingia naye kwenye ndoa utashangaa anawaleta mabasha zake hata nyumbani kwako na wanam-perform wewe unaona..ndioo...si umeukubali uzezeta hata kabla hujamwoaaaa.??....am out man
 
Du hayo mambo fomula yake aijua muumba.Tatizo la hawa kina dada wanafanya maamuzi kabla ya kujihakikishia kweli wamefika.Wanapomuona kijana anafananafanana ya takwa lao wanamua kujiingiza huku wakijua kesho watamuona mwingine na kuona kuwa anamfaa zaidi.Hasa hawa wa vyuoni.Anakuwa na boyfriend na wanawekeana promise kibao,chuo kinapoisha wanaingia mitaani wakikutana na wanaume wengine wanaona ndo anafaa zaidi ya yule alokuwa nae.Ushawahia kusikia msichana anabanjuliwa siku moja kabla na baada ya send off nwa mwanaume tofauti na mchumba wake?Imetoke tena siku si nyingi na hata anapigiwa simu akiwa ktk mechi.

Dada zetu nawaambia mkiamua jambo muwe mumeamua kwelikweli sio kama pusi na panyas
 
whenever there r two devils, you choose the less one... kusamehe kuna machungu yake a kuacha kuna machungu yake bro...! angalia maamuzi yenye manufaa kwako... tumia utashi wako... na hatimye uamue... BE A MAN.. STAND IN YOUR PRINCIPLES!!!!!!
Pole sana, hay ndio maisha yetu ya leo!
 
Chichi,
Muda wa kukaa katika uchumba sio kusubiri na kufanya maandalizi ya arusi la hasha, muda wa uchumba hasa wakati ule wa MWL ni kuchunguzana kati ya wachumba, kuifahamu vilivyo familia atokayo mchumba wako, historia yao kwani kuna mambo mengi yanayoonyeshwa na mchumba kutokana na background yao mfano: baadhi ya magonjwa, tabia za ajabu ajabu (wizi, majivuno, ujeuri, ugomvi, kutovumilia n.k). Na si mambo mabaya tu pia 'positives' alizonazo mchumba lazima uzichunguze then mtakapooana unaweza kuzitumia katika kuleta maendeleo katika familia yenu.

Kwa vile muda wa uchumba kwako umedhihirisha kasoro kwa mwenzako, kinachofuata ni namna ya kulitafutia ufumbuzi ambao kwa sasa umewaomba wanaJF wakusaidie. Mimi nasita kukuamulia. Lakini nimejenga mazingira ili uamue wewe mwenyewe na uamuzi wako utakaoufanya ukusute/ukufaidishe hapo baadae. Maelezo yako umesema ulimsamehe, mimi nasema haujamsamehe, maana ungemsamehe usingelileta suala hili tena hapa barazani na kuomba msaada. Nikutakie kila la kheri katika kulimaliza suala hili. Zingatia ushauri wa wanaJF, lakini sio lazima uufuate, mikuki unayo mikononi mwako.
 
Kusamehe na kuendelea kuwa nae ni vitu viwili tofauti, hivyo na kushauri umsamehe lakini kamanda kama ni kunguru hawezi kufugika achana naye,huo msalaba huuwezi ni mzito mwanangu.
 
Last edited:
Chichi huyo mchumba wako nakushauri achana nae. Kama anaweza megwa kwenye uchumba, ktk ndoa si ndo itakuwa balaa? Amini usiamini huyo au hao jamaa wanaommega anawapenda vilevile, na anaweza endeleza nao libeneke hata ukishamwoa, na hapo unaweza kuja kujinyonga mzee!!!! Anza, tafuta mwingine
 
Back
Top Bottom