Mchumba hasomeshwi? Simulizi ya kutisha na kuumiza

Mchumba hasomeshwi? Simulizi ya kutisha na kuumiza

Patrick Oita Nyapara, ambaye ni police nchini Kenya alimuua mpenzi wake kwa kumtandika Risasi 47 baada ya binti huyo kumkataa, pindi alipomaliza masomo Chuo Kikuu.
Kwa maelezo ya Patrick ni kwamba alimchukua mdada huyo aliyejulikana kwa jina la Christine Maonga kutoka katika familia duni kijijini na kumpeleka mjini Nairobi kama mke wake ambapo aliamua kumsomesha mpaka chuo kikuu.

Alikuwa akimlipia karo na mahitaji mengine pamoja na kutuma pesa kwa mama mzazi wa binti huyo kama msaada kutokana na familia hiyo kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za maisha.

Baada ya kuhitimu masomo yake, Christine alimwambia Patrick kuwa amechoka kuwa naye kwani ni mtu asiyekuwa na hadhi yoyote na hafai kuwa mpenzi wake hivyo ni vyema kila mtu afanye mambo yake.

"Nimepata mpenzi mwingine ambaye ananifaa sana pia ni Mkurugenzi wa Kampuni moja kubwa sana jijini Nairobi hivyo siwezi kuwa na wewe Patrick mtu usiyekuwa na future na ni daraja D ambalo ni dhaifu kwangu", alisema Christine.

Patrick hakuielewa kauli ya mpenzi wake, akaamua kwenda kijijini kwa mama yake na Christine kuomba msaada wa suluhu ili aweze kumuoa binti yao kwani alikuwa ametumia gharama kubwa mno kumsomesha.

Mama yake binti alijibu kuwa hawezi kumpangia mtoto wake mume wa kumuoa hivyo anapaswa aachwe ajiamulie yeye mwenyewe. Patrick hakukubali, akamtafuta dada yake Christine na kumwelezea hali halisi lakini alijibiwa kuwa hana hadhi ya kumiliki mwanamke aliyehitimu Chuo Kikuu hivyo atafute mwanamke wa level ya mgambo kama yeye.

Aliondoka na kurudi nyumbani na kuchukua uamuzi mgumu wa kumuita Christine nyumbani kwa lengo la kuongea na kumaliza tofauti zao ili waachane kabisa, binti alienda nyumbani kwa Patrick mapema zaidi. Alifika na kumkuta Patrick amejihami kwa silaha, hawakuzungumza chochote zaidi ya kumkandamiza risasi 47 na zote zikapita mwilini mwa Christine hali iliyopelekea kifo chake papo hapo. View attachment 3547879
A man should be strategic in his every move or action. Kufanya mambo kisa hisia ni tabia za kike, mwanaume mtu mzima usipende kama litoto vile, penda sawa ila weka mipaka na kwenye mapenzi utoe kitu unachoweza kupoteza
 
Wakenya nao bwana hawaishiwi vituko,sasa huyo mrembo hapa yuko wapi!!
Screenshot_2026-02-24-10-58-54-656_com.google.android.googlequicksearchbox.jpg

Ukimuangalia ana sign zote kwamba ananuka mdomo halafu kuna mtu anamwita mrembo na alimsomesha kabisa.
 
Wakenya nao bwana hawaishiwi vituko,sasa huyo mrembo hapa yuko wapi!!
View attachment 3547901
Ukimuangalia ana sign zote kwamba ananuka mdomo halafu kuna mtu anamwita mrembo na alimsomesha kabisa.
Katika yote usipende kudharau watu hapa kinachozungumziwa si uzuri wa huyu dada ni maswala ya usaliti baada ya mtu kuwekeza mda na mali
 
Hmm sasa wanandoa masikini wataishije bila watoto? Mimba zisizotarajiwa hazijapangwa, hapa tunaongelea mfano wa familia duni!
lazima tujifunze uzazi wa mpango, kuandaa asset, strategy bora za namna ya kuishi kutokana na mabadiliko ya maisha.

Hatuwezi fanya vitu vile vile, halafu tutarajie matokeo tofauti.
 
Alifanya maamuzi sahihi , nifundiso Kwa wanyonyaji wengine. Kama hupendi usipokee kitu kutoka kwake. Na usimkubali, majibu TU yanaonesha hii ni familia ya washenzi
 
Back
Top Bottom