Mchumba kakataliwa kisa shepu

Mchumba kakataliwa kisa shepu

Jamani wana Jamiiforums wenzangu nimebaki njia panda. Nilienda kumtambulisha mchumba wangu kwa wifi zake (dada zangu) juzi jumatatu huko kwetu sinza mida ya jioni baada ya kutoka kazini kwa kuwa tunafanya kazi ofisi za karibu pale posta.

Ila walichonijibu ni kuwa nitafute mwingine kwa kuwa huyu hana shape hawajampenda. Huyu mchumba angu yeye ni slander (mwembamba). Jamani naombeni ushauri wenu nifanyeje sasa nimebaki njia panda.
Sasa unachukuaje dem asiye na shepu mkuu!?
 
Back
Top Bottom