Mchumba kakataliwa kisa shepu

Mchumba kakataliwa kisa shepu

Tena tukalale barabarani pale karume!! Tukemee ubaguzi wa ki umbo.
Ila twin wanaume wa kuamuliwa na dada zao tunawahitaji kweli?

kabisaaa ........mwanaume wa hivyo tegemea kuishi kwa shida nyumba itaendeshwa na ndugu zake.
 
mmh we unaonekana ni zile type za wanaume wanaosikiliza sana ndugu zao, mwanamke utakaekuja kumuoa atapata shida sana
 
acha ushamba wewe, kila mtu na chaguo lake, wewe kama moyo wako hujampenda huyo kaka sawa, lakini eti umuache kisa mwembamba? kwani yeye alipenda awe mwembamba? kwa nini hao dada zako hawakukwambia toka zamani kuwa ikiwa unatafuta mchumba basi tafuta mnene? hadi umempotezea kaka wa watu muda wake? shauri yako tafuta laana tu!!

mtoa mada ni mwanaume, kwahiyo anaekataliwa hapo ni mwanamke
 
anza kumlisha ufuta atanenepa... pole mkuu ufanyje kwani dada zako ndo wanamuoa si wewe,... potezea kula kitu roho inapenda njoo nichukue mimi tunyenye unipeleke basi..... wewe ndo unajua kitu kilichokuvutia kwa huyo chembamba jilipue kwa kufuata ushauri wa dada zako ufe na presha ukiwa namiaka 40... wambie dada zako unene siyo dili tena , au mvalishe masponchi ya mchina ya kuongeza kalio loh... binadamu hawana heri
 
Jamani wana Jamiiforums wenzangu nimebaki njia panda. Nilienda kumtambulisha mchumba wangu kwa wifi zake (dada zangu) juzi jumatatu huko kwetu sinza mida ya jioni baada ya kutoka kazini kwa kuwa tunafanya kazi ofisi za karibu pale posta.

Ila walichonijibu ni kuwa nitafute mwingine kwa kuwa huyu hana shape hawajampenda. Huyu mchumba angu yeye ni slander (mwembamba). Jamani naombeni ushauri wenu nifanyeje sasa nimebaki njia panda.

Wape hicho wanachodhani mwenzao anafaidi!
 
eti baraka za ndugu!!! hivi kuna baraka kwenye ubaguzi? haya waambie basi wakutafutie huyo tukunyema anayefanana nao?
 
Jamani wana Jamiiforums wenzangu nimebaki njia panda. Nilienda kumtambulisha mchumba wangu kwa wifi zake (dada zangu) juzi jumatatu huko kwetu sinza mida ya jioni baada ya kutoka kazini kwa kuwa tunafanya kazi ofisi za karibu pale posta.

Ila walichonijibu ni kuwa nitafute mwingine kwa kuwa huyu hana shape hawajampenda. Huyu mchumba angu yeye ni slander (mwembamba). Jamani naombeni ushauri wenu nifanyeje sasa nimebaki njia panda.

Hao dada zako wana mashepu?je nao wao wameolewa? kama ndio vipi wako home kwenu?
 
anaye oa ni mimi ila baraka za ndugu wa tumbo moja ni muhimu sana!!

Baraka muhimu ni za wazazi tuu kwani ukianza maisha yako wao watakuwa na maisha yao pia kwahiyo kuwa na msimamo wakuwasikiliza ni wazazi,na ukioa play role yako kwa ndugu zako na kwa mkeo wenyewe wataelewa somo.
 
Back
Top Bottom