Mchumba wangu amelala na Mtu na Mama yake, je atabadilika?
Niko kwenye mahusiano na huyu kaka, huu ni mwaka wa pili. Kabla ya kukutana naye, alikuwa ameshaoa, lakini alikuja kuachana na mke wake kwa sababu alianzisha mahusiano na mama mkwe wake. Ndiyo, kaka huyo aliingia kwenye mahusiano na mama mzazi wa mke wake.
Kilichotokea ni kwamba, mimi niko huku (sitataja eneo), ambapo wanawake ni malaya sana na hawajali kuhusu kuchangia mwanaume na hata ndugu. Hivyo, kipindi mke wake alipokuwa kajifungua, mama yake alikuja kumtunza katika uzazi. Wakati wa kukaa huko, alianza mahusiano na mama mkwe wake, mpaka mtoto wa mke wake akajua.
Waligombana sana, na mama mkwe alikataa kurudi nyumbani kwa mume wake hadi kikao cha familia kilipokaa na kumlazimisha kurudi kwa mume wake. Mama mkwe alirudi, lakini bado aliendelea kumsumbua binti yake. Mwisho wa yote, binti huyo aliondoka kwa hasira, na mwanaume huyo akampa talaka.
Binti aliondoka, lakini maisha hayakumwendea vizuri, hivyo alitaka kurudi kwa mume wake. Hata hivyo, aliporudi alikuta tayari nipo kwenye mahusiano na huyo mwanaume. Kwa miaka miwili sasa,yeye na Mama yake wamekuwa wakinisumbua kwa kunivurugia amani, wakisema lazima niondoke.
Mimi nimekaa kimya kwa sababu mwanaume aliniahidi kuwa hawezi kurudiana na familia hiyo kwa sababu anaamini familia hiyo ina laana kwa kitendo walichofanya.
Sababu ya kuja kwako ni kwamba, nimemshika simu ya mwanaume na kugundua kuwa bado ana mawasiliano na aliyekuwa mke wake. Wanaitana "mke" na "mume," na wanatumiana mpaka picha za uchi. Nikimuuliza, anadai kuwa ni mambo ya mtoto. Kinachonishtua zaidi ni kwamba bado ana mawasiliano na yule mama mkwe.
Sijawahi kuona meseji za mapenzi kutoka kwa huyo mama, lakini mwanaume anamtumia pesa, anamnunulia zawadi, na nikimuuliza anadai ni kwa sababu ni mama mkwe wake na wanakaa na wajukuu zake, hivyo hawezi kumtenga.
Kwa sasa nimemchoka, na kuna wakati mama na binti yake hunipigia simu na kunitukana wakisema watafan*ya kila kitu kuniondoa. Mwanaume ananiambia nione kama wapuuzi na nipuuze maneno yao. Mwezi ujao, anatarajia kuja kujitambulisha nyumbani kwetu na kunitolea mahari, lakini naogopa sana kama huyu mtu atabadilika.