Mchumba wangu ameniuliza "Lowassa ndio nani?"

Natumaini j2 ya leo ni njema kwetu sote.

Katika harakati za kutafuta mwenza wa maisha, nimefahamiana na binti mmoja wa Kilokole ambaye ni mtoto wa Mchungaji wa moja ya Makanisa ya Kipentekoste ambapo na mimi naabudu.

Kabla sijampokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yangu, nakiri kuishi maisha yaliyotawaliwa na uzinzi na starehe za kila aina kama ulevi n.k.

Baadaye nikapata neema ya kuokoka. Nikajikuta nasali Kanisa 'X' ambamo ndio nimekutana na huyo binti wa miaka 23, mhitimu wa kidato cha 4 mwaka 2022, mrembo sana, Mcha Mungu, mwanakikundi wa kikundi cha Maombi Kanisani na muimbaji hodari wa nyimbo za Injili. Kabila ni muha.

Nina miezi 9 hapa Kanisani lakini nina miezi 2 tangu nifahamiane nae. Nimejiridhisha pasina shaka kwamba binti ni bikira. Na msimamo wake ni kwamba hatafanya zinaa mpaka siku atakayoolewa.

Baada ya kupendekeza wazo langu kwake akaomba nimpe muda wa kunichunguza. Alipojiridhisha kuhusu mwenendo wangu akaridhia ombi langu kwa sharti la kutofanya nae zinaa mpaka siku ya ndoa!

Bado hatujamshirikisha baba yake ambaye ni Mchungaji kwasababu na mimi nilimuomba anipe muda nijitafakari kama kweli niko tayari kutomuingilia kimwili kabla ya ndoa. Ukizungumza na huyu binti utagundua kwamba bado ni mshamba sana, ameshatembea mikoa 2 tu, mkoa mmoja ukiwa ni wa Shule aliyomaliza kidato cha 4.

Kwa sasa ni mjasiriamali kwasababu hakufanya vizuri kidato cha nne, malengo yake ni kusoma masomo ya uuguzi na sifa anazo.

Leo baada ya kutoka church tukaenda mahali kupata chakula cha mchana, ameniuliza swali la ajabu sana, kwamba Lowasa ni nani? Nadhani amekutana na taarifa za kifo cha Lowasa mitandaoni. At first nilidhani anatania, baadaye nikagundua alikuwa serious kwamba hamjui Lowasa!

Sasa wakuu, mwanamke wa hivi, ambaye amemaliza kidato cha 4 na amepata daraja la 3 la mwisho, inawezekanaje akawa hamjui Hayati Lowasa?

Kwa mtazamo wenu, anaweza akawa mama bora wa familia? Kiukweli ana exposure ndogo sana lakini ni mtafutaji mno. Anajielewa. Ana misimamo. Na anamtumikia Mungu katika roho na kweli.

Hebu tupeane uzoefu ili nisije nikajichanganya wakuu...
Hao wasio na akil ndo wazur..hata ukicheat unajitetea kitaalam wanaamin..braza vip wew...mbuz kafia kwa muuza supu braza
 
amekuja lini mjini? usije kumhukumu bure.
 
Aiseee. Mbona hii taarifa kama ina kuhusu wewe mwenyewe. Nikutafute umekua hela? Wewe ndio una stress aisee umenichekesha kweli[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23]

Basi tuliza mshono mkuu. Acha kujipa umuhimu kwenye maisha yangu. Zipo nyuzi nyingi tu nenda huko achana na chai yangu [emoji28][emoji28]

Wapo wenye akili timamu ambao wanaelewa ninachozungumza.

Ebo [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kama kuambiwa ni chai umeambiwa na wengi ila umenikalia mimi kooni na essay zako. Kama hukutaka nirudi ku comment si ungepotezea reply yangu, mbona umejibu ili nipate notification.😂😂😂
Tuliza wewe kitenesi
 
Mkuu ukimuoaa jiandae kuchapa watoto kisa wanakuwa wa mwisho darasanii...!! uandae urithi kabisa wa kuwapa maana wakirithi akili za mama yao elimu itawapiga chengaa sanaaa
 
Kama kuambiwa ni chai umeambiwa na wengi ila umenikalia mimi kooni na essay zako. Kama hukutaka nirudi ku comment si ungepotezea reply yangu, mbona umejibu ili nipate notification.[emoji23][emoji23][emoji23]
Tuliza wewe kitenesi
Mkuu, hebu wataje hao wengi...kama sio wewe na mwendawazimu mwenzako ambao mmekuja kwa kasi ya 5G kwenye uzi ambao hamkutakiwa kuwepo right from the start. Uzuri mwenzako amekuwa muelewa, wewe ndio unaniletea ujuaji!

Siwezi kunyamaza nikakuacha uendelee na ujinga wako.

Acha ambao wameona uhalisia ndio wa-comment, otherwise naweza kukuvunjia heshima ukanichukia maisha yako yote ingawa hatufahamiani.

Biblia imesema makwazo hayanabudi kuja, ila OLE WAO WALETAO MAKWAZO. Unanikwaza mkuu, bilashaka una mambo mengi ya kufanya, weka jitihada huko, achana na huu uzi, acha kujipa umuhimu kwenye maisha yangu.

Please!

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Tukienda kwenye interview tunaulizwa maswali ya kwenye JD na tunapewa maksi kubwa humo. Sasa mkuu muulize maswali kuhusu interest yake ndio utaweza kupima uwezo wake wa kiakili kwa uzuri.

Ukimjudge kwa hili utakuwa unamuonea. Hata hivyo watoto wanarithi akili kwa mzazi wa kike.
 
Una akili sana.

Kuna mkuu mmoja nimemjibu katika muktadha huu. Kwamba criteria ya kupima intelligence ya mtu haiwezi kuwa confined kwenye uwezo wake wa utambuzi kwenye maswala ya kisiasa tu. Yapo maeneo mengine mengi, hasa maeneo yake ya interest.

Otherwise tutamuonea binti wa watu bure tu.

Asante kwa mchango wako mkuu.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Watoto wa 2000 unakuta TV yake wasafi TV...
Ungemuuliza unamjua Baba levo?akupe history ambayo hata wewe pengine huijui..😃
Kama ulikuwepo
Kuna dogo mmoja naishi kamaliza chuo , hana ajira ila kila kukicha cha kwanza ni kufungua wasafi tv 😃
 
Natumaini j2 ya leo ni njema kwetu sote.

Katika harakati za kutafuta mwenza wa maisha, nimefahamiana na binti mmoja wa Kilokole ambaye ni mtoto wa Mchungaji wa moja ya Makanisa ya Kipentekoste ambapo na mimi naabudu.

Kabla sijampokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yangu, nakiri kuishi maisha yaliyotawaliwa na uzinzi na starehe za kila aina kama ulevi n.k.

Baadaye nikapata neema ya kuokoka. Nikajikuta nasali Kanisa 'X' ambamo ndio nimekutana na huyo binti wa miaka 23, mhitimu wa kidato cha 4 mwaka 2022, mrembo sana, Mcha Mungu, mwanakikundi wa kikundi cha Maombi Kanisani na muimbaji hodari wa nyimbo za Injili. Kabila ni muha.

Nina miezi 9 hapa Kanisani lakini nina miezi 2 tangu nifahamiane nae. Nimejiridhisha pasina shaka kwamba binti ni bikira. Na msimamo wake ni kwamba hatafanya zinaa mpaka siku atakayoolewa.

Baada ya kupendekeza wazo langu kwake akaomba nimpe muda wa kunichunguza. Alipojiridhisha kuhusu mwenendo wangu akaridhia ombi langu kwa sharti la kutofanya nae zinaa mpaka siku ya ndoa!

Bado hatujamshirikisha baba yake ambaye ni Mchungaji kwasababu na mimi nilimuomba anipe muda nijitafakari kama kweli niko tayari kutomuingilia kimwili kabla ya ndoa. Ukizungumza na huyu binti utagundua kwamba bado ni mshamba sana, ameshatembea mikoa 2 tu, mkoa mmoja ukiwa ni wa Shule aliyomaliza kidato cha 4.

Kwa sasa ni mjasiriamali kwasababu hakufanya vizuri kidato cha nne, malengo yake ni kusoma masomo ya uuguzi na sifa anazo.

Leo baada ya kutoka church tukaenda mahali kupata chakula cha mchana, ameniuliza swali la ajabu sana, kwamba Lowasa ni nani? Nadhani amekutana na taarifa za kifo cha Lowasa mitandaoni. At first nilidhani anatania, baadaye nikagundua alikuwa serious kwamba hamjui Lowasa!

Sasa wakuu, mwanamke wa hivi, ambaye amemaliza kidato cha 4 na amepata daraja la 3 la mwisho, inawezekanaje akawa hamjui Hayati Lowasa?

Kwa mtazamo wenu, anaweza akawa mama bora wa familia? Kiukweli ana exposure ndogo sana lakini ni mtafutaji mno. Anajielewa. Ana misimamo. Na anamtumikia Mungu katika roho na kweli.

Hebu tupeane uzoefu ili nisije nikajichanganya wakuu...
Mwanamume na utu uzima wako unaamini kabisa kuwa umeokoka? Labda nikuulize, umeokoka na nini?
 
Back
Top Bottom