MWANDENDEULE
JF-Expert Member
- May 24, 2015
- 4,099
- 7,466
Amani iwe nanyi.
Ndugu zangu nimeona vyema nije kwenu mnipe msaada wa kimawazo kwani nimechanganyikiwa kabisa hata usingizi sijapata usiku wa leo hii ni baada ya kupokea text kutoka kwa mpenzi/mke wangu mtarajiwa kuwa yuko moshi chuo cha polisi kitu ambacho kwa kweli sikutaka aende huko badala yake akasome chuo kozi yoyote ambayo angependa mwenyewe kutokana elimu yake (kidato cha nne).
Kaenda CCP bila kuniaga japokuwa najua alifanya usaili na kapata nafas ila baadae tulikaa tukakubaliana nimtafutie chuo na kweli nikafanya hivyo na chuo nikawa nimepata na alitakiwa aripoti chuo jumatatu (14/09/'15). Wakati mimi nafanya maandalizi yake ya kwenda chuo aliniaga aende kumuaga shangazi yake Mwanza nikamruhusu, cha ajabu amefika huko (nilivyokuwa naamini kaenda mwanza) kawa hapatikan hewani mimi nikajipa matumaini kuwa ni tatizo la chaji kwa kuwa sehemu nyingi zinakabiliwa na kukatika katika kwa umeme nchini.
To my surprise, usiku wa leo nikapata sms kutoka namba ngeni ila nikajua ni yeye kwani niko nae yeye pekee, baada ya kuchati nae kidogo kaniaga akisema, " kwa heri baby, kuwasiliana hadi mwakani"Sikujali maneno yake ila karudia tena kusema ndo nikamwuliza kulikon akaanza kwa kuomba msamaha kisha akasema, "niko Moshi CCP". Nilihisi kuchanganyikiwa na siko vizuri kimawazo saivi kwani sina imani kama atarudi salama baada ya mafunzo.
Ndugu, naomba mnipe mwanga kuhusiana na usalama wa watoto wa kike huko chuoni na uwezekano wa raia wa kawaida kumwoa askari kama huyo. Au ndo nianze mchakato wa kumtafuta mrithi wake? Kingine askari anaruhusiwa kuolewa baada ya mda gani tangu ahitimu mafunzo ama aanze kazi?