Mchumba wangu kaenda chuo cha polisi

Mchumba wangu kaenda chuo cha polisi

MWANDENDEULE

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2015
Posts
4,099
Reaction score
7,466
Amani iwe nanyi.

Ndugu zangu nimeona vyema nije kwenu mnipe msaada wa kimawazo kwani nimechanganyikiwa kabisa hata usingizi sijapata usiku wa leo hii ni baada ya kupokea text kutoka kwa mpenzi/mke wangu mtarajiwa kuwa yuko moshi chuo cha polisi kitu ambacho kwa kweli sikutaka aende huko badala yake akasome chuo kozi yoyote ambayo angependa mwenyewe kutokana elimu yake (kidato cha nne).

Kaenda CCP bila kuniaga japokuwa najua alifanya usaili na kapata nafas ila baadae tulikaa tukakubaliana nimtafutie chuo na kweli nikafanya hivyo na chuo nikawa nimepata na alitakiwa aripoti chuo jumatatu (14/09/'15). Wakati mimi nafanya maandalizi yake ya kwenda chuo aliniaga aende kumuaga shangazi yake Mwanza nikamruhusu, cha ajabu amefika huko (nilivyokuwa naamini kaenda mwanza) kawa hapatikan hewani mimi nikajipa matumaini kuwa ni tatizo la chaji kwa kuwa sehemu nyingi zinakabiliwa na kukatika katika kwa umeme nchini.

To my surprise, usiku wa leo nikapata sms kutoka namba ngeni ila nikajua ni yeye kwani niko nae yeye pekee, baada ya kuchati nae kidogo kaniaga akisema, " kwa heri baby, kuwasiliana hadi mwakani"Sikujali maneno yake ila karudia tena kusema ndo nikamwuliza kulikon akaanza kwa kuomba msamaha kisha akasema, "niko Moshi CCP". Nilihisi kuchanganyikiwa na siko vizuri kimawazo saivi kwani sina imani kama atarudi salama baada ya mafunzo.

Ndugu, naomba mnipe mwanga kuhusiana na usalama wa watoto wa kike huko chuoni na uwezekano wa raia wa kawaida kumwoa askari kama huyo. Au ndo nianze mchakato wa kumtafuta mrithi wake? Kingine askari anaruhusiwa kuolewa baada ya mda gani tangu ahitimu mafunzo ama aanze kazi?
 
punguza hofu kama kweli mnapendana mtalindana
 
askari anaruhusiwa kuolewa baada ya miaka mitatu kwa polis lakini mengine ni nyie wenyewe kwani uaminifu wa mtu ni yeye mwenyewe
 
tatizo jeshi linautaratibu wake ORDERS...amri...kwahiyo anapoagizwa kazi marufuku kubisha ni kuitekeleza tu...akiagizwa kwa boss mkware kutoa huduma..kaisha......tafuta mwingine tu ndugu
 
Kuolewa Ni miaka 15 ndo aolewe.kumegewa huko Ni kawaida,maana kuna shida sana na kule hakuna kukataa mkuu wako anachosema.pole sana huna mke tena.
 
Maboss wote ni wakware tu, hapo ni kazi tu!! sorry hapo fanya mabadiliko tu!!!
 
Hiyo ya kuolewa sijui....

Ila kama hofu yako ni kumegewa hata angeenda chuo kingine kama mwenyewe akiamua kumegwa angemegwa tu

Wewe ndio unamjua mpenzi wako...hofu ya nini??

Wasiwasi wangu ni juu ya maofisa na wale wanaowapa mafunzo kwani watu waliopitapita huko hudai eti mademu wanajilegeza kwa wale jamaa ili wawahurumie katika mtizi.
 
Akijilegeza huko ujue hata akienda chuo kingine ujue ataliwa na malecture.......


Wasiwasi wangu ni juu ya maofisa na wale wanaowapa mafunzo kwani watu waliopitapita huko hudai eti mademu wanajilegeza kwa wale jamaa ili wawahurumie katika mtizi.
 
Kuolewa ni miaka 5 baada ya kuajiriwa!

Ahsante kwa kunijuza.
Vipi lakini uwezekano wa mtu kuacha kazi hiari baada ya mda fulani inaruhusiwa? na kama wanafanya kazi kwa mkataba, mtu anaweza toa ombi la kuacha kazi baada ya muda gani?
 
MWANDENDEULE hapa town nikiamka saa kum na moja nawakuta barabani wanapiga mchakamchaka na kuimna nyimbo kama hawana akili nzuri!!! Kwa wanavyodau kuamka ni saa nane usiku saa tisa tizi inaanza duuuuuhh yan nawaoneaga huruma!!! Kuna mmoja nilimuona anaachwa nyuma kila siku sijui ndo demu wako????? Kwa kifupi akimaliza jiandae kushika adabu...maana ukileta ujinga utakuta unapigwa makofi na virungu mbele za watoto!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom