Mchumba wangu kaenda chuo cha polisi

mapolisi watamu sana...take it from me....mzee usimuache demu kisa kaenda kuwa polisi....Ndicho anachopenda...Give her anachopenda
 
Ahsante kwa kunijuza.
Vipi lakini uwezekano wa mtu kuacha kazi hiari baada ya mda fulani inaruhusiwa? na kama wanafanya kazi kwa mkataba, mtu anaweza toa ombi la kuacha kazi baada ya muda gani?

Kama aliweza kwenda ccp bila kukupa taarifa utawezaje kumshauri aache kazi akakuelewa? Kwa wazo lako hilo nakushauri uachane nalo, acha afanye kazi aliyoichagua hata kama wewe huipendi.

Umesema mchumba wako ameenda ccp tena bila kukutaarifu mapema, hapo unaweza kuniambia unadhani ni kwanini hakukujulisha mpango wake huo?

Umesema alikupigia simu kwa namba usiyoijua, je umechunguza namba hiyo ni ya nani na kwanini akupigie kwa namba hiyo na si ile unayoijua wewe?

Una uhakika kama ni kweli yupo ccp moshi na sio yupo na mwanaume mwingine na anatumia jina la polisi kukufunga mdomo ili usimfuatilie?

Ningekushauri jambo lakini kwa kuwa wewe ndiye unayemfahamu vizuri huyo mwenzako basi wewe ndio unatakiwa kujishauri na kuamua nini kifanyike.

Jambo la kukusisitizia tu ni kuwa ikiwa ni kweli yupo huko alipokuambia hesabu huna chako na kitendo cha yeye kufanya michakato bila kukushirikisha ndio dalili yenyewe ya kwamba hakuheshimu na hajali mawazo yako au vinginevyo ujue wewe ulikuwa unamchagulia kitu asichokitaka hivyo akaamua kufanya suala la kwenda ccp liwe siri ili usije kumsumbua.


Fanya uchunguzi kwanza kujua kama namba aliyokupigia ni yake au aliazima, kama ni yake basi tumia hiyo kumtafuta siku za jumatatu hadi ijumaa hasa nyakati za asubuhi na mchana kwa muda fulani utaweza kujua kama kweli yupo chuoni ccp au la! akipatikana kwenye simu nyakati hizo jua kuwa hayupo ccp(sijui kama ccp wanaruhusu kutumia simu).

Tafuta habari kwa ndugu na marafiki zake wa karibu, ukiona bado hujapata ukweli, vuta subira tu, muda utakuwa mkweli kwako, ni suala la muda halafu utajua mbivu na mbichi ipi.
 

Unawaona barabara gani wakipiga mchakachaka?
 
Last edited by a moderator:
Kujua ukweli kama kaenda kule au la tayari nimejiridhisha kwa hilo na kweli yeye yuko ccp na namba aliyotumia ni ya hapo ccp.
Kuhusu kwenda bila kuniaga kwa maelezo yake alivyosema siku kanicheki kwa namba ngeni ni kuwa baada ya kwenda huko mwanza waliafikiana na shangazi yake aende tu ccp na kwa vile mimi nilikuwa nimeshamshauri asiende huko na badala yake aende college toka alipofanya usaili na kupita akaona aende kimya kimya kwani alihofia ningetia ngumu. Amefika huko ccp akaona anitaarifa akianza kwa kuomba msamaha kwa kwenda bila kunitaarifu lakini kaahidi kuwa mwanminifu kitu ambacho si rahisi kuamin, you know women ain't trustful na hiki ndo kikanipa shida sana kwamba huko atakuwa salama au makoplo hujisevia kila wamtakaee maana mimi sina uzoefu na mwmbo ya huko mbali na kusikia tu kwa watu.
Kingine nimewasiliana na dada zake wawili tofauti wameonekana kusikitishwa na kitendo cha kwenda bila kuniaga na wanasema wao walikuwa wanajua alinitaarifu juu ya hili hata kabla ya kuwatarifu wao nyumbani punde tu shangazie aliposisitiza aende ccp na yeye kuridhia.
 
Hapo kwenye rangi ya bluu ndicho nilichokihisi kwenye post yangu ya hapo awali.

Hapo kwenye rangi ya bluu angalia usiwe ----- unayefurahi kwa kuwa tu umeahidiwa, huko aliko sio kuzuri kwa mtoto wa kike, na hata akimaliza kozi yake bado mazingira ya kazi yatakuwa yanakunyima raha. Kwa kuwa hukupenda aende huko fanya maamuzi ya busara, bora ungempenda akiwa tayari yupo kazini kuliko kabla maana atakuja na tabia nyingine itakayokufanya ujione ulipoteza muda tu kuwa naye.

Muweke pending atoke kwanza huko ccp halafu uone yuko vipi? pia jiandae na changamoto ya muda wa atakaokuwa nao kabla hajaruhusiwa kuolewa vile vile mazingira ya kazi, maana anaweza kupelekwa mtwara wakati wewe labda upo kigoma. Fanya tathmini ukiona hutayaweza achana naye na umpe taarifa mapema ajue kuwa umefikia uamuzi huo kwa sababu hukupenda yeye aende ccp.
 
Acheni mambo ya ajabu bana...kama unataka kutafuta mwanamke mwingine wewe tafuta tu ila sio kwa kuanza kumhukumu binti wa watu. tena nisisikie ukimwambia nakuacha kwa sababu umeenda polisi.

Pili bado ni binti mdogo ana haki yote ya kuwasikiliza wazazi wake kabla yako. Ungekuwa mchumba wake hata familia ingekushirikisha kwenye maamuzi ya nini afanye..heshimu uamuzi wa familia yake.

tatu, kwenda polisi kwako unatakiwa umshukuru sana kwani baada ya hapo atakuwa na ajira yake hata kama ataamua kusoma haitakuwa kwa mzigo wako. Ukome kabisa kumsimanga huyo mtoto kwa sababu zako binafsi.

nne uchumba na watoto wa shule ulianza lini? maana walioenda ccp kwa kidato cha nne ni wale waliomaliza kidato cha nne 2014. Kwa mantiki hiyo ulianza mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi na huoni aibu kuja kutushirikisha kosa lako la jinai hapa.

tano GROW UP MAN! ukisikiliza kila unalolisikia hutadumu kwenye mahusiano yoyote...!!!
 

kama hofu yako kubwa ni "kuliwa" basi ondoa shaka maana huko ni obvious kabisa, fanya maamuzi kwa mwelekeo huo.
 
Nimewasiliana nae tu jana lakini kasema hatakuwa hewani tena na mimi sijaicheki namba hewani tena kwa sababu hiyo ya kutokuruhusiwa kuwa na simu.
Kuhusu ubikira, hilo bila kuficha demu nilimkuta kitu hakijaguswa kabisa-I love that lady indeed

If yu realy love her, yu can wait even for 14 years tena usione ni kitu. Tulia wala usiulize ulize watu, hakuna anayeujua upendo uliompenda huyu mdada
 
Mlikubaliana umtafutie chuo cha kweli? Ndio chuo gani hicho? Kwani ccp ni chuo cha uongo? Au ndio ile kudharau kazi za wenzenu?
 
Kuolewa ni miaka 3 ila kutokana na janga la ukimwi sasa ivi wanazaa na kuolewa kabla ya muda huo, na akuna tatizo tofauti na zamani
 
 
Well said, unajua jamaa atakua anachepuka kwanini awaze kuchapiwa?
Unajua Mwizi always anahisi aibavyo ndivyo wafanyavyo wengine. Amwache mtoto wawatu akasome, alafu nahisi huyu jamaa bado chalii sana.
 
Well said, unajua jamaa atakua anachepuka kwanini awaze kuchapiwa?
Unajua Mwizi always anahisi aibavyo ndivyo wafanyavyo wengine. Amwache mtoto wawatu akasome, alafu nahisi huyu jamaa bado chalii sana.


Si kweli usemavyo.
Kuna vitu ambavyo ni obvious.
Mazingira mengine ya kazi yanatia wasiwasi.
 
Sikubaliani na hilo hizo nifikra kivuli,kwanza hata angempeleka wapi kama demu kazoea kugawa atagawa tu, na kwanini ahisi Kuchapiwa asihisi vingine? kwani hiyo papuchi imekua sabunu kuwa ikitumiwa inaisha agaaah
Si kweli usemavyo.
Kuna vitu ambavyo ni obvious.
Mazingira mengine ya kazi yanatia wasiwasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…