Mchumba

Mchumba

moko

Member
Joined
Apr 9, 2011
Posts
57
Reaction score
2
Mchumba,wajamani nina tatizo ambalo ni siriaz naomba msipuuzie,nina mchumba nimempenda na si ishi nae mwaka ss umeisha,kuna shida moja nampenda sn na yeye ananipenda shida ni kwamba mi niko chuo kikuu yeye ameishia form 4,alifel nimemwambia arisit pepa hataki nami nataka awe na ht credit ili asomee ht ualimu hataki,nataka nimuache,manake nikifikiria maisha nadata kwani nimagumu sn kwa wawili km hamtajituma kwenye kazi na kuzalisha,nifanyeje wakuu ushauri wenu ni wamuhimu
 
Sio lazima wote tuwe wasomi....umemuuliza anataka kufanya nini yeye kama yeye???
 
mbona mchumba mvivu?hajui kama maisha ya sasa ni kusaidiana?labda umwambie ajaribu kufanya biashara
 
sio lazima wote muwe na degree.yeye anaweza akajiari na elimu ya form 4 kama hataki kuendelea kusoma.labda pengine hujampenda.......
 
Sio waliosoma wote wamefanikiwa......Huyo mchumba wako anaweza akawa na mkono mzuri sana wa bihashara.....
 
Anaweza asisome lakini akawa a very good wife na akaweza kuendesha shughuli za hapa na pale... mana wew unafaham vizuri do you think ataweza fanya walau biashara..
 
Kwanza unatakiwa utambue mapenzi ni nini.. Labda hataki kuwa mwalimu kilamtu ana vitu ambavyo yeye anaona akivifanya vitamsaidia maishani. Huenda anawezakuwa mjasiriamali mzuri.. Ni vyema ukaenae chini na umuulize anachotaka nini, mara nyingine msaada wa kisaikolojia siajabu hakuamini kama atafel so kufeli kumemfanya aone kusoma hakuna maana. Dawa ya tatizo sio kulikimbia ni kulikabili unaweza mkimbia asietaka kusoma ukakutana na kicheche.. Nathani huna mapenzi ya dhati na huyo binti ndo maana unataka kuchukua uamuzi wa kumwacha.
 
Mbona huyu niliye nae mimi ni std 7 na maisha yanakwenda tu
 
Hapa kuna shida, jamaa mawazo aliyonayo ni kuwa na mwanamke aliyesoma. Hata mmshauri vipi bado hicho kitu kitamsumbua. Kuliko baadae mje muanze oooh ndiyo maana hujasoma mara ulikataa shule, fikiria mara mbili kabla hujaenda kwenye hatua ya kuoana. Hapa utapata ushauri wote mzuri na watu wenye uzoefu, lakini kama ww mwenyewe kwa mtazamo wako unafikiri vingine itakuja kukusumbua baadae.

Soma yote na uyazingatie lakini baadae fanya maamuzi kufuata moyo wako unasemaje.

Good luck.
 
Nashukurumi kwa ushauri, lkn kiukweli maisha ni magumu sn mwanamke kua golikipa sio ishu,anatamani kusomea mambo ya hotelia certificate level only,nafikiri sn jamani nieleweni elimu sio sababu lkn je kwamaisha haya tutatoka?mi namwona km ni mvivu
 
Na kitu gani kilichomfanya afeli? May be ana tatizo na anahofia kuja kutokea tena hali hiyo huku muda ukiwa umeshapotea.
 
ahaa inanikumbusha mbali sana, but ni jambo la kukaa na kujua nini anawawaza na kujua muelekeo wake, waweza msaidia, usiogope na kumkimbia
 
Nashukurumi kwa ushauri, lkn kiukweli maisha ni magumu sn mwanamke kua golikipa sio ishu,anatamani kusomea mambo ya hotelia certificate level only,nafikiri sn jamani nieleweni elimu sio sababu lkn je kwamaisha haya tutatoka?mi namwona km ni mvivu

Kaka naona hauko tayari kukaa na mwanamke ambaye hana kazi ama hajasoma. Nakushauri tafuta mwenye mlengo wako. Lasivyo utakuwa unautesa moyo wako bila sababu yeyote ya maana.
 
Sema umeshapata bond huko chuo ndio unatafuta sababu. Mfungulie biashara uone ataiendeshaje. KUFELI SHULE SIO KUFELI MAISHA.
 
Hapa kuna shida, jamaa mawazo aliyonayo ni kuwa na mwanamke aliyesoma. Hata mmshauri vipi bado hicho kitu kitamsumbua. Kuliko baadae mje muanze oooh ndiyo maana hujasoma mara ulikataa shule, fikiria mara mbili kabla hujaenda kwenye hatua ya kuoana. Hapa utapata ushauri wote mzuri na watu wenye uzoefu, lakini kama ww mwenyewe kwa mtazamo wako unafikiri vingine itakuja kukusumbua baadae.

Soma yote na uyazingatie lakini baadae fanya maamuzi kufuata moyo wako unasemaje.

Good luck.

Mimi like this so much . . .
Mi nakubaliana na wewe kuhusu kuelimika, ni muhimu sana hasa ukizingatia huko tunapokwenda.
Nimeona mabinti wengi wanakata tamaa mapema siku hizi, hasa wakimaliza Form 4 na kufeli
Utasikia " . . . mi nimechoka kusoma bwana, nataka nianze kufanya kazi"
Na kazi zenyewe wanazotaka ni hizi za kwenda kuwa wahudumu wa mahoteli, masekretari n.k.
Last week nilionana na mdada mmoja niliyesoma nae primary, ananiambia " . . . ingewezekana kurudi mdogo, ningerudi na ningebukua balaa, hata kama kupata kazi ukiwa msomi ni ngumu vipi, bado ningepambana na ningeweza kufanikiwa kuliko hivi sasa ambapo kazi nyingi nzuri naziona zinahitaji watu waliosoma angalau degree ya kwanza '
 
Mchumba,wajamani nina tatizo ambalo ni siriaz naomba msipuuzie,nina mchumba nimempenda na si ishi nae mwaka ss umeisha,kuna shida moja nampenda sn na yeye ananipenda shida ni kwamba mi niko chuo kikuu yeye ameishia form 4,alifel nimemwambia arisit pepa hataki nami nataka awe na ht credit ili asomee ht ualimu hataki,nataka nimuache,manake nikifikiria maisha nadata kwani nimagumu sn kwa wawili km hamtajituma kwenye kazi na kuzalisha,nifanyeje wakuu ushauri wenu ni wamuhimu

Tatizo ni wewe..wawezakuwa chanzo cha kufeli kwake ni wewe na siyo kwamba hana akili sana za darasani.....jaribu kufikiri utagundua county ya kichwa chako haifanyi kazi vizuri!
Elimu aliyonayo inatosha kumfanya aweze kuandika risiti na kurudisha chenchi kilichopo muulize anataka kufanya biashara gani iliumfungulie.unajua unaweza ukamaliza chuo na ukasota mtaani zaidi ya miaka miwili bila ya kupata hata kibarua mahali so hiyo biashara ikawainakusaidia hata ukapata nauli ya kwenda kwy interview mikoani.
mimi nawafahamu wafanyabiashara wengi tu hapa nchini walioishia std seven lakini kwy current account zao wana mamailioni ya fedha.
 
Ndugu,unataka kumwacha kwa kuwa amekataa kujiendeleza na masomo? Nadhani hautakuwa sahii utakapomwacha manake wewe ka wewe huwezi kutabiri maisha yenu ya usomi yatakuwa na muhafaka gani mbeleni.Kwani wangapi wamewashauri waqpenzi wao wasome nakisha baada ya kula book wakachikichia na njemba zingine?na je, hujui kuwa mwaweza nyote muwe wasomi lakini mapenzi ndani ya nyiumba yakapotea?So,we kama umempenda kuwa naye na atafanya hata biashara zingine sio lazima sana wote msome.
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu, hata mimi nilikuwa mbishi kama huyo mchumba wako aisee ila jamaa alinikazania sana sana mpaka nikarudi shule na sasa ni mmoja kati ya wasomi lol maisha jamani haya!! ila endelea kumshauri akikataa aanze tu biashara kwani wadada wengi sana siku hizi wanafanya biashara na wanafanya vizuri tu
 
Back
Top Bottom