Mchungaji adai mume wa Zari bado yupo hai

Mchungaji adai mume wa Zari bado yupo hai

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Mchungaji Mondo Mugisha ameibua mjadala mpya kuhusu kifo cha mfanyabiashara na aliyekuwa mpenzi wa Zari The Bosslady, Ivan Semwanga, baada ya kudai kuwa bilionea huyo hakufariki dunia kama ilivyoripotiwa mwaka 2017, bali bado yuko hai na amejificha.

Kupitia video iliyosambazwa kwenye mtandao wa TikTok, Mondo alidai kuwa anafahamu mahali Semwanga alipojificha, akieleza kuwa mfanyabiashara huyo aliamua kutoweka ili kukwepa mambo ambayo alikuwa akitakiwa kuyatekeleza.

"Hakuna uwezekano kwamba Semwanga angeshindwa kujificha kutokana na mambo ambayo walikuwa wakimtaka ayafanye," Mondo alisema.

Aidha, mchungaji huyo alidai kuwa Semwanga aliamua kujitenga na aliyekuwa mpenzi wake, Zari Hassan, na kuanza maisha mapya sehemu nyingine. Aliongeza kuwa mfanyabiashara huyo anafahamu watoto wake wako salama, hivyo hana sababu ya kurejea.

Hata hivyo, Mondo hakueleza alikozipata taarifa hizo wala kutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yake kwamba Semwanga bado yuko hai.

Madai hayo yamekuja siku chache baada ya mwandishi wa habari Simon Kaggwa Njala kuibua tena maswali kuhusu mazingira ya kifo cha Semwanga kilichoripotiwa kutokea nchini Afrika Kusini mwezi Mei 2017.

Njala alihoji mazingira ya kulazwa kwake hospitalini na kutaka ripoti ya uchunguzi wa mwili wake baada ya kifo iwekwe wazi.

Kutokana na kauli hizo, Zari alijibu kwa msisitizo kuwa Semwanga alifariki dunia na mwili wake ulirejeshwa nchini Uganda kwa ajili ya mazishi.

"Sisi tuliopata msiba tunajua kuwa alifariki dunia. Tulithibitisha kifo chake, tukafunga jeneza lilokuwa na mwili wake na kukamilisha taratibu za nyaraka za kuurejesha mwili wake nchini Uganda," Zari alisema.

Zari pia alieleza kuwa uchunguzi wa mwili wa Semwanga ulifanyika nchini Uganda na kwamba wanawe walishiriki katika maandalizi ya mwili wa baba yao kwa kuzingatia mila na desturi za jamii yao.

Aidha, Zari alipuuzia maswali ya Njala, akihoji sababu za mwandishi huyo kuendelea kuibua suala hilo miaka mingi baada ya kifo cha Semwanga.

Ivan Semwanga alikuwa akifahamika kwa maisha yake ya kifahari na uhusiano wake na kundi maarufu la Rich Gang. Aliripotiwa kufariki dunia mwezi Mei 2017 baada ya kukaa hospitalini nchini Afrika Kusini kwa takribani siku 11.
 
Mchungaji anatafuta fursa alipwe sadaka Nono ili aseme atamrudisha billionaire.
Wagalatia hatari Sana kwa utapeli wa kutumia miujiza.
 
Back
Top Bottom