Mchungaji afia gesti akiwa anamuombea maombi ya faragha mrembo wa Kanisani kwake

Mchungaji afia gesti akiwa anamuombea maombi ya faragha mrembo wa Kanisani kwake

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,864
Reaction score
5,254
Mchugaji Michael Kofi Appiah muanzilishi wa kanisa la Light of Faith Ministry, Tokoradi -Ghana amefariki kifo cha kushtusha baada ya kufia gesti alipokuwa akimuombea msichana mrembo katika shughuli za nje ya kanisa.

Uchunguzi wa polisi ulionesha kuwa mchungaji Kofi alikuwa amefika hapo na msichana mrembo ambaye anatajwa kuwa ni mwanachuo na walipaswa kuwa na faragha kwa ajili ya maombezi humo chumbani, ambapo walipewa vyakula na vinywaji mida ya asaa 4 usiku.

Hata hivyo katikati ya usiku wa manane msichana huyo alipiga kelele ambazo ziliwafanya walinzi wa gesti hiyo kwenda na kuona mchungaji huyo amelala akiwa nusu utupu.

Uchunguzi ulibaini mchungaji Kofi alikuwa amefariki na bado polisi wanaendelea kuchunguza kuwa huenda ni sumu kwenye chakula au ugonjwa wa moyo.

Mchungaji Kofi ameacha mke na watoto mpaka sasa watu wanajiuliza je, kweli mchungaji anaweza kuwa na maombezi ya faragha kiasi cha kufanyia gesti au hotelini na mwanamke, wakati yeye ameoa?
FB_IMG_1776263187332.jpg
 
Uchunguzi wa polisi ulionesha kuwa mchungaji Kofi alikuwa amefika hapo na msichana mrembo ambaye anatajwa kuwa ni mwanachuo na walipaswa kuwa na faragha kwa ajili ya maombezi humo chumbani, ambapo walipewa vyakula na vinywaji mida ya asaa 4 usiku.😂
 
Back
Top Bottom