Mchungaji afia gesti akiwa anamuombea maombi ya faragha mrembo wa Kanisani kwake

Mchungaji afia gesti akiwa anamuombea maombi ya faragha mrembo wa Kanisani kwake

Huyu mleta mada ameamua kumsaidia shetani kueneza uongo. Ameongeza chumvi ili kuwavuta wapenda habari za udaku. Habari original haisemi Mchungaji alikutwa nusu uchi, wala haisemi huyo mwanamke alikuwa mrembo. Na wala haisemi alikuwa anamfanyia maombi.

Original source hii hapa:

Hata hivyo siungi mkono kitendo cha Mchungaji huyo kwenda guest na mwanamke, usiku, hata kama ni kwa nia njema.

Mchungaji aliongozwa guest na Roho Mtakatifu wake au vipi ??
 
Nikadhani bongo bana

RIP mchungaji.
Ajali kazini
Huyu mleta mada ameamua kumsaidia shetani kueneza uongo. Ameongeza chumvi ili kuwavuta wapenda habari za udaku. Habari original haisemi Mchungaji alikutwa nusu uchi, wala haisemi huyo mwanamke alikuwa mrembo. Na wala haisemi alikuwa anamfanyia maombi.

Original source hii hapa:

Hata hivyo siungi mkono kitendo cha Mchungaji huyo kwenda guest na mwanamke, usiku, hata kama ni kwa nia njema.

Home / HABARI ZA KIMATAIFA / PASTOR AFARIKI DUNIA KATIKA NYUMBA YA MWANAMKE

PASTOR AFARIKI DUNIA KATIKA NYUMBA YA MWANAMKE​

Omari Makoo 10:19 PM HABARI ZA KIMATAIFA
Hali ya taharuki ilikumba mtaa wa Buruburu, Nairobi baada ya mwili wa kasisi kupatikana katika chumba cha kulala cha mwanamke aliyesemekana kuwa muumini wa kanisa la pasta huyo.

[td]
​
[/td]​
[td]
Estate Za Buruburu Nairobi​
[/td]​
Kasisi huyo mwenye umri wa miaka 70 alisemekana kutembelea mwanamke huyo katika mtaa wa Buruburu Phase 1 mwendo wa saa tano asubuhi na kukaa ndani ya chumba hicho siku nzima.

Maafisa wa polisi walisema mwili wa kasisi Geoffrey Maingi ulipatikana bila majeraha yoyote.
Mkuu wa Polisi wa Buruburu Richard Kerich alisema kasisi huyo anayehudumu katika kanisa la Redeemed Gospel Buruburu aliliegesha gari lake katika duka la Tuskys mtaani humo kabla ya kuelekea kwa mwanamke huyo.

Mwanamke mwenye chumba hicho alisema kasisi huyo alikuwa ameenda kumuombea na kuongeza kuwa hakujua iwapo alikuwa mgonjwa.

“Si mara ya kwanza kwake kuja tushiriki maombi pamoja. Amekuwa akinitembelea mara kwa mara,” alisema mwanamke huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 aliwaambia polisi kuwa kasisi huyo alianguka ghafla na kufariki.
“Kando na kuwa pasta wangu yeye pia ni rafiki na ndio maana huwa tunashiriki maombi pamoja,” akasema

Jirani wa mwanamke huyo alithibitisha kuwa kasisi huyo amekuwa na ziara kadhaa chumbani humo.

Tukio hilo lilivutia umati mkubwa huku baadhi ya wakazi wa mtaa huo wakidokeza kuwa huenda kifo cha pasta huyo kilitokana na matumizi ya dawa za kuongeza hamu/ashiki za mapenzi.

“Hii ilikuwa adhabu ya Mungu kwa kasisi huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo. Mungu alikuwa anataka kuleta vitendo vyake vya gizani hadharani,” jirani mmoja alinukuliwa.

Majirani walisema mwanamke mshukiwa alikosana na mumuwe mwaka uliyopita kufuatia mzozo wa kifamilia.

Waendesha teksi walisema kuwa mwanamke huyo aliwaomba msaada ampeleke hospitalini lakini tayari alikuwa amekufa.

Kuachiliwa:
“Alikuja hapa akitaka tumpeleke marehemu hospitalini lakini baada ya kufika kwake tulipata mwili wake ukiwa baridi kumaanisha alikuwa ashakufa,” alisema mhudumu wa teksi ambaye alisema baadaye waliwajulisha maafisa wa polisi.

Polisi walimzuilia mwanamke huyo kwa saa kadhaa ili kutoa habari kuhusu kisa hicho lakini wakamwachilia baadaye.
“Tutabaini chanzo cha kifo cha kasisi baada ya mwili wake kufanyiwa upasuaji, kwa sasa hauwezi kutoa taarifa yoyote,” alisema Bw Kerich .

Bw Kerich alisema kuwa polisi wamekusanya bidhaa katika chumba hicho ambazo zitatumiwa katika uchunguzi.

Mwili wa marehemu ambao polisi walisema haukuwa na majeraha yoyote ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City kufanyiwa upasuaji.

Waumini wa kanisa la Redeemed Gospel Buruburu walifika katika eneo hilo na kuondoa gari la pasta huyo ili kuzuia wanahabari kulipiga picha.
CHANZO:WACHIMBA RIZIKI​
 
Mchugaji Michael Kofi Appiah muanzilishi wa kanisa la Light of Faith Ministry, Tokoradi -Ghana amefariki kifo cha kushtusha baada ya kufia gesti alipokuwa akimuombea msichana mrembo katika shughuli za nje ya kanisa.

Uchunguzi wa polisi ulionesha kuwa mchungaji Kofi alikuwa amefika hapo na msichana mrembo ambaye anatajwa kuwa ni mwanachuo na walipaswa kuwa na faragha kwa ajili ya maombezi humo chumbani, ambapo walipewa vyakula na vinywaji mida ya asaa 4 usiku.

Hata hivyo katikati ya usiku wa manane msichana huyo alipiga kelele ambazo ziliwafanya walinzi wa gesti hiyo kwenda na kuona mchungaji huyo amelala akiwa nusu utupu.

Uchunguzi ulibaini mchungaji Kofi alikuwa amefariki na bado polisi wanaendelea kuchunguza kuwa huenda ni sumu kwenye chakula au ugonjwa wa moyo.

Mchungaji Kofi ameacha mke na watoto mpaka sasa watu wanajiuliza je, kweli mchungaji anaweza kuwa na maombezi ya faragha kiasi cha kufanyia gesti au hotelini na mwanamke, wakati yeye ameoa?
View attachment 3573216

Hawa wachungaji labda ndivyo wanavyoongozwa na Roho Mtakatifu wao

View: https://www.youtube.com/watch?v=GjsT50zJ3M8
 
Mchugaji Michael Kofi Appiah muanzilishi wa kanisa la Light of Faith Ministry, Tokoradi -Ghana amefariki kifo cha kushtusha baada ya kufia gesti alipokuwa akimuombea msichana mrembo katika shughuli za nje ya kanisa.

Uchunguzi wa polisi ulionesha kuwa mchungaji Kofi alikuwa amefika hapo na msichana mrembo ambaye anatajwa kuwa ni mwanachuo na walipaswa kuwa na faragha kwa ajili ya maombezi humo chumbani, ambapo walipewa vyakula na vinywaji mida ya asaa 4 usiku.

Hata hivyo katikati ya usiku wa manane msichana huyo alipiga kelele ambazo ziliwafanya walinzi wa gesti hiyo kwenda na kuona mchungaji huyo amelala akiwa nusu utupu.

Uchunguzi ulibaini mchungaji Kofi alikuwa amefariki na bado polisi wanaendelea kuchunguza kuwa huenda ni sumu kwenye chakula au ugonjwa wa moyo.

Mchungaji Kofi ameacha mke na watoto mpaka sasa watu wanajiuliza je, kweli mchungaji anaweza kuwa na maombezi ya faragha kiasi cha kufanyia gesti au hotelini na mwanamke, wakati yeye ameoa?
View attachment 3573216
"Maombezi" yalinoga hadi nabii akafariki. RIP mchungaji.
 
Huyo Kondoo hakujua kua anapelekwa gesti kutafunwa na mchungaji?

Halafu huyo mchungaji inaonekana hiyo ndio tabia yake.
Hata ingekuwa wewe ungefia kwenye maombi kifuani mwa mrembo mkuu. Msichana mrembo kama huyu unamuachaje kwa mfano?
 
Kila mara nasema walokole ni jamii ya hovyo kuwahi kutokea kwenye uso wa dunia ,mnabisha.
Mkuu walokole ni binadamu kama walivyo binadamu wengine.
Wataabudu na pia watavunja amri za Mungu.
Wasamehe tu
 
Nashangaa mtu anatumia viagara kwenda kukutana na mwanamke huwezi kukomoa **** hata siku moja ile inatanuka kutokana na maumbilie inayokutana nayo
 
Hasa ukiwa na tatizo la BP, itakuua tu. Na huwa inakuua ukikaribia mshindo au baada tu ya mshindo

Mbaya zaidi, kuna wale wanaamua kunywa vidonge viwili, wakiona kama cha kwanza hakipandishi mdadi sawasawa. Hapo ni kifo kinakuja
Hatari sana mkuu.
 
Kuna muhuni anakwambia ukimwi ni hatari sana anasahau kuna presha kuna kisukari hayo magonjwa kukuua ni kugusa tu
 
Kuna mda tunaish na maralia ipo juu.
Ila inakua haijaamka.

Sasa ukinyeshewa mvua, au kupgwa kofi au kiboko au kupiga bao ukiwa unasex.
HAPO MARALIA INAAMKA MTU ANAZIDIWA GHAFLA
 
Back
Top Bottom