Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,986
Makanisa yakiongezeka wanakuaje insecure?Mkuu Zanzibar ni nchi ya kiislamu, 99% ya watu wake ni waislamu, kwahiyo hakuna cha ajabu kuwa na mifumo ya kiislamu kwenye maisha yao, ni tofauti na Bara ambapo uwiano wa dini hizi mbili ni mkubwa nearly 50 - 50, So cha muhimu ni kufahmu kuwa haiwezekani mazingira ya Zanzibar yakawa sawa na Bara. Tujaribu kulitathmini kwa uandani na sio kuishabiki. Tatizo kuu la Zanzibar ni suala la Makanisa kuwa yanaengezeka kwa kasi kila siku zinavyokwenda, Na hilo linawafanya wananchi wao wengi kuwa insecure. Nchi nyingi ambazo ziko dominated na dini moja kwa zaidi ya 90% ni lazima watu wa dini nyengine wata experience mambo kama hayo, na hasa wakiwa Wageni.
Na kwa nini makanisa yasiongezeke? Hata na waislamu wanairuhusiwa kwenda kwenye wakristo wengi na kujenga misikiti wanavyotaka