Mchungaji aliyedai kuvunjiwa Kanisa Zanzibar afunguka. Serikali yatangaza kumsaka, yasema ni nyumba siyo Kanisa

Mchungaji aliyedai kuvunjiwa Kanisa Zanzibar afunguka. Serikali yatangaza kumsaka, yasema ni nyumba siyo Kanisa

Huyo mkuu wa wilaya angekutana na Kibatala au Malya kizimbani ingependeza sana. Na haya maneno yake yakatumika kama ushahidi! Nawaza tu
 
Mkuu Zanzibar ni nchi ya kiislamu, 99% ya watu wake ni waislamu, kwahiyo hakuna cha ajabu kuwa na mifumo ya kiislamu kwenye maisha yao, ni tofauti na Bara ambapo uwiano wa dini hizi mbili ni mkubwa nearly 50 - 50, So cha muhimu ni kufahmu kuwa haiwezekani mazingira ya Zanzibar yakawa sawa na Bara. Tujaribu kulitathmini kwa uandani na sio kuishabiki. Tatizo kuu la Zanzibar ni suala la Makanisa kuwa yanaengezeka kwa kasi kila siku zinavyokwenda, Na hilo linawafanya wananchi wao wengi kuwa insecure. Nchi nyingi ambazo ziko dominated na dini moja kwa zaidi ya 90% ni lazima watu wa dini nyengine wata experience mambo kama hayo, na hasa wakiwa Wageni.
Aliyevunjiwa ni mgeni kutoka Kenya, Uganda, Ulaya, Asia au Marekani?
 
Hawa jamaa wakiwa majority wanakua miyeyusho sana kwa wanachofanyiwa china au myamar ni sawa kwa kua wao niwachache ?

kuna aliyeteswa Zanzibar kama wanavyoteswa hao wachina? tena ni wazawa kabisa
 
Kuna watu wengine ni wakorofi tu of all places kwanini ujenge kanisa Zazibar? ambao hamna wateje? 99% ni dini moja ya kiislamu? Ni yale yale ya kuweka bucha ya kitimoto karibu na mskiti wakati kuna sehemu zingine kwa kisingizio xha uhuru wa mtu kufanya biashara popote.
Are you serious? Kwa hiyo palipo na wakristo au aethist wengi basi msikiti ukatazwe!
 
Nitoke nje ya mada kidogo, hv makanisa ya kilokole kuubiri bila vipazasauti haiwezekani. Yaan SoMo haliwezi kueleweka. Japo dini na madhehebu mengine nao hufanya hivyo lakini wanaunafuu kidogo ukilinganisha na walokole.
Mbona misikiti inatunyima usingizi kwa vipaaza sauti, saa ingine na matusi ndani alfajiri?
 
Mkuu kuhusu hiyo namba 4 halina utata kabisa, Ni kweli Zanzibar kuna Wakristo wengi ila majority yao ni wahamiaji. Wakiristo wa asili kwa maana ya wale wanaotambulikana kama ni wazanzibari wakichanganyika na wahindu hawawezi kufika hata asilimia 1.
Hivi watu kutoka bara ni wahamiaji? Je wale toka Zanzibar waliopo bara ni sahihi kuwaita wahamiaji?
 
kuna aliyeteswa Zanzibar kama wanavyoteswa hao wachina? tena ni wazawa kabisa
Mkuu,
Hiyo hapo chini maana yake nini, siyo MATESO?!!!
👇👇👇
..Pia miezi michache ijayo kipindi cha mfungo kikianza huwa ni marufuku kwa wakristo kula sehemu za wazi, ukikutwa unafungwa mpaka mfungo uishe, wengine huwa wanapigwa sana...
 
Mbona misikiti inatunyima usingizi kwa vipaaza sauti, saa ingine na matusi ndani alfajiri?
Hama mji rudi kijijini kwenu ,utasikia sauti Za komba Tu alfajiri
 
So, what is your point here na tushike lipi hasa...?

Kwamba mamlaka za mipango miji huko Ugunja - Zanzibar ziliamua kulivunja kanisa la Mch. David Suni kwa sababu they are all insecure....?

Au tumwamini DC asemaye kuwa, zimevunja kanisa hilo kwa sababu ya utabiri wa hali ya hewa kusema kuna mvua kubwa zinakuja huko Ugunja - Zanzibar na mvua hizo zimelenga kuja kulipitia kanisa hilo tu ktk mtaa huo...?
Ina maana serkali iliona isaidie kuvunja hiyo sehemu ya nyumba kuliko ilihali isivunjwe na upepo wa mvua. Jamani, huyu DC anahitajika huku bara, ambako nyumba mamia na mamia huezuliwa au kuvunjwa na mvua/upepo ili avunje hizi nyumba mapema na kuokoa mabati. Hii itakuwa huduma ya aina ya pekee kutolewa duniani. Sijawahi kusikia popote duniani nyumba huvunjwa na serkali utabiri wa hali ya hewa ukionyesha upepo na mvua hatarishi. Mimi huwa nasikia kama kunategemewa mvua/upepo hatarishi watu wanaambiwa waondoke kwenye nyumba zao wakaende sehemu salama. Ni ajabu kuvunja nyjm,ba na mwenye nyumba kuachwa sehemu hatari.
 
Hivi watu kutoka bara ni wahamiaji? Je wale toka Zanzibar walipopo ni sahihi kuwaita wahamiaji?

Mkuu nchi yetu intambua wtu wa aina mbili tu ambo ni Watanzania na Wazanzibari. Wazanzibari wote ni watanzania, Ila Sio watanzania wote ni Wazanzibari.
 
Msikilize huyu X mchungaji


Siongei na huyo mchungaji naongea na wewe.

Kwa taarifa yako hiyo mihadhara nimeisikiliza saaaaaana miaka mingi nyuma huyo mwaipopo namfahamu vizuri sana,kwa hiyo hakuna jipya katika hiyo clip.

Mzanzibar ni nani ?
 
Hizo sheria zimetungwa baada uvamizi. Wazanzibari tunajuana vizuri Na Hao wakristo wanajulikana. Haya makanisa ya uyoga yanakuja kuleta fujo Tu.
Kuna video ya mchungaji aliyesilimu anaeleza vizuri malengo yao naitafuta nikuwekee
Hivi unadhani mimi ni mgeni katika uislamu mpaka unitafutie sauti za akina mwaipopo na wengineo wakielezea mambo waliyofanya miaka kadhaa nyuma wakiwa wakristo ?

Hayo mambo nayafahamu zamani sana na kwa taarifa yako hata waislamu huo utaratibu wa kuwashawishi watu waingie katika uislamu tunao,tunaita kufanya daawa na kuwalingania wasiokuwa waislamu waje kwenye uislamu.

Sasa kama ambavyo sisi waislamu tunafanya jitihada za kuwavuta watu waje kwenye uislamu vipi tubeze na tuone kama ni ujambazi na jinai kwa mapadre wanapotumia juhudi zao kuwavuta watu katika ukristo ?

Unafahamu kwamba kwenye utaratibu wa zaka kuna pesa unaweza kutoa kuwapa wasiokuwa waislamu ili wapate mazingatio kwwmba uislamu unawajali hata wasiokuwa waislamu ?

Haya yote hata wakristo wanafananya na tusione kama ni booonge la jinai,wao pia wanafanya daawa ya kuwavuta watu kwenye dini yao.
Hizo sheria zimetungwa baada uvamizi.
Kabla ya hizo sheria naomba uniambie mzanzibari ni nani ?
Wazanzibari tunajuana vizuri
Mnajuanaje ?

mnajuana kwa vichwa bapa na masikio makubwa yaliyosimama ?
au mnajuana kwa kuangalia weupe?
Au mnajuana kwa kuangalia kazaliwa zanzibar au bara ?
Au mnajuana kwa lafudhi ?

Elezea mnajuanaje ?

Elezea mzanzibari ni nani ? acha kuuma maneno
Hao wakristo wanajulikana.
Kuna uhusiano gani wa wakristo na wazanzibari ?

Uliposema wazanzibari mnajuana ulitakiwa useme kwamba na wabara pia wanajuana,lakinj kusema wakristo maana yake unataka kuaminisha umma kwamba wazenji wote waislamu ?

Ukisema wazenji wote ni waislamu naomba uniambie maana ya mzenji/mzanzibari ni ipi ?
 
Wanadamu wangefahamu kuwa amri kuu kuliko zote ni upendo wasingegawanywa na dini.
Tatizo ktk uislam amri yao kuu ni usichangamane na asiyekuwa muislam ukipata chance mle kichwa uione pepo sasa hii theory ya kwamba pendaneni haiwazi ku-match hata mara moja.

Waislam wana chuki moja mbaya sana kwa wasiokuwa waislam ni vile duniani zimekuwepo sheria kama sivyo hawa wangeleta shida sana wanatakaga humu duniani wawepo wao tu.
 
Back
Top Bottom