Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 8,428
- 4,022
Hivi unadhani mimi ni mgeni katika uislamu mpaka unitafutie sauti za akina mwaipopo na wengineo wakielezea mambo waliyofanya miaka kadhaa nyuma wakiwa wakristo ?
Hayo mambo nayafahamu zamani sana na kwa taarifa yako hata waislamu huo utaratibu wa kuwashawishi watu waingie katika uislamu tunao,tunaita kufanya daawa na kuwalingania wasiokuwa waislamu waje kwenye uislamu.
Sasa kama ambavyo sisi waislamu tunafanya jitihada za kuwavuta watu waje kwenye uislamu vipi tubeze na tuone kama ni ujambazi na jinai kwa mapadre wanapotumia juhudi zao kuwavuta watu katika ukristo ?
Unafahamu kwamba kwenye utaratibu wa zaka kuna pesa unaweza kutoa kuwapa wasiokuwa waislamu ili wapate mazingatio kwwmba uislamu unawajali hata wasiokuwa waislamu ?
Haya yote hata wakristo wanafananya na tusione kama ni booonge la jinai,wao pia wanafanya daawa ya kuwavuta watu kwenye dini yao.
Kabla ya hizo sheria naomba uniambie mzanzibari ni nani ?
Mnajuanaje ?
mnajuana kwa vichwa bapa na masikio makubwa yaliyosimama ?
au mnajuana kwa kuangalia weupe?
Au mnajuana kwa kuangalia kazaliwa zanzibar au bara ?
Au mnajuana kwa lafudhi ?
Elezea mnajuanaje ?
Elezea mzanzibari ni nani ? acha kuuma maneno
Kuna uhusiano gani wa wakristo na wazanzibari ?
Uliposema wazanzibari mnajuana ulitakiwa useme kwamba na wabara pia wanajuana,lakinj kusema wakristo maana yake unataka kuaminisha umma kwamba wazenji wote waislamu ?
Ukisema wazenji wote ni waislamu naomba uniambie maana ya mzenji/mzanzibari ni ipi ?
Hivyo ulivyoandika umeandika kwa jaziba, hata hujamsikiliza ni mbinu gani walizokuwa wakizitumia, Laiti ungalitulia ukamsikiliza usingeandika hayo uliyoyaandika Kama muislamu.
Nakuambia tena Wazanzibari tunajuana kwani hii sio Tanganyika, kila mmoja ana kwao .