saimon rusana
Member
- Mar 15, 2024
- 28
- 98
Habari za jioni mabibi na mabwana
natumaini hamjambo nyoote,
Mimi nimekuja kuomba ushauri natambua humu kwenye jukwaa kuna watu tofauti tofauti kwanzia kiumri, kidini, nitatuma, nk.
Mimi ni kijana wa miaka 28 katika kutafuta maisha kwangu nimeamua kuchukua maamuzi magumu ya kuachana na uzinzi nataka kuoa, sasa nimepata mchumba huko kijijini kwetu na kwa jinsi alivyo nimemuelewa na nilitaka nitoe kishika uchumba kabisa ili mwezi wa 12 tufunge ndoa.
Pia soma: Alidanganywa na Mwanaume wake kuwa ni Askari sasa limemkuta Jambo. Tumuombee
Jumapili tulikua tumepanga ndio nipeleke kishika uchumba lakini cha kushangaza leo nimepewa taarifa kwamba mama mkwe mtarajiwa alikwenda kwa mchungaji wao kuwapa taarifa kuhusu binti yao kupata mchumba na tunahitaji kufunga ndoa, chaajabu mchungaji wao amegoma kwa sababu ya dhehebu langu (KKKT) kwamba sio la kiroho coz wao ni wa Pentecostal Eti na kama watakaidi na kutengwa.
Sasa kwa haraka haraka nikagundua nia yao watataka mimi nifuate dhehebu la binti japokua hawataki kunyoosha maelezo, na mimi siko tayari kwa hilo. naomba maoni yenu.