Mchungaji Ananje: Ni ujinga watoto kugombania mali za marehemu kwasababu nao ni sehemu ya mali/mifugo yake

Mchungaji Ananje: Ni ujinga watoto kugombania mali za marehemu kwasababu nao ni sehemu ya mali/mifugo yake

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Mchungaji huyu akitoa maoni yake juu ya watoto wa marehemu kugombea mali ameponda vikali.

Amesema watoto ni mifugo/ mali ya marehemu hivyo hawana chao kabisa kwenye mali za marehemu. Mifugo inadai urithi wa mifugo wenzie? Amehoji mchungaji huyo

Wapeni salaam watoto wa Mrema na mzee Mengi
 
kwa hiyo watoto wa hayati mzee mengi na mzee wa kiraracha nao ni mifugo kwa mujibu wa mchungaji!?
 
Mchungaji huyu akitoa msoni yake juu ya watoto wa marehemu kugombea mali ameponda vikali.

Amesema watoto ni mifugo/ mali ya marehemu hivyo hawana chao kabisa kwenye mali za marehemu. Mifugo inadai urithi wa mifugo wenzie? Amehoji mchungaji huyo
Mimi nakubaliana na huyu mchungaji kabisa,
Japokuwa ni haki watoto wa marehemu kurithi mali za wazazi wao lakini ikitokea mzazi wako akakunyima mali
zake siyo haki kuzigombania. Jambo la kujiuliza ni je yeye alizipataje? Mimi pamoja na kupewa urithi na baba yangu
nami nimepambana kupata za kwangu,Urithi mkubwa nilioupata kwa wazazi wangu ni elimu na hivyo nimepambana kutoka kwa kuitumia hiyo.

Ni kosa kubwa kukodolea macho mali za wazazi,ukijivunia kuendesha magari yao,na kuishi kwenye nyumba zao
ukisubiria Mungu awachukue upate urithi.Toka pepo(kwa sauti ya mchungaji ananja)
 
Japokuwa ni haki watoto wa marehemu kurithi mali za wazazi wao lakini ikitokea mzazi wako akakunyima mali
zake siyo haki kuzigombania.
Kuna watoto wanaacha kutafuta zao wanasubiria za baba zao
 
Huyo mchungaji hajasindikiza hata na reference moja ya Biblia? Labda sio Taaluma yake. Na hapo ndipo Waislam wanapowapiga Gap Wakristo Kwa Hoja.

Ishu ya Urithi ipo Kisheria na kiimani.

Kugombea Urithi ni lazima na wajibu kwani ni Haki ya Watoto.

Hata hii nchi tumeirithi kutoka Kwa Mababu zetu. Bila Urithi hakuna maisha. Aache akili za mkumbo
 
Na wewe hujaweka hicho kifungu cha Sheria au maandiko?!?!
 
Mchungaji yupo sahihi

Kugombania kitu ambacho hujakitafuta Ni upuuzi mkubwa.

Waafrika mmeshachanganywa tayari.
Hamjui hata haki zenu ni zipi.

Ni upuuzi Kama hujui kuwa Kitu cha Baba yako unahaki ya kurithi. Labda yeye ndiye asitake na awe na sababu za msingi
 
Waafrika mmeshachanganywa tayari.
Hamjui hata haki zenu ni zipi.

Ni upuuzi Kama hujui kuwa Kitu cha Baba yako unahaki ya kurithi. Labda yeye ndiye asitake na awe na sababu za msingi
Sawa Mkuu kwanza waafrika Wana Mali ? Gani mkuu za -kurithi
 
Sawa Mkuu kwanza waafrika Wana Mali ? Gani mkuu za -kurithi

Hata nchi, mashamba ni Mali.

Kama hakuna Urithi basi hakuna utaifa.
Fikiria mtu aje akuambie ni upuuzi kupigania nchi yako/urithi WA nchi yako utamuona anaakili?

Baba au Mama ni family level katika mambo ya Urithi.

Ukiona mtu hajui umuhimu wa Urithi jaribu kuangalia akili yake na kwao wakoje, wengi ni masikini na wasiojielewa.
 
Halafu hapo mwishoni wanataka sadaka, yani hawa wahuni waliojificha kwenye ni hatari sana.
 
Ameongea hv na waamini wakaitikia amina sio 😄 kuwa kiongozi wa dini raha sana maana ni kama wameruhusiwa kuongea chochote
 
Kama hajawakwekwa kwenye mgao ndani ya wosia aloauacha maana yake hataki. Inashangaza kuona watoto wanaenda mahakamani.

Utofauti wa kifikra unatoka na asili na familia ulipotoka ila incommon na hata kidini na hasa kwa dini ya kiislam urithi unamaana kubwa sana...mali alizotafuta mzazi siku zote sio sawa kuzitegemea maana zipo kwajili ya kumsaidia mwenyewe kwenye muda ulobaki kabla ya kifo kwaiyo ile ni hazina yake na ndo nguvu yake ukiacha watoto. Ila ikitokea kifo na watoto wake wapo basi ni haki ya wototo wake kurithi zile mali kwasababu kuna familia zingine wazazi wameweza kufanikisha malengo yao wakiwa na watoto wao na pia kushirikiana na watoto wao(binafsi nishashuhudia first born mmoja akichunga ng'ombe za wazaz wake alipokua mdogo na akiingiza kipato kuzuri tu kwenye familia kupitia maziwa) kwaiyo kama ni mzazi mwenye busara ni vema kuwapa warithi wako(wapendwa/damu yako) ulohangaika nao kipindi ukiwa mzima waweze kuendeleza au kuvuna matunda yako kipindi ulipokua duniani kuliko kugawa kwa watu baki au watu wasio kua na jasho lolote kwenye mali zako.

Kwa kumaliza tu naamini mchungaji sio mungu naye nibinadam anafikra zake namitazamo yake na sio alinenalo kua ni sheria au ndo sahihi apana ndo maana kwenye kila uongozi kuna kukaimu na zaman watu walikua wanarithi hadi ufalme ndo ivo ivo kwenye maisha ya kawaida unapondoka ni muhimu sana kukarudisha mali zako kwa wapendwa wako na sio kosa kurithi wala kugombania haki yako ya urithi kama kweli kuna dhulma ndani yake kwa kufwata sheria za nchi mila ama dini husika.
 
Back
Top Bottom