Benaya-
JF-Expert Member
- Jul 31, 2019
- 4,415
- 7,631
Katika hali ya kushangaza, siku zote mzee wa Upako huwa upande wa serikali.
Lakini leo ameamua kuvunja ukimya na kuinyoshea serikali kidole tena kwa ukali kuwa ijihadhari isije kuharibu amani ya Tanzania.
Wakati akitoa angalizo hilo, amewataja kwa majina akianza na Kassim Majaliwa waziri mkuu, Rais Samia na Mpango.
Amewakumbusha kuwa sio vyama vya upinzani pekee huleta machafuko bali hata Serikali huwa ni chanzo cha machafuko.
Ameonya kuwa uonevu ukizidi hata askari taratibu huungana na raia kinyume cha watawala kwani hata wanao onewa ni jamaa zao na maaskari.
Zaidi ameionya serikali kujiepusha na kuingilia mambo ya kidini kwani hata wakizifuta imani za dini ziko mioyoni mwa watu na sio kwenye usajili wa kiserikali.
Amekumbusha kuwa miaka ya 80 serikali ilijaribu kufuta usajili wa makanisa hata kuwafunga wengine lakini ilishindwa na tena wakristo waliungana.
Amesema watu wa imani moja huungana wakati wa kuonewa hivyo wajihadhari na jambo hilo.
Amesema kwasasa serikali ina matatizo makubwa kisiasa, corona nk kwa hiyo isiongezee mzigo wa kidini haitabaki salama.
Zaidi msikilize hapo chini kwenye link.