Mchungaji apigwa faini ya Sh5 milioni kwa cyber bullying

Mchungaji apigwa faini ya Sh5 milioni kwa cyber bullying

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
52f778ba-57bb-4705-a573-ec414782d604.jpg


Mahakama ya Wilaya ya Kahama imemhukumu Mchungaji Shaniel Sosoa kulipa faini ya Sh5 milioni au kwenda Jela miaka mitatu kwa kosa la la uonevu mitandaoni (Cyber Bullying).

Akizungumzia hukumu hiyo, Katibu wa Kanda ya Serengeti ya CHADEMA, Jackson Mnyawami, amesema Mchungaji Sosoa alikuwa ameshitakiwa kwa makossa matano, lakini akakutwa na hatia ya kosa moja la Cyber Bullying.

“Hii kesi ni ya tangu mwaka jana, baada ya Mchungaji Sosoa kutoa video akilalamikia utekaji na kusema kwamba Serikali imeshindwa kutatua hilo tatizo. Alikamatwa na kuwekwa mahabusu kwa muda mrefu, kwa sababu masharti ya dhamana yalikuwa pamoja na kupata mtumishi wa umma, lakini tukakosa.

“Hata hivyo, baadaye alipata dhamana akawa anahudhuria kesi na ndio hukumu imetoka Julai 31, 2025,” amesema.

Amesema kwa sasa wanaendeleza mchango wa kupata faini ya Sh5 milioni kutoka kwa watu wenye mapenzi mema.

“Mpaka sasa tumeshakusanya Zaidi ya Sh2.5 milioni na michango inaendelea,” amesema.
 
Ukishaamua kuwa rais umekubali kuwa kuna cyberbullying.

Kama hutaki kuwa cyberbullied usiwe rais.

Kazi ya urais si nyoronyoro.

Rais anatakiwa kuwa ndiye mtu mwenye protection ndogo kuliko Mtanzania mwingine yeyote kwenyw cyberbullying.

Sisi tunafanya the opposite, tunamuwekea rais the most protection.
 
Back
Top Bottom