Mchungaji Dustan Maboya, umepatwa na nini hadi uanzishe ibada za usiku wa manane? Polisi chunguzeni huduma hii

Jamaa amepotoka sana. Unaposhirikiana na manabii wanaolambisha asali manake na wewe unakubaliana nao
 
Inamaana hujui kuwa Maboya ndiye baba wa kihuduma wa huyo Makondeko na Mwamposa?
Wakati Maboya anainukia kwenye huduma miaka ile ya 80, watumishi wenzake ndani ya EAGT walimsema kuwa anatumia nguvu za kipepo. Yeye akawa anakataa.

Baadaye akajitenga na kuanzisha Calvary Assemblies of God. Kanisa lilikua vizuri hasa miaka ile ya 90. Watu walianza kuamini kuwa jamaa ni mtumishi wa kweli wa Mungu.

Kumbe anatumia hill dhehebu kama kichaka cha kuzalisha manabii na walimu wa uongo ili waendelee kupotosha yamkini hata wateule wa Mungu. Hakika tupo nyakati zilizoongelewa kwenye maandiko 2Petro 2:1-11, Yuda 1:1-15, 1Yoh 4:1-3

Bottom line: Si kila anayejiita mtumishi wa Mungu ni mtumishi kweli wa Mungu. Wakristo wanapaswa kuwa macho kutofautisha mtumishi wa kweli na wa uongo na njia sahihi ni kupitia kujifunza maandiko. Vinginevyo, watu wataendelea kuburuzwa kwenda upotevuni.
 
Mungu waponye watoto wako na hawa manabii wa uongo. Uponyaji ni imani tu yako kwenye maneno ya Mungu basi. mengineo wanayoyafanya ni ya kichawi kama wachawi wengine
 
Mh, Bujibuji mbona huyo ni Joshua Makondeko ndio mwenye hilo kanisa kulingana na kipeperushi. Soma vizuri, hapo Maboya kawekwa kama chambo kuvuta nyomi.

Hii tabia ipo sana ya kutumia jina la mtu maarufu ili kupata nyomi. Sijui huwa wanapata approval au ndio vile tena!
 
Hahahaha, pale kiwanja Cha NMC. Nikiwa Arusha sec, Yani umenikunbusha mbaliii
 
Jane naomba uje nikanyage asali yako,nimeambiwa ni tiba ya kipururu
 
Huyu Maboya ndiyo yupo na Makundi na yule dogo wa kuuza mapazia pale corner ya SUA - Moro?
 
Mkuu umeua
 
Hzo pipi za miujiza ndo kaniacha hoi kabisa!
 
Hawa watu huwa hawachukuliwi hatua kwa sababu mafundisho yao ya imani yamepumbaza watu wengi ambao mwisho wa siku watu huwa wanatumika kama mtaji wa kisiasa kwa wanasiasa .... So hautokuja kusikia huyo jamaa akiguswa na mamlaka yoyote yale labda aende kinyume na matakwa ya wenye nchi ....refer yale ya mwamposa kukanyagisha mamia yawatu mafuta na watu hao baadhi wakafa lakini mpaka leo yupo uraiani anapeta tu
 
Hawa jamaa ni wachangiaji wazuri wa chama, ndio maana hawagusiki kirahisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…