Akilinjema
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 11,430
- 11,813
Mchungaji kuhamishwa Usharika sio mgogoro,labda kama huyo mchungaji haendi sawa sawa na kiapo chake cha kichungaji, acheni upambe na mheshimu taratibu za Kanisa.Huu mgogoro usije ukawa kama ule wa KKKT Dayosisi ya Konde, Mbeya. Inabidi busara itumike maana hii migogoro kwenye taasisi za dini haileti afya kwa maisha ya kiroho ya waumini wake.
Rejea:
Download Wachungaji 17 Wafukuzwa Kazi Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Askofu kwa uchungu Anena Mazito
Wachungaji 17 Wafukuzwa Kazi Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Askofu kwa uchungu Anena Mazito (6.45 MB) ~ Free Download Wachungaji 17 Wafukuzwa Kazi Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Askofu kwa uchungu Anena Mazito (04:42 Min) mp3 and mp4 ~ Download lagu mp3 & mp4 Wachungaji 17 Wafukuzwa Kazi Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Askofu kwa uchungu Anena Mazito...............
Uchi unaujua wewe? Hilo kanisa la wavaao uchi litakua la freemason labdaMavazi wanavaa uchi makanisani
Kwa uelewa wangu hakuna mgogoro hapa.ila ni mtu na muajiri wake kuna mambo ya kuyaweka sawa.ni sawa na mwalimu mmoja akisimamishwa kazi kupisha jambo fulani litunzwe.Hapo utasema serikali ina mgogolo na waalimu?Huu mgogoro usije ukawa kama ule wa KKKT Dayosisi ya Konde, Mbeya. Inabidi busara itumike maana hii migogoro kwenye taasisi za dini haileti afya kwa maisha ya kiroho ya waumini wake.
Rejea:
Download Wachungaji 17 Wafukuzwa Kazi Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Askofu kwa uchungu Anena Mazito
Wachungaji 17 Wafukuzwa Kazi Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Askofu kwa uchungu Anena Mazito (6.45 MB) ~ Free Download Wachungaji 17 Wafukuzwa Kazi Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Askofu kwa uchungu Anena Mazito (04:42 Min) mp3 and mp4 ~ Download lagu mp3 & mp4 Wachungaji 17 Wafukuzwa Kazi Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Askofu kwa uchungu Anena Mazito...............
UNAPOSEMA AMENYOOKA UNAKUWA UNA MANA GANI? JE KWAMBA KANISA KKKT LINA MAMBO YSIYOFAA KATIKA JAMII MPAKA HUYO ANAONEKANA NDIYO MAMBO YANAYOFAA? YAANI HAPO NAONA KAMA UMELIPAKA MATOPE KANISA KUWA HALIFAI LABDA KAMA UTATUPA SABABU AU HUYO JAMAA AMENYOOKAJENilijua ipo siku KKKT watamfyatua out aidha kwa figisufigisu ili akimbie mwenyewe.
KKKT haipendagi mtu alinyooka ktk ukweli, sasa jamaa huwa yupo straight forward huwa hapindipindi hata kidogo, so kwa Lutheran hiyo ni kasoro, pia kuna ngoma nyingine Askofu Bagonza huyu nae ni kisiki hawana cha kumfanya make huyu nae ni kichwa kingine ambacho kimenyooka na hakuna mtu mwenye uwezo nacho ndani ya KKKT.
Huyo Kimaro na Mgogo ndiyo wanalibeba kanisa, shida ni kwamba kazi ya Mungu lazima ipate upinzani wa shetani na hao wanao mletea figisu ndiyo mashetani wenyewe
unamzungumzia aliyewahi kuwa Mchungaji mbezi beach kkkt?Duh
Mnamuondoa Eliyona mnamleta Anna?
1 Timotheo 2:12
[12]Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
But I suffer not a woman to teach, nor to usurp authority over the man, but to be in silence.
Ikiwa ya kwamba mnalisaliti neno ambalo kwalo mnajihalalisha kusimamia wengine mtashindwa nini kulana wenyewe kwa wenyewe?
Kkkt kwa kiasi kikubwa inaendeshwa kama chama cha siasa.
Fitina nyingi, uchawa mwingi na hata ushirikina mwingi hasa kwenye uchaguzi.
Hiyo Dayosisi ya mashariki na Pwana ina vita vya mda mrefu kati yake na watu wa ukanda wa kaskazini uliochagiza hata askofu wake Malasusa kuungana na Magu katika mkakati wa kuwademolish hawa watu.
Kuna mch mmoja huko kutoka kanda ya kaskazini aliyekuwa mkuu wa jimbo kwa wivu aliondolewa na kupelekwa huko Mwanarumango.
Sasa wakati Kimaro akitendewa haya yule Maksai wa Kimara Korogwe atie maji na baadae aliyekuwa Ubungo Plaza kabla ya kuhamishiwa Mbezi luis ajiandae kwa panga la Alex G.
Huyo Kimaro na Mgogo ndiyo wanalibeba kanisa, shida ni kwamba kazi ya Mungu lazima ipate upinzani wa shetani na hao wanao mletea figisu ndiyo mashetani wenyewe
Kwenye hili nahisi pastor Kimaro ataenda kujitafakari.
Mimi ni muumini wa KKKT hapo Kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji Kimaro ni kwamba alikuwa anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alishaonywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.
Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.
Kimaro ana kiburi cha umaarufu. Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?
Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazoimba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyopaswa.
Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa KKKT ila najua wachache sana wataelewa hili.
Kama mtaweza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.
Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.
Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.
Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.
Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.
ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
Sasa hata yasipoyumba so what? IMPACT YAO NI NINI? Msifanye vitu kwa mazoea, Kimaro na Mgogo wana injilisha kwa namna yenye kuleta mapinduzi, kimaisha na kiimani
Mbona unapiga kelele mkuu ungeandika kwa font ya kawaida bado ungeeleweka.
Dayosisi imefanya maamuzi sahihi sana, na tena yamechelewa mno.
Huyu na mwenzake wa Kimara ni wachungaji wachache ndani ya kanisa wenye kiburi kilichokomaa na kuzeeka.
Mchungaji amekuwa mtu wa kusema hovyo ili kujipatia umaarufu wa kidunia, ni juzi tu ametoka kusema vijana wa kikristo hawaaminiki na yeye anawaamini sana vijana wa kiislam, hii sio kauli ya kusemwa na Mchungaji.
Mchungaji Kimaro kama kweli ana Mungu ndani yake, atumie hizo siku 60 kijitafakari na kufanya toba, kiburi chake kiliinuka zaidi na akataka kujitwalia utukufu wa Mungu.
Ni muda sasa KKKT iangalie sana watu wa kuwabariki kuwa wachungaji na kuwapa sharika, kutokana na ugumu wa ajira watu wengi wanapigania kuwa wachungaji ili kupata uhakika wa ajira hapo baadae. Kanisa lipime sana watu, lichuje kwa kumshirikisha Mungu.
Washarika wote wanamlilia Mchungaji wakae chini na wajitafakari kama ni wakristo kweli, wanaamini katika Mungu au katika Mchunga?
Mkuu KKKT ilianza kuwa na wachungaji wanawake tangu miaka ya tisini mwanzoni...Tokea lini wa KKT wakawa na wachungaji wanawake
Sema tu wazi Roman Catholic wanabadili sala ili wauze vitabu tutakuelewa ila tutafunga kwa ajili yako 😂😂Halafu wanabadilisha sala na kuziondoa nyingine kimya kimya, ila ukiwa na version za zamani za vitabu vya sala na kuhudhuria ibada muda wote unaushitukia mchezo!
Inategemea unatumia kifaa gani kusoma maandishi yangu, pia afya ya macho yetu inatofautiana.Mbona unapiga kelele mkuu ungeandika kwa font ya kawaida bado ungeeleweka.
Taratibu za kanisa unamaanisha mapokeo, na utaratibu uliotungwa na wanadamu au unamaanisha msingi ulio kwisha kuwekwa na Yesu mwenyewe alisema hakuna atakaye weza kuvunja?.Mchungaji kuhamishwa Usharika sio mgogoro,labda kama huyo mchungaji haendi sawa sawa na kiapo chake cha kichungaji, acheni upambe na mheshimu taratibu za Kanisa.
Kanisa ni waumini au ni Jengo?
Kama ni waumini Kimaro anao mtaji mkubwa.
KKKT MSIKURUPUKE KWA HILINITAWAGHARIMU SANA
Kila taasisi ina taratibu zake, kama umeamua kutangaza neno la Mungu kwa kupitia kanisa la Roman Catholic utalazimika kufuata taratibu zao. Ni nini huelewi hapa?Taratibu za kanisa unamaanisha mapokeo, na utaratibu uliotungwa na wanadamu au unamaanisha msingi ulio kwisha kuwekwa na Yesu mwenyewe alisema hakuna atakaye weza kuvunja?.
Sala gani zilizobadilishwa? Kuanzia tuko wadogo mpka Leo sala ni hzo hzo popote unasali hata usiende miaka MISA haitakupitaSema tu wazi Roman Catholic wanabadili sala ili wauze vitabu tutakuelewa ila tutafunga kwa ajili yako [emoji23][emoji23]