Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
- Thread starter
-
- #41
ndio shida ya kukimbilia wachungaji
wanaoibuka hovyo'mbasha anaumia aisee
ila amuachie mungu tu,kisasi cha mungu ni cha haki
Ha ha ha bongo tatizo uhun mwing bora ukiskia mwinjilist kuliko anayejiita pastor.
Kunyamaza pia neno,huyo Mbasha angenyamaza akamuachia Mungu...........
Sijasema hana haki,nimesema kunyamaza pia neno,atasema watabishana halafu what is next?Anahaki ya kulinda na kutetea kilicho chake kwa njia yoyote ile anayo ona inafaa pia anawajibu wa kutujuza kuhusu hawa matapeli.
ha ha ha ha ha haya bana si unajua hivi vi smart vya wachina wa kijijini havina majukwaa ni kanyaga twende tu kakaEskroo wako jukwa lao huku jukwaa la matanuzi ya weekend.
Ogopa kuchapiwa na mwenye pesa wewe...utabaki unalia tu...by the way Mbasha yuo sahihi...kuliko kufia jela kimya kimya ni bora amesema......Hawa wachungaji sijui rwakatare,Mzee wa Upako,Gwajima na wengine wote ni wasanii tu...ni wezi.....Sema Mungu aonaye sirini anajua vizuri
Mkuu Candid Scope, naona Tabby amepaniki, ingawa kistaarabu sana! Eti Gwajima ana akili kuu...
Umekosea kidogo Mjukuu wangu. Mimi sija punic hata kidogo. Niko vizuri sana kwa hilo. Ungepatia sana kama ungesema nimekasirika.
Kweli wananiudhi sana. Wanaendesha hili suala kama vile hawajawahi kumjua Mungu, lakini pia hawana malezi ya familia? Hata kama kwa sababu yoyote hawakupata malezi bora ya familia, hata kujiunza kwa wenye hekima hakuna? Kama wanakotoka wenye hekima hawapo, siku hizi kuna professional washauri. Wangetafuta hata huyo angewapa mkakati mzuri sana wa kushughulika na hili suala na lingeleta tija kwa wote kuliko uhuni na ujinga wanaoundeleza hapa.
Uliona wapi ndoa ikajengwa kwa matusi na marumbano?
Tangu lini kudhalilishana kulitengeneza mahusiano bora?
Emma anachukua wapambe wahuni wajinga wajinga ndio wanakaa wanamuanika gazetini anadhani ataonekana mshindi kumbe anajididimiza. Hekima Halii?
Narudia tena, tatizo la hawa watoto halikuanza mnavyotaka kulipeleka.
Na chanzo chake si pesa nyingi, gwajima wala admirer mwingine yeyote wa yeyote kati yao.
Huku wanakotaka mushinde mnadharirishana, mnamtumikia shetani na mwisho wake mtahukumiwa tu. Jifunzeni maarifa mtashinda.
Sidhani kama unafika umri wa kuwa babu yangu, angekuwa hai leo anhekuwa na miaka 140 hivi, kanusha usemi.
Napenda navyojiamini, napenda mwandiko wako na napenda mtiririko wako wa mawazo. Huyu mtoa mada si mpambe kama ambavyo wewe umeaminishwa na walio juu yako (ambao msimamo wao ndio sheria). Ni mtu mwenye mawazo huru ambaye pengine ameona umuhimu wa jambo analolisisitiza. Kupanga kwako hoja hakuondoi ukweli kuwa nawe ni mpambe wa upande wa Mchunga Kondoo, a.k.a Baba kama ambavyo nyie humwita.
Najua hisia ulizonazo juu ya wanaoitwa 'watu wa Mungu' (kimsingi wote ni watu wa Mungu) lakini hili haliondoi ukweli kuwa hata hawa wanaweza kuwa wahuni, wadhulumu, wauza unga na wagoni bila kujali wewe unadhani ana ukaribu kiasi gani na Mungu.
Tujikite kwenye hoja, kwanini kaka mkubwa mwenye kondoo wa kutosha hajaona umuhimu wa kututoa tongotongo, hasa sisi ambao tunamuona kuwa mtu wa kawaida ambae ameona fursa kwa jina la Mungu.
Unajua Mphamvu, ni kwa vile hatujawahi kuonana. Siku tukibahatika kukutana, utashangaa kwa nini bado niko hapa naandika na kuandika. Siku hiyo mmoja watu ataabika!. Mimi ni kibabu na wala siwezi kushusha umri.
Binafsi, sijawahi kumwona wala sijawahi kusali kwenye kanisa la Gwajima.
Tatizo angu huwa sina ushabiki kwa sababu katika uzzee huu, sioni sababu ya ushabiki tena. Ninajitahidi kufanya right things.
Hivi unaamini kwamba kwa mkakati huu, wa kushambuliana, kudhalilishana, kuvuana nguo hadharani ndio kuimarisha ndoa?
Unafahamu tofauti ya kuoana na kuishi pamoja kwa mapenzi na kule kuishi pamoja kwa ajili ya sympathy, gratitude, social and community pressure and obligations ama economic insecurities?
Elewa kijana.