LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 18,611
- 27,615
Wanabodi,
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uonga aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?. Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu tuu, lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "kiumbe".Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa, ndivyo Bwana Yesu alivyofundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tuudhi?.
Clip ya Mchungaji Gwajima Akihubiri Mambo ya Dunia Hii na Sii Mambo ya Mungu.
Baada ya Mashekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuridishwa na kazi nzuri iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuwaumbua kwa kuwataja wazi wazi, baadhi ya wabwia unga na wauza unga hadharani, hivyo wakaamua kumuombea dua maalum ya ulinzi, ili Mungu azidi kumlinda, Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, ndipo Mchungaji Gwajima, amemuonea vivu kuwa dua zile zitazidi kumnyooshea mambo yake Makonda, yazidi kuwa mazuri na kumyookea, hivyo Yeye Gwajima,(mwenye utajiri wa ajabu ikiwemo Hammer, Helcopter, na kanisa kubwa), akaamua kumbomoa, na kumponda, na kumsingizia Makonda vitu vya uongo!.
Mahubiri ya Gwajima Kumhusu Makonda.
Katika mahubiri yake ya jana, kanisani kwake Ubungo Maji, Mchungaji Gwajima, amemuelezea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kuwa ni mtu mhalifu wa makosa ya jinai ya fojari ya kuiba jina la mtu mwingine, na kosa la kughushi kwa vyeti vya mtu mwingine na kujipatia elimu kwa njia ya udanganyifu, na alikwenda mbali zaidi hadi kudai kuwa eti jina analotumia Paul Makonda, sii jina lake halisi, bali ni jina la wizi, jina la ku foji, na kueleza kuwa ni jina la mtu mwingine kabisa ambaye yupo!. Mchungaji Gwajima, alikwenda mbali zaidi kwa kulitaja jina halisi la Makonda ni Daudi Albert Bashite!.
Swali ninalojiuliza, huyu Mchungaji anawezaje kuusema uongo kama huu kwa waumini wake na hadi sasa hajachukuliwa hatua zozote za kisheria?!.
Jee ni Kweli Mkuu wetu wa Mkoa, Paul Makonda ni Mhalifu?.
Mkuu wa Mkoa, ni mteule wa rais, mtu huwezi kuteuliwa kushika wadhifa wowote na rais wa JMT, kwa sababu kwa kawaida, kabla mtu yoyote, hajateuliwa kushika madaraka yoyote, hufanyiwa vetting na vyombo husika, hadi kijijini kwake alikozaliwa, hivyo haiwezekani kabisa Mhe. Paul Christian Makonda, ambaye ndie Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akawa ni mhalifu aliyefoji vyeti, hadi yeye Gwajima akagundua na kutangaza kanisani kwake, wakati tuna vyombo vya uchunguzi na ulinzi na usalama ambavyo vilipaswa kulijua hili. Mchungaji Gwajima atakuwa ni muongo!. Kama kweli Paul Makonda ni majina bandia, na amefoji vyeti, saa hizi, asingekuwa bado ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, bali angepaswa kuwepo pale mahali wahalifu wengine wote wanapaswa wawepo!.
Kwa Magufuli ninayemfahamu mimi, kama hizi tuhuma kuhusu Makonda zingekuwa na ukweli wowote, saa hizi, zamani angeishatumbuliwa!. Kitendo cha Makonda anaendelea kudunda mpaka sasa, huu ni uthibitisho, tuhuma hizi ni uongo za kupikwa tuu na wabwia na wauza unga!.
Mchungaji Gwajima ni Zaidi ya Mbunge, Zaidi ya Waziri, Zaidi ya Rais?!.
Kwa vile Bwana wetu Yesu Kristu, ametufundisha, namna ya kuwatambua manabii wa uongo, ni kuwatambua kwa matendo yao, jee Yesu aliwahi kujitapa kuwa yeye ni zaidi ya yeyote?. Alipopelekwa kwa Pilato kwa kosa la kutaywa "Yesu Mnazareti Mfalme wa Mayahudi", licha ya Yesu kuwa ni Mfalme kweli, alinyamaza kimya, na alivyosisitizwa, akasema "wewe wasema", sasa iweje Mtumishi wa Mungu, Mchungaji akajiinua kuwa yeye ni zaidi ya rais wa nchi?, na kuwa kugombea urais kwake ni demotion!. Hivi kwa mtumishi wa Mungu wa kweli, anaweza kusema maneno kama haya madhabahuni kwa Mungu, au Mchungaji huyu, ni wale Manabii wa Uongo, Bwana wetu Yesu Kristu aliotuhusia?.
Msikilize Mchungaji Dr. Josephat Gwajima. Sikiliza Kwa sikio la roho, na sio sikio la mwili.
Mimi nimeisikiliza hii clip hii ya Mchungaji Gwajima, akimzungumzia Daudi Albert Bashite, A.K.A Paul Christian Makonda, akidai kuwa kilichomponza yeye Mchungaji Gwajima hadi kusingiziwa madawa ya kulevya, ni dhana kuwa anataka kugombea ubunge jimbo la Misungwi, kufuatia kutua kijijini Kolomije kwa Chopa, (Helcopter), hivyo Daudi Bashite, A.K.A Paul Makonda anajipanga kugombea jimbo hilo mwaka 2020!. Mchungaji Gwajima akajitapa Ubunge, Uwaziri hadi Urais kwa Mtumishi wa Mungu aliye hai ni demotion!. "Mtumishi wa Mungu ni zaidi ya Rais wa nchi!". Jee hii ni kweli?.
Daudi Albert Bashite, A.K.A Paul Christian Makonda "Kiumbe Huyu"
Akielezea kuhusu Daudi Albert Bashite, na yeye Mchungaji Gwajima, ni watu wa kabila moja na wametokea kijiji kimoja cha Kolomije. Daudi Bashite alisoma Shule Msingi ya Kolomije hadi darasa la tano, akahamia Shule ya Msingi ya Nyanza hadi akamaliza Darasa la 7, hakuchaguliwa, lakini akajiunga na Shule ya Sekondari Pamba ambayo ni ya serikali kwa jina jingine, akiwa anakaa kwa mama Kamese (Gwajima ana simu yake) ambako alipata Divisheni 0, ndipo dada mmoja wa Kihaya kwa jina la Christina (Gwajima ana simu yake) akamuunganishia Daudi Albert Bashite, kwa mdogo wake, Paul Christian, hivyo Daudi Bashite akaanza kutumia cheti cha kaka yake Paul Christian ndipo akajiunga Nyegezi kusomea certificate ya uvuvi kwa jina la Paul Christian Makonda, kisha akajiunga Chuo cha Mbegani Bagamoyo kuchukua diploma ya uvuvi na kumalizia Chuo cha Ushirika kuchukua degree kwa majina ya kughushi ya Paul Christian. Huu jamani sio uongo huu?.
Katika kumuelezea Daudi Bashite, Mchungaji Gwajima amemuita "kiumbe huyu", hili sio neno zuri kwa kiongozi wa dini ya Mungu kweli, kumuita binadamu mwenzako kiumbe!.
Vyeti vya Daudi Albert Bashite na Paul Christian Makonda Mezani Kwa Gwajima.
Ila pia Mchungaji Gwajima amedai, anavyo vyeti vyote ofisini kwake tangu cha Daudi Albert Bashite alichopata Divisheni 0. hadi cheti cha Paul Christian alichounganishiwa na Christina!, na kudai kuwa ana mshitaki Makonda kwa Ndalichako na kwa Magufuli, na asipochukuliwa hatua zozote, yeye atashangaa sana na atavitoa vyeti hivyo hadharani, umma uvione. Hii naweza kuwa kweli?, huu sio uongo mwingine huu?!. Mtanisamehe, mimi ni Tomaso, na hapa namwita Mchungaji Gwajima ni muongo hadi atakapo vitoa vyeti hivi hadharani tuvione ndipo nitaamini!.
Hoja 20 za Uongo Kumhusu Paul Makonda
1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.
2. Majina yake halisi ni Daudi Albert Bashite
3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bashite. Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.
4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).
5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.
6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamba.
7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero).
8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg.Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.
9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.
10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg. Benjamin Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Meya wa Kinondoni kwa sasa). Wakawa marafiki.
11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi, aliombaadmission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini akakosa nafasi.
12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.
13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).
14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokuwa akisoma (akawa discontinued).
15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza first yearakiwa na carries 3 ambazo alienda nazo 2nd year. Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wacarry over na supplementary. Akaamua kuacha chuo.
16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.
17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya. Akaachana na CMA akachagua Community & Economic Development (CED).
18. Mwaka 20012 akahitimu shahada ya kwanza ya Community & Economic Development kwa jina la Paul C Makondabadala ya majina yake halisi ya Daudi Albert Bashite
19. Jina Makonda analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda baada ya kuapa mahakamani.
20. Ndugu Daudi Albert Bashite ameoa (tangu mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa.
Hoja Moja ya Kweli Kumhusu Paul Makonda
Paul Makonda ndilo jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliyeteuliwa na Rais wa JMT. Jina la Paul Christian Makonda ndilo jina lake na elimu yake ni Shahada ya Chao Kikuu.
Mengine Yote ni Uongo Mtupu. Ukweli ni hiki kilichopo Sasa kuwa Paul Makonda ndiye Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Huyu ni mchungaji wa Mungu au mungu. Hili la kudai anavyo vyeti vya Daudi Bashite na Paul Christian, Jee hii inaweza kuwa kweli?!. Nijuavyo mimi, mtu ulikuwa ukipata Div. 0 hupewi cheti chochote na NECTA zaidi ya Leaving Certificate, sasa hicho cheti cha Daudi Bashite alichonacho Mchungaji Gwajima, kimetoka wapi?. Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo madhabahuni, jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu, au ndio hawa wachungaji wanaomtumikia mungu?!.
Jumatatu Njema.
Paskali
Gwajima aachane na malumbano ya kidunia. Atawapoteza waumini wengi sana kama ataendelea kutoa mipasho kwa watu Aina ya makonda. Yeye kama askofu mkuu mwenye waumini wengi agekaa kimya afundishe waumini wake namna ya kukabiliana na mikasa anayokutana nayo.Vinginevyo ataonekana si mtumishi wa Mungu aliye hai.Si vizuri kutumia madhabahu ya Mungu kwa namna hii.Watu wanaenda kanisani kusikia habari za matumaini katika imani zao na kufarijiwa wanaishia kupokea habari za makonda na Albert. Hebu askofu avue kola na atafute jukwa muafaka tofauti na madhabahu. Atekwaza washirika wengi na watamkimbia.Ajikite katika kufundisha neno la kweli la Mungu.Vinginevyo waumini watamuona si askofu wa kweli