Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Gwajima aachane na malumbano ya kidunia. Atawapoteza waumini wengi sana kama ataendelea kutoa mipasho kwa watu Aina ya makonda. Yeye kama askofu mkuu mwenye waumini wengi agekaa kimya afundishe waumini wake namna ya kukabiliana na mikasa anayokutana nayo.Vinginevyo ataonekana si mtumishi wa Mungu aliye hai.Si vizuri kutumia madhabahu ya Mungu kwa namna hii.Watu wanaenda kanisani kusikia habari za matumaini katika imani zao na kufarijiwa wanaishia kupokea habari za makonda na Albert. Hebu askofu avue kola na atafute jukwa muafaka tofauti na madhabahu. Atekwaza washirika wengi na watamkimbia.Ajikite katika kufundisha neno la kweli la Mungu.Vinginevyo waumini watamuona si askofu wa kweli
 
Mbona hueleweki, unaulizia swali huku unalo jibu lako kichwani...... Haya basi wewe si unaamini ni wa uongo. Tufanye wa uongo
 
U have a point ...na mimi pia naona hana hekima zaidi ya kupandikiza chuki
 

Ndugu Paskali dawa ya uwongo ni kusema ukweli ukiambatana na vielelezo maridhawa ili uwongo ujitenge. La msingi hapa ni kumshauri anayesingiziwa kufoge vyeti kutueleza form I - IV alisoma wapi kwa jina gani na alikuwa na akina nani darasani. Kukaa kimya mara nyingi ni kukosa majibu yenye mashiko. Kama ni mkristo wa kweli anweza hata akaweka cheti cha ubatizo au kipa imara katika kupinga uongo unaozagaa kwa kasi. Sasa taabu iko wapi katka kudhihirisha hili??????
 
Pasco kajitoa fahamu njaa mbaya sana.
inasikitisha sana. halafu kaunganisha pesa na ukabila. ni sawasawa na kujikana. angalia uandishi wake na jinsi alivyojitoa ufahamu ni ukweli usio pingika amehongwa ili kuzima moto. nadhani aliyemuhonga ndiye aliyeliwa. hela zimekwenda bure ila hii kasheshe haitapita. gwajima kasema rais akikaa kimya yeye ataibuka upya so mjadala utaibuka upya. Lugumi walijitahidi sana kuizima humu na upande wa pili wakajitahidi sana kuendelea kuwasha moto leo hii Kitwanga yuko wapi?? Rais kwa kutumia vyanzo vyake nae anatafuta ukweli wa jambo hili. na vyanzo vyake havitamficha ukweli. vitamweleza mzee ishu hii ni kweli au sio kweli mbona ni rahisi sana? makonda kuliko kuhonga ni bora hela hizo angezitumia kujiandalia biashara ya kufanya. watu walikula sana hela ya kitwanga lakini wapi. na kitwanga ni swahiba mkubwa sana wa magfuli kuliko huyu. huyu ni ukabila tu ndio umembeba sio uswahiba. kweli njaa mbaya sana
 
Sisi wauminu hatujui hasa nani mkweli katika haya mambo ya imani..la msingi ni watu kumjua Mungu basi mengineyo yatajijua mbele kwa mbele
 
Hajasema ana matokeo, amesema ana vyeti mezani kwake, hivi kweli kuna cheti cha divisheni 0 ya miaka hiyo?.

Paskali
Ndugu yangu Paskali, achana nao wote wawili( Makonda and Mchungaji Gwajima) Hata Makonda anawaita watu vichaa na kwamba yeye ametauliwa na Mungu kuwa mkuu wa mkoa. Na kwamba aliposimama Mkonda Mungu yupo. Wanafanana
 
Wote mnakumbuka sokomoko la Mch. Gwajima na Dr. Slaa, pia la Mch na Askofu Pengo na sasa hili la kwake na Mh. Daudi. Mara zote amekuwa akiibuka na ushahidi uliyokamili kiasi cha kuwafanya wapinzani wake kukaa kimya.

Je ni nani aliye nyuma yake?

Na nini utakuwa mwisho wake, kwenye nchi za aina ya Afrika?
 



COURAGE

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…