Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Uandishi na msimamo huu sometimes nashangaaaa. Gwajima either ni mchungaji au nabii wa uongo au tapeli hiyo ni juu yake na Mungu wake when it comes kwa kiongozi wa watanzania tunayo haki ya kujua. Tuache kutetea kitu ambacho kipo wazi ni udanganyifu sasa kama waandishi mnaandika kwa kuabudu au kukumbatia watu basi bado tuna Safari ndefu. Gwajima Mungu atamhukumu kwa jinsi yake na Daudi atahukumiwa na watanzania kwa jinsi yake period!
 
Gwajima ni mwanamikakati tu. Nchi hii ina wachungaji wengi Sana kwa nini gwajima ana trend sana mitandaoni peke yake tu ?
 
Kuna siku Makonda alimdhalilisha mama wa wa watu live kwenye moja ya mikutano yake nanukuu "Hawa ndio wale vichaa tunaowatafuta" personally niliumia na watu kama sisi ndio wengi tupo nyuma ya Gwajima.
 
Kwani unamjua aliyekuwa nyuma ya RC wakati anataja majina ya wauza sembe na watumiaji?

 
Kwani leaving certificate ni nini?Na statement of results/result slip kwa kiswahili inaitwaje?
 
L
 
Kuna siku Makonda alimdhalilisha mama wa wa watu live kwenye moja ya mikutano yake nanukuu "Hawa ndio wale vichaa tunaowatafuta" personally niliumia na watu kama sisi ndio wengi tupo nyuma ya Gwajima.
huyu jamaa analaana ya watu wengi ukipitia hiyo thread halo chini utagundua mengi
Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu
 
Nilifikiri paskali ataleta ushahidi kuwa Makonda sio Daudi Bashite badala yake ni hukumu tuu nakejeli kwa Gwajima.yote haya ni sababu yakujipendekeza kwani huyu Pascal anafahamika kwa hilo.


Hili jambo ni rahisi sana anayesemwa ni Daudi Bashite atoke na vyeti vyake OG na kuuthibitishia umma kuwa yeye sio Daudi ni PCM.

Kuna wakati trump alimwandama Obama kuwa si mmarekani kwa sababu hakuzakiwa marekani. Obama mwanzoni alipuuza ila nadhani alishauriwa aonyeshe cheti chake cha kuzaliwa ili kumaliza ubishi na anafanya hvo...ingawaje yeye alisema ni jambo la kipuuzi ila kwa kiasi fulani lilimaliza kikichokuwa kinaendelea. Ingawa kuna baadhi waliendelea na msimamo wao kuwa siyo mmarekani.

PCM toka na vyeti vyako wainyeshe watanzania kuwa wewe si DAB Bali wewe ni PCM...ikiwezekana hata na cheti cha kuzaliwa uonyeshe ili kumaliza hii kitu once na for all.

Ukishaonyesha wa kuamini ataamini na wa kutokuamini ataendelea kutokuamini na baada ya hapo endelea kuchapa Kazi kama siafu.

Ukiendelea kukaa kimya kwa madai eti siwezi kuwajibu wapiga kelele unatufanya tuamini yanayosemwa juu yako ni kweli.
 
Pascal Naona Umeamua kujikosha baada ya ile hoja yako ya kuhusu wanaume wa kisukuma, Kwanza wewe ni mwandishi wa habari tena wa muda mrefu sana na unajua kuwa hoja upingwa kwa hoja, umesema unakubaliana na hoja Moja Kati ya hizo 20, sasa kama unasema hoja hizo nyingine ni za uongo uko wapi ushahidi? Mbona ni nadharia tuuuu?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…