Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Bila ujasiri wa huyu jamaa, watu wengi wangesotea sero, maana yule jamaa alishapanga mpaka awamu saba
 
Haiwezekani amuite Mkuu wa Mkoa kiumbe...ni kosa kubwa sana
Kosa kubwa kivipi, binadamu, wanyama wote waliopo duniani, nchi kavu na majini, miti pamoja na mimea yote ni viumbe.., bashite is no exception.
 
Dini ni kweli inakataza kulipa kisasi kwani inasema kisasi kulipiza ni kazi ya Mungu mwenyewe. Gwajima ameingia kwenye ubinadamu zaidi na kumwacha Roho wa Mungu pembeni. Kwani yeye ilitakiwa amwombe Mungu aingilie kati kuonewa kwake naye angejidhihirisha na kuchukua hatua azijuazo yeye Muumba. Pia kunawakati huwa yupo sahihi kwani kazi ya watumishi wa Mungu ni kukosoa na kukemea pale haki inapopotoshwa au kudhulumiwa. Pia nivyema makonda akaweka vyeti vyake hadharani kwani taaluma sio siri ili kukata mzizi wa fitina.
 
Umenukuu vifungu vya biblia vizuri kabisa. Ila tafsiri unayotaka kuambatanisha navyo inaniogopesha. Kuwa mkristo sio kuja kutetea uovu kwa kigezo cha upendo. Sio kunyamazia ubaya fulani eti usionekane una hasira. Ukristo sio kuogopa kufunua vyeti feki eti usionekane huwezi kusamehe.

biblia inasema mtu akikosea akaja kuomba msamaha" msamehe. Awali kabisa gwajima alisema daudi aombe msahama kabla chungu hakijapata moto zaidi. Daudi akakausha. Sasa mkuu unaponukuu habari ya msamaha bila mwombaji kuhitaji msamaha una maama gani? Sisi tunafundishwa kwamba Mungu ni wa rehema tukiziungama dhambi zetu, je usipotubu, Mungu anawezaje kukusamehe?

Namalizia kwa kile kiitikio chetu "wacha maneno weka vyeti"
 
Ukweli ni kwamba sijawahi mwamini huyu mwinjilisti. Imani yangu kwake ilitoka pale alipokuwa anamshauri Rais magufuli kuwa ajitoe ndani ya ccm na urais wake na kujiunga na chama kingine. Angewezaje kkuvua uanachama na kubaki na urais?
Lakini pia katika hili sakata lake na mh.makonda,mara ya kwanza alisema makonda alimaliza kidato cha nne pale pamba sec.na akapata zero,juzi anasema kuwa alifukuzwa,ukweli ni upi? Anatueleza pia kwamba ana cheti cha daudi bashite na kwamba ana zero,kama kweli makonda alihitimu mwaka 2000, Mimi nilihitimu 2001,div.0 walikuwa hawapewi vyeti.gwajima kakipata wapi?
Kwakeli gwajima anaongea sana,na amepata washabiki wengi,ila Mimi simwamini kwakuwa tangu nianze kumsikiliza nimekosa kumwelewa hasa kwenye mwendelezo wa story zake,na uelewa wako juu ya mambo ya kawaida.
Ni maoni yangu tu.
 
Suluhisho ni kwa mkuu wa mkoa kutoa vyeti vyake tu hlf wote tutamdharau Gwajima, atoe hata kadi ya kliniki iliyoandikwa Paul basi mchezo utakuwa umeisha, vingine askofu ataendelea kuwa shujaa!
 
Ushujaa wa askofu hautatokana na makonda,ushujaa wake itategemea jinsi anavyowaandaa kondoo wake kwa haki na kweli ili kuurithi uzima wa milele.
 
Kama ww haumuani Gwajima. je ww unauona ukweli ni upi hususu Bashite au Makonda?
 
Gwajima na Makonda nani Haaminiki? nani mbabaishaji na anaeshindwa kuthibitisha ukweli.
 
Unaonaje bashite nae atoe vyeti then upigilie kabisa msumari kwa Gwajima kutomkubAli kabisa hebu mshauri iko kitu bwana bashite
 
Result slip ya nini wakati MTU kapate divisheni ziro,sufuri au 0? Hakuna kitu kama hicho.
 
Asante sana Paskali,
Pamoja na kwamba si kubahatiwa kusoma kwa umakini mkubwa mwanzo mwisho wa andiko lako lenye uchambuzi wa kina, hoja moja ni dhahiri hata mimi ninamuunga mkono Mchungaji Gwajima. Kiongozi wa kweli wa kiroho ni zaidi ya rais wa nchi. Wakati rais anaweza kuwabagua watu kwa ajili ya maslahi ya chama chake , kiongozi wa kiroho hawezi akawa na "hawa ni wangu na hawa sio". Wakati rais anaweza kuwateua wateule wake kwa kuwafahamu tu na kulipa fadhila kwa au kumpingia kura au kumsaidia kupandisha ngazi fulani huko nyuma, kiongozi wa kiroho anawaona watu wote ni sawa.

Na kwa marais wa siku hizi, wenye chuki na watu, visasi nk. nidhahiri kuwa kiongozi wa kweli wa kiroho ni zaidi ya rais. Na kuna wakati nashawishika kuaamini kuwa hata baba wa familia anayejitambua anazo sifa za ubora kuliko hawa marais wa siku hizi. Baba wa familia hawezi kutengeneza njama miongoni mwa watu wake. Hana upande.
 
Kama kwa kufichua vyeti vya Daudi Bashite ndiyo unamuita Nabii wa uongo, acha awe na mimi binafsi ndiyo nitazidi kumpenda na Jumapili nitaenda pale kanisani kwake kusali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…