iipwisa
Member
- Feb 1, 2013
- 36
- 7
Aende zake badala ya kufanya Kazi ya mungu anang'ang'ania umbea tu tu sjui kala maharage ya Jana??WE ngoja akuBASHITE na wewee ndo utamjua
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aende zake badala ya kufanya Kazi ya mungu anang'ang'ania umbea tu tu sjui kala maharage ya Jana??WE ngoja akuBASHITE na wewee ndo utamjua
anayofanya pia ni kazi ya mungu anasafisha kuondoa hizi taka aina ya BASHNETDAUDIAende zake badala ya kufanya Kazi ya mungu anang'ang'ania umbea tu tu sjui kala maharage ya Jana??
Hahahaha haya buana Ila bíblia inasema vya kaisali MPE kaisali na vya mungu MPE mungu.......anayofanya pia ni kazi ya mungu anasafisha kuondoa hizi taka aina ya BASHNETDAUDI
Hahahaha haya buana Ila bíblia inasema vya kaisali MPE kaisali na vya mungu MPE mungu.......
Mi pia ameshaanza kunikera, ni bora kwenye ibada yake aweke segment inayoitwa makonda kabisa
Kosa kubwa kivipi, binadamu, wanyama wote waliopo duniani, nchi kavu na majini, miti pamoja na mimea yote ni viumbe.., bashite is no exception.Haiwezekani amuite Mkuu wa Mkoa kiumbe...ni kosa kubwa sana
Umenukuu vifungu vya biblia vizuri kabisa. Ila tafsiri unayotaka kuambatanisha navyo inaniogopesha. Kuwa mkristo sio kuja kutetea uovu kwa kigezo cha upendo. Sio kunyamazia ubaya fulani eti usionekane una hasira. Ukristo sio kuogopa kufunua vyeti feki eti usionekane huwezi kusamehe.Hivi kati ya watumishi wa Mungu, Gwajima naye ni mmojawapo? Hata kama kakosewa kama anavyodai, je yeye neno la kusamehe huwa linampita pembeni? Au akisoma Biblia vifungu vinavyohusu kusamehe huwa vinafutika? Huwa anawafundishaje waumini wake kuhusu somo la msamaha?
Mathayo 6:14-15 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba wenu wa mbinguni atawasamehe ninyi bali msipowasamehe watu makosa yao wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu."
Waefeso 4:32 "Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma ninyi mkasameheane kama na Mungu katika kristo alivyowasamehe ninyi."
Mathayo 18:21-22 "Kisha petero akamwendea akamwambia Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi nami ni msamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia sikwambii mara saba bali hata saba mara sabini."
1 Wakorintho 13:4, 5. “Upendo ni wenye ustahimilivu na wenye fadhili. Upendo hauna wivu, haujigambi, haujivuni, haujiendeshi bila adabu, hautafuti faida zake wenyewe, hauchokozeki. Hauweki hesabu ya ubaya. Haushangilii juu ya ukosefu wa uadilifu, bali hushangilia pamoja na kweli. Huhimili mambo yote, huamini mambo yote, hutumaini mambo yote, huvumilia mambo yote.”
Unaonaje bashite nae atoe vyeti then upigilie kabisa msumari kwa Gwajima kutomkubAli kabisa hebu mshauri iko kitu bwana bashiteUkweli ni kwamba sijawahi mwamini huyu mwinjilisti. Imani yangu kwake ilitoka pale alipokuwa anamshauri Rais magufuli kuwa ajitoe ndani ya ccm na urais wake na kujiunga na chama kingine. Angewezaje kkuvua uanachama na kubaki na urais?
Lakini pia katika hili sakata lake na mh.makonda,mara ya kwanza alisema makonda alimaliza kidato cha nne pale pamba sec.na akapata zero,juzi anasema kuwa alifukuzwa,ukweli ni upi? Anatueleza pia kwamba ana cheti cha daudi bashite na kwamba ana zero,kama kweli makonda alihitimu mwaka 2000, Mimi nilihitimu 2001,div.0 walikuwa hawapewi vyeti.gwajima kakipata wapi?
Kwakeli gwajima anaongea sana,na amepata washabiki wengi,ila Mimi simwamini kwakuwa tangu nianze kumsikiliza nimekosa kumwelewa hasa kwenye mwendelezo wa story zake,na uelewa wako juu ya mambo ya kawaida.
Ni maoni yangu tu.
Result slip ya nini wakati MTU kapate divisheni ziro,sufuri au 0? Hakuna kitu kama hicho.Aisee kumbe wengine mmesoma kw kukariri,kwani akiwa na result slip si ni cheti pia?
Nyinyi mnawajua watumishi wote wanaosali kwa gwajima je kama wamempelekea ushahidi huo wa kuprint hata kama ni document sio cheti?pascally wewe nina wasi wasi utakuwa ni mhanga kama daudi bashite.
Asante sana Paskali,Wanabodi,
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.
Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.
Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, Makonda alipewa tuu list yenye majina na kazi yake ilikuwa ni kuwataja tuu, aliyemtaja Gwajims ni muumni wake mtiifu, koss ls Makonds ni lipi?!.
Jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa, kwa ubaya na kumsingizia uongo, ndivyo Bwana Yesu alivyofundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?!. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kuume mgeuzie na la kushoto. Adui mpende. Samehe saba mara sabini. Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo? .
Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.
Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.
Paskali
Jumatatu Njema.
Paskali