Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Kwanza tudhibitishie alizunguka mkoa upi na upi kumnadi huyo unayemuita fisadi ambaye mnaogopa ata kivuli chake achia mbali kumfunga.
 
Hajasema ana matokeo, amesema ana vyeti mezani kwake, hivi kweli kuna cheti cha divisheni 0 ya miaka hiyo?.

Paskali
pascal mayala unaboa sana. halafu acha kuchafua wenzako, nahisi kuchafuliwa kunauma sana, na wewe unaweza kuwa unajua iyo experience kama alivyosema jamaa hapo nyuma kwamba wewe pia ulihangaika kweli kujisafisha hapa baada ya kusemekana una practice ukameron. kama ni kweli sawa, lakini kama sio kweli nahisi itakuwa ilikuuma sana, na ikizingatia mkeo ameachana na wewe watu ndio watapigia mstari kabisa kwamba mama alikimbia mdada mwenzie. the same way uache kuhangaika kwenye mitandao kuchafua na kutoa conclusion kwenye maisha ya wenzio, tafuta maisha yako ili uheshimike. la sivyo hata wewe kuna mengi yapo gizani yakiwekwa nuruni utatamani ardhi hii ipasuke uingie.
 
Naheshimu sana michango yako senior Pascal Mayalla,lakini kwa baadhi ya maeneo nikitafakari kwa utulivu napata shida sana kukuelewa,UNAPOSEMA GWAJIMA AMESEMA UWONGO,unamaanisha nini,na huo uongo ni upi,na kama alichosema Gwajima ni uongo,ukweli ni upi basi,ni vema ukathibitisha uwongo wa Gwajima kwa kuweka ukweli halisi bayana.

Pascal,wewe ni mwanasheria,unadhani unachosema ni sawa katika misingi ya kisheria?
GWAJIMA atabaki kuwa mkweli kwa swala zima la vyeti vya MAKONDA,mpaka MAKONDA aje na vyeti vyake Hadharani,kuthibitisha Uwongo wa GWAJIMA.

Ni ukweli usiopingika kwamba hata wenye vyeti vyenye UTATA katika zoezi zima la uhakiki kwa watumishi wa umma,ili kumaliza utata wao WAMEAMBIWA WAENDE BARAZA LA MITIHANI NA VYETI VYAO HALISI.wala hakuna sababu ya kukesha kumtetea BASHITE,GWAJIMA WAS AND STILL IS,RIGHT UNTILL MAKONDA PROVE IT OTHERWISE!!
 
Nahisi kama vile unapoteza muda na nguvu nyingi kujaribu kumuelimisha mtu ambaye kajitoa ufahamu kwa makusudi vile....!!
 
Mkuu Genta, kwanza pole kwa uzi wako huu kuunganishwa kwangu!, nimelisoma bandiko lako na maudhui yake, ni tofauti kabisa na uzi wangu.

Mode: Uzi wangu ulizungumzia unabii wa mchungaji Gwajima kama ni nabii wa kweli au wa uongo, uzi huu unamzungumzia Mchungaji Gwajima kuchanganya dini na siasa. ni vitu viwili tofauti.

Paskali
 
You're wrong these two are inseparable. Unamjua mtu anayeitwa Musa? Huyo alikuwa mtumishi wa Mungu na alifanya siasa alipokwenda kuwakomboa wana wa Israeli kutoka utumwani misri. Lakini pia huyo mnaye mwita fisadi papa mbona hamumpeleki kwenye mahakama ya mafisadi ambayo tunaambiwa imekosa wateja? Au huo ujenzi wa hiyo mahakama
 
Kwa sa
Sasa mbona Lowassa na Maalim Seif wanaulilia sana urais? Kwa nini wasiwe wachungaji?
Mkuu kwa sababu uchungaji ni kazi ya kiroho zaidi kuliko uraisi. Ni wale walio rohoni tu ndiyo watakuwa wachungaji. Kiroho Gwajima is right, uchungaji ni zaidi ya uraisi. Ukiwa mchungaji mwema faida yake ni eternal wakati uraisi hata ukichakachua ni miaka kumi tu. halafu unakaa nasi benchi.
 
Hajasema ana matokeo, amesema ana vyeti mezani kwake, hivi kweli kuna cheti cha divisheni 0 ya miaka hiyo?.

Paskali
Mayala naona nawe sasa umeazimwa kama ilivyo kwa akina Lemutuz! Mayala elewa kuwa mtu anapotaka kukutumia ili kumsafisha au kumsemea anakuwa tyr amejua akili yako ni nyepesi sana! Kuwa makini mkuu utapoteza credibility yako mkuu.
Ila kuhusu Gwajima ni 'mpiga deal' kama walivyo wengine wanaotumia jina la Yesu na nchini wako wengi tu.
 
Bottomline ni kuwa wanadamu wote ni unpredictable na waongo. Huyu anayesema yeye ni rais wa wanyonge ni kweli? msemakweli ni mpenzi wa Mungu, ni kweli anasema kweli? etc, etc, etc,
Hivyo ya Gwajima ni kama ya wengine, hata wewe Paskali! Kuna wanaokuona hivyo kumpenda Katili! Hata mimi kuna wanaoniona katili, mwongo etc! La muhimu tusiende kwenye extremes kuwapoteza wenzetu! Tumpinge Gwajima, tusimuue, tusimtoe roho!
 
Kweli alizunguka nchi nzima?
 
Mayalla uhome boy umemmaliza, hatuna mwandishi tena
 
Pascal Mayalla,
Kuna aina mbili za injili
1.Kuna injili ya kikoloni
2.Na kunainjili ya kweli

Injili ya kikoloni imemeza wengi ndio maana watu hawataki.

Uwe unatoa maelezo vizuri hasa na ushaidi mzuri, siku io alio ongea hayo nilikwenda kwakua kulikua kuna habari ya makonda.

Alisema hivi "hawezi gombea ubunge ama uraisi kwakue yeye alie mpa kazi hiyo ni Mungu mwenyewe rais kaajiliwa na wananchi na swaiba wake kaajiliwa na raisi hivyo yeye ni zaidi kwakua amepewa kazi hiyo na Mungu "
 
Sasa mbona Lowassa na Maalim Seif wanaulilia sana urais? Kwa nini wasiwe wachungaji?
Kila mtu ana wito wa aina yake, huwezi wapangia watu wafanye kazi ambayo si wito wao. Wewe huwezi panga hatma ya wanadamu wenzako maana wewe si Mungu. Wao wito wao ni uanasiasa na Gwajima wito wake ni uchungaji. Kaa uelewe kwaamba haitakaa ije kutokea binadamu wote wakawa na wito wa aina moja. Ikiwa hivyo basi hata dunia itapoteza ladha yake.
 
Ni rahisi sana muumini wa kawaida kuingia mbinguni kuliko mchungaji kuingia mbinguni. Trust me
Haya ni maoni yako binafsi. Kwa Mungu hakuna lisilowezekana. Kama jinsi ilivyo kwa waumini kwamba kuna watakaoingia na watakaoshindwa, kadhalika ndivyo ilivyo na kwa wachungaji. Mungu ni Mungu wa haki na ndani yake hakuna udhalimu wowote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…