Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Mkuu unataka Kiongozi wa kidini (kiroho) awe sawa na Hawa wanasiasa??? Wanasiasa ndio zao.. Je Hawa wachungaji ni sahihi?
Kwa dunia ya sasa siasa ndio mfumo na mzunguko wa maisha yote... "Siasa ni sayansi"(Dr. Slaa) sio kama unavyofikiria wewe, kila kitu ni siasa... Hivyo basi ni vigumu wachungaji, mapadri mashehe kutozungumzia siasa.. Siasa ikivuruga amani, uhuru wa kuabudu unapotea......
 
Umesema kweli Mkuu. Lakn sasa katika ugomvi wao, kimengia kitu chenye public interest.....
Mkuu hawa wote ni viongozi mmoja wa kiroho na mwingine wa umma na wote wapo Dsm hivyo siyo busara kugombana waziwazi, busara za wazee zitumike, hawa wazee wakina Warioba, Paul Bomani, Mangula ndiyo kazi zao hizi.
 
Tulieni anyoooshwe,Gwajima kasema,ukinijia kwa mbwembwe unazo zijua ww,mimi nikikupiga unapotea mazima.Mr David ndo kiama chake.

Hata siku ile wakati anahubiri kanisani baada ya kutajwa katika list ya unga, alitoa mfano wa akina Abel ana Abedinego.... Akasema, kama ni kweli anatumia au kuuza madawa ya kulevya Mungu na ampatilizie mbali. Lkn pia akasema kama amesingiziwa, basi Mungu wake ataushusha moto mkubwa kwa yule aliyemsingizia...... Naanza kupata ka-wasiwasi fulani hii inaweza kuwa retribution...
 
Kwa dunia ya sasa siasa ndio mfumo na mzunguko wa maisha yote... "Siasa ni sayansi"(Dr. Slaa) sio kama unavyofikiria wewe, kila kitu ni siasa... Hivyo basi ni vigumu wachungaji, mapadri mashehe kutozungumzia siasa.. Siasa ikivuruga amani, uhuru wa kuabudu unapotea......
Wanasiasa wanawachokonoa wachungaji kwenye TV unataka wao wakae kimya?
 
Jamani, pamoja na vyeti nk, lakini vita iliyopo mbele yetu ni madawa ya kulevya.tafadhali hata kama makonda aliishia chekechea,kama ana dhati ya kusaidia taifa liondokane na huu uchafu tafadhali apewe nguvu.kabla bw makonda hajaingia kwenye hii vita hatukusikia habari hii ya kufoji vyeti. Twaona magenge ya walanguzi na madalali wa unga sasa wameungana kumshughulikia kila eneo.tuacha unafiki tutokomeze hiili baa linaharibu vijana
Hivi unaposema tuache unafiki unamaanisha kweli???
Au umesema bila kutafakari impact ya neno hilo..
 
Mambo ya wachungaji ni magumu sana kama ilivyo mambo ya waumini ilivyo magumu kweli kweli na huyu hajaanza leo kutukana viongozi alianza na kardinali pengo sembuse makonda
 
Mkuu Pascal Mayalla, tulishasema hapa kuwa lengo lilikuwa zuri, tatizo ni njia aliyotumia ndugu RC. (Hapa nimepata kigugumizi cha jina) tulitegemea haya yaje! Haina jinsi, tunywe tu maji.
 
Mtu akipata zero(akizungusha),hua anapewa vyeti?,Ngwajima kasema anavyeti vya makonda alivyopata ziro
Pasco mayala katumia fursa hii kujipatia vicent toka kwa GSM na makonda ili awatetee lakini kasahau kuwa wana JF wengi siku hizi ni Wajanja wanajua kuwa kuna Timu ya majungu na uongo itaenda kwa makonda kuchukua pesa kisha wajidai kumtetea lakini moyoni wanajisuta.
 
Safari hii mliopewa hela mmsafishe Makonda mtaumbuka sana.
Gwajima huwa anapiga panapouma siku zote na aliyepigwa huwa haachi kuweweseka
Anaefikiri kuwa yeye si kiumbe aseme na kisha atuambie yeye ni nani, kama ni jiwe tujue kwa maana vitu vyote hai na visivyokuwa hai ni viumbe kwa maana ya kuwa vyote vilivyoumbwa na mwenyezi Mungu hata shetani nae ni kiumbe
 
Ni kweli utumishi wa Mungu ni zaidi ya Rais
Ni kiwewe tu! Nani alimpa utumishi wa MUNGU. Kila anayehubiri anajiita mtumishi wa Mungu. Kila mtu anataka aitwe mtumishi wa Mungu. yeye aseme ni mchungaji, muhubiri.

Sasa naona nasema ni zaidi ya Rais. Hata Yesu alikataa kuambiwa ni zaidi ya Kaizari.
 
Back
Top Bottom