Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Anaefikiri kuwa yeye si kiumbe aseme na kisha atuambie yeye ni nani, kama ni jiwe tujue kwa maana vitu vyote hai na visivyokuwa hai ni viumbe kwa maana ya kuwa vyote vilivyoumbwa na mwenyezi Mungu hata shetani nae ni kiumbe
Leta reference ulikotoa haya maneno
 
Kwa nini sasa lifutwe???
Mkuu wa mkoa hana mamlaka ya kufuta kanisa na hata likifutwa yy atafaidika na nini? akumbuke ni makonda alianza kumchokonoa Gwajma na sasa Gwajma kaamua kujihami iweje mtu kaamua kujihami wapige hesabu ya kufuta kanisa lake? ina maana walikuwa wanamtafutia sababu tu.
 
Ziro is zero hata upambe namna gani ukipata F vipindi vyote ni zero tu.
Hata ukitoa matamko yanayo vuruga nchi au ukapiga kiongozi anayetambuliwa kikatiba .
Ni vyema upewe Kazi inavyo kufaa.
Kama kukamata wavuvi haramu.
Hapo mheshimiwa ajipime mwennyewe asingoje rungu la jemadari.
 
Aisee kumbe wengine mmesoma kw kukariri,kwani akiwa na result slip si ni cheti pia?
Nyinyi mnawajua watumishi wote wanaosali kwa gwajima je kama wamempelekea ushahidi huo wa kuprint hata kama ni document sio cheti?pascally wewe nina wasi wasi utakuwa ni mhanga kama daudi bashite.
Aliekwambia pascal kasoma ni nan mkuu? Hawa waandishi Si ndo wale form four failures.??

Hawa bure kabisa
 
Haya yote yanayoendelea kwa ndugu yangu Paul Makonda ni matokeo ya kufanya kazi kwa sifa,uonevu,dhuluma,
kuwaharibia watu na kuwachafua wenzako ili ww ndio uonekane mchapa kazi,kufanya kazi kwa visasi ili kuwakomoa watu wengine.Hakuna mwanadamu mkamilifu kila MTU ana mapungufu yake ndio maana mwisho wa siku mtu ukimharibia anakaa kimya kujipanga ili nae akuharibie kwa namna yoyote ile.Watawala wetu,viongozi wetu wakifanya kazi kwa kufuata katiba,sheria, kanuni,miongozo
mbalimbali, Job descriptions,hekima na busara itapelekea kupunguza malalamiko kama haya ya Gwajima kwa viongozi wetu.
 
Ni rahisi sana muumini wa kawaida kuingia mbinguni kuliko mchungaji kuingia mbinguni. Trust me

Hivi mnamuabudu sana Makonda eeh? Aliropoka upuuzi na kwa Gwajima kamjibu upuuzi. Tatizo liko wapi hapo?

Acheni kumtetea huyu mjinga anaechafua watu
 
Kabla ya kuanza kumchambua huyo Nduguyo Msukuma mwenzio Mchungaji Gwajima naomba kwanza tuanze na Wewe kwa kukuuliza kwamba mbona siku hizi hueleweki halafu naona kama vile kuna Vitisho umevipata au Maslahi yako yameshaanza kuguswa kwani baada ya ujio wako ndani ya miezi miwili ya kuisema Serikali ya Awamu ya Tano ( 5 ) kuanzia Rais na Watendaji wake akiwemo Daud Albert Bashite ( sasa Paul Christian Makonda ) kwa wiki hizi mbili tatu naona na Wewe umeamua tena kubadili gia angani ghafla kwa kuanza kujikosha kama siyo kujipendekeza kama siyo kujikolombweza kwa Utawala ule ule uliokuwa na naamini bado unauchukia.

Najitahidi kukutofautisha Wewe na Steve Nyerere lakini ninashindwa sijui kwanini.
Mkuu ukirudia kusoma thread ya Paschal ndiyo utaelewa anamaanisha nini! hata mimi mwanzoni niliingia chaka nikaanza kumtuhumu Paschal, siku hizi amebadilisha mashambulizi anatumia ndege zisizo na rubani, jamaa mjanja sana huyu.
 
Ni kiwewe tu! Nani alimpa utumishi wa MUNGU. Kila anayehubiri anajiita mtumishi wa Mungu. Kila mtu anataka aitwe mtumishi wa Mungu. yeye aseme ni mchungaji, muhubiri.

Sasa naona nasema ni zaidi ya Rais. Hata Yesu alikataa kuambiwa ni zaidi ya Kaizari.
Unaumia sana Gwajima kuwa mhubiri? Umemuelewa anamaanisha nini anaposema yupo juu ya Rais?
 
Mayala njaa itakuua hapa mjini acha kujidhalilisha. Mayala unayoyazungumza ndiyo yale yale ambayo vijana waliambiwa wayafanye ili kumpa mtu sifa za uongo.
Wao nasikia walipewa 2m mwenzetu umeambulia ngapi?
huyo mlevi anayesema vyeti vyote vya watumishi wa serikali vipo serikalini wenyewe wana nakala naye zuzu kweli.....baba askofu anasema matokeo sio vyeti.
 
Hivi mnamuabudu sana Makonda eeh? Aliropoka upuuzi na kwa Gwajima kamjibu upuuzi. Tatizo liko wapi hapo?

Acheni kumtetea huyu mjinga anaechafua watu
Gwajma anajihami baada ya kuchokozwa na makonda, cha ajabu eti wapo watu wanabariki uchokozi wa makonda huku wakitaka Gwajma akae kiimya!
 
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Huyu ni mchungaji wa Mungu au mungu. Hili la kudai anavyo vyeti vya Daudi Bashite na Paul Christian, Jee hii inaweza kuwa kweli?!. Nijuavyo mimi, mtu ulikuwa ukipata Div. 0 hupewi cheti chochote na NECTA zaidi ya Leaving Certificate, sasa hicho cheti cha Daudi Bashite alichonacho Mchungaji Gwajima, kimetoka wapi?. Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo madhabahuni, jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu, au ndio hawa wachungaji wanaomtumikia mungu?!.
Mkuu Paskali,

Nadhani hoja yako kuu ni uongo wa Gwajima...!! Lakini pamoja na kuelezea uongo wa Gwajima bado umeshindwa kuupangua uongo huo kwa kuweka ukweli wenyewe!!

Ina maana hujaona mapungufu ya hoja yako hapo?!

Lakini si hivyo tu, hapo juu kwenye RED unahoji:"Hili la kudai anavyo vyeti vya Daudi Bashite na Paul Christian, Jee hii inaweza kuwa kweli?!" Hapa unapishana na hoja yako kuu ya uongo wa Gwajima na kinyume chake unafanya shaka ikiwa anayosema Gwajima yana ukweli wowote! Umetoa chance ya uwezekano wa Gwajima kwamba anasema kweli!

Hiyo nayo haiturudishi kule kule kwamba ina maana hujaona mapungufu ya hoja yako?! Upande mmoja una-conclude kwamba Gwajima ni muongo na kwa upande mwingine unatoa chance ya kuwepo ukweli kwenye hoja ya Gwajima... which is which?
 
Mashambulizi ya Mayalla kwa Daudi ni ya hatari ni kisu cha mgongoni. Ni kweli Gwajima kaibua kufikirisha kutokana na ushaidi alioutaja... mfano Daudi hakuchaguliwa/hakupata nafasi ya kujiunga na sekondari baada ya kumaliza Nyanza primary halafu tunamuona Daudi kajiunga na Pamba secondary ambayo ni shule ya serikali (kunahitaji ufafanuzi) pili Christina ni nani kwa Daudi mpaka amuunge na Paul? Na kwa nini sasa Christina yuko tayali kumuumbua Daudi?

Kuna mahali dot za kupachikwa jina Makonda imepatiwa connection kwamba ni initial object M kwenye Paul Christian. M

Utata mwingine upo kwenye kuwa vyeti ofisini kwa mchungaji je ni copy ya results slip au original? Amevipataje?

Swali lako la msingi linajibiwa na swali hili kati ya mchungaji na rais nani humpigia magoti mwenzie kwa hiyari?

Mwisho: Gwajima kaeleza kisa cha Daudi kumtaja ili kumchafua ni hofu ya kisiasa na hapo vita lazima iwe kubwa maana kuna adui mpya kaainishwa ambae ni Kitwanga, na hapo ndio Daudi aka Paul anapoharibu maana ya vita ya Madawa.
 
Kwani yeye alivyomsingizia mwenzake anauza madawa na ushaidi asipate alitegemea nini
Hapa ni Jino kwa Jino tu, Hata kama ikiwa Gwajima amesema uongo hawezi kufungwa kwa vyovyote
Bashite si alianza yeye kusema Uongo, basi na yeye akafungwe kwa kumsingizia Madawa Mtumishi Wa Mungu
 
Kwanza nashauri tusimpuuze sana Gwajima. Ana watu wengi, na si ajabu kupata taarifa kama matokeo ya form 4. Kwani tuna uhakika gani kwamba hakuna muumini wa kanisa lake anayefanya kazi NECTA? Lkn kwa upande mwingine, tuombe pia kile anachoomba Paskali kiwe kweli. Kwamba isije kudhihirika kwamba yule kiumbe jina lake la kweli ni Daud Bashite! Itakuwa ni a shame of the century.. Cha muhimu zaidi, tunaomba ukweli ujulikane na kila mtu atendewe haki.
 
Back
Top Bottom