Mtoa mada umeshindwa kuficha hisia zako. Ulichofanya hapa, ni certified butt kissing. Gwajima ametoa tuhuma nzito akidai ana ushahidi, mtoa mada unatuambia kuwa anadanganya ilhali pia hujatoa ushahidi, just some theories. It's his words against yours. Mtoa mada ungekuwa makini, ungeshauri Gwajima apelekwe kwenye vyombo husika na atoe ushahidi wa tuhuma alizotoa, na kama uongo basi awajibike. Mpaka sasa, sio Magufuli wala Bashite/Makonda aliyechukua hatua kutokana na tuhuma za Gwajima, pengine wana sababu za kukaa kimya.
Kuhusu Gwajima kusema yeye ni zaidi ya rais, inawezekana hayuko sawa ila sio uongo bali suala la mtazamo. Ametoa kauli hizo mbele ya kondoo wake, so pengine katika imani na mafunzo yao, uongozi wa kidini una nafasi na hadhi kubwa kushinda uongozi wa kidunia.