Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Hajasema ana matokeo, amesema ana vyeti mezani kwake, hivi kweli kuna cheti cha divisheni 0 ya miaka hiyo?.

Paskali
Paskali kwa ulichokiandika hapa unastahili kukamatwa "kwa kuivua nguo serikali". Kama alivyosema Gwajima kuwa atashangaa Ndalichako na JPM wasipochukua hatua dhidi ya Bashite, mimi pia nitashangaa iwapo hadi kesho muda huu utakuwa hujaswekwa mahabusu kwa kutumia akili nyingi kuivua nguo serikali!
 
Mtoa mada umeshindwa kuficha hisia zako. Ulichofanya hapa, ni certified butt kissing. Gwajima ametoa tuhuma nzito akidai ana ushahidi, mtoa mada unatuambia kuwa anadanganya ilhali pia hujatoa ushahidi, just some theories. It's his words against yours. Mtoa mada ungekuwa makini, ungeshauri Gwajima apelekwe kwenye vyombo husika na atoe ushahidi wa tuhuma alizotoa, na kama uongo basi awajibike. Mpaka sasa, sio Magufuli wala Bashite/Makonda aliyechukua hatua kutokana na tuhuma za Gwajima, pengine wana sababu za kukaa kimya.

Kuhusu Gwajima kusema yeye ni zaidi ya rais, inawezekana hayuko sawa ila sio uongo bali suala la mtazamo. Ametoa kauli hizo mbele ya kondoo wake, so pengine katika imani na mafunzo yao, uongozi wa kidini una nafasi na hadhi kubwa kushinda uongozi wa kidunia.
 
Wote mnakumbuka sokomoko la Mch. Gwajima na Dr. Slaa, pia la Mch na Askofu Pengo na sasa hili la kwake na Mh. Daudi. Mara zote amekuwa akiibuka na ushahidi uliyokamili kiasi cha kuwafanya wapinzani wake kukaa kimya.

Je ni nani aliye nyuma yake?

Na nini utakuwa mwisho wake, kwenye nchi za aina ya Afrika?
Nyuma yake kuna waislam na wakristo wa Tanzania wasiopenda mambo ya kijinga.
 
Hili jambo ni rahisi sana anayesemwa ni Daudi Bashite atoke na vyeti vyake OG na kuuthibitishia umma kuwa yeye sio Daudi ni PCM.

Kuna wakati trump alimwandama Obama kuwa si mmarekani kwa sababu hakuzakiwa marekani. Obama mwanzoni alipuuza ila nadhani alishauriwa aonyeshe cheti chake cha kuzaliwa ili kumaliza ubishi na anafanya hvo...ingawaje yeye alisema ni jambo la kipuuzi ila kwa kiasi fulani lilimaliza kikichokuwa kinaendelea. Ingawa kuna baadhi waliendelea na msimamo wao kuwa siyo mmarekani.

PCM toka na vyeti vyako wainyeshe watanzania kuwa wewe si DAB Bali wewe ni PCM...ikiwezekana hata na cheti cha kuzaliwa uonyeshe ili kumaliza hii kitu once na for all.

Ukishaonyesha wa kuamini ataamini na wa kutokuamini ataendelea kutokuamini na baada ya hapo endelea kuchapa Kazi kama siafu.

Ukiendelea kukaa kimya kwa madai eti siwezi kuwajibu wapiga kelele unatufanya tuamini yanayosemwa juu yako ni kweli.
Kukaa kwake kimya yawezekana yuko kwenye harakati yakutengeneza hvyo vyeti.kila kitu kinawezekana chini ya ccm,hadi maiti wanapigaga kura.
 
Fakalava, asante sana.......Kuhubiri neno ni pamoja na kukemea Maovu.
Gwajima hajakosea kukemea maovu!
 
Back
Top Bottom