Nukuu ya Mtumishi Gwajima aliposema atafanya nini baada ya kuchafuliwa na issue ya drugs
"Wajinga hulipa kisasi
Wenye akili huachia
Walio na Mungu husamehe,
Mimi nina Mungu kwahiyo nasamehe"
Kinachoendelea kanisani kwa Gwajima haki hakisi hata nukta moja ya alichokisema
Watumishi kwa mujibu wa bibilia wanatufunza tusamehe saba mara sabini,
Sala ya Bwana inasema Mungu atusamehe kama tunavyo wasamehe waliotukosea
Gwajima aliwahi kumporomoshea matusi mazito askofu Pengo, lakini Pengo alijibu namsamehe na nitamuombea kwa Mungu
Katika ukristo vita yetu si ya kimwili bali kiroho, Gwajima anapigana vita ya kimwili sasa, goti pekee lilitosha kumuachia Mungu afanye mustakabali kwa alichofanya makonda kwa mtumishi
Gwajima amesamehe nini sasa? Kauli kali za kidunia dhidi ya mtu aliye mkosea hazi akisi maneno yake kama mtumishi, Mungu wetu hadhiakiwi wala hapiganiwi kwa nguvu na fitina za kidunia
Ni kupitia maombi, kuongea na Mungu direct na kumuachia Mungu kutenda kwa kadiri imfaayo
Mwisho kabisa nimalizie kwa kusema Hii haina uhusiano wowote na kumtetea Makonda dhidi ya kashfa ya kutumia vyeti vya kugushi.
Kama raia mwema naunga mkono Makonda athibitishe elimu yake na ikiwa amefoji sheria ichukue mkondo wake kama kawaida