La Princesa
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 1,049
- 1,160
Habarini wanajamvi,
Mimi siyo muandishi mzuri wa threads lakini kwa hili la Gwajima na uchungaji/utumishi feki nimeguswa kulizungumzia,Ninaamini baada ya hapa moyo wangu utapata amani..
Nimekuwa nikiwafuatilia watumishi hasa hawa wa makanisa yanayojiita ya maombezi kwa ukaribu sana na nikagundua vitu vingi sana kutoka kwao...Ila leo sitaki kuwaongelea wengine,case study yangu atakuwa ni ndugu Gwajima...!Katika utafiti wangu usio rasmi nimegundua ya kuwa Gwajima ni mtumishi feki wa MUNGU(Kama nimekosea,MUNGU WA MBINGUNI ALIYE HAI ANISAMEHE DHAMBI HII).Ninasema hivi kwa sababu zifuatazo....
i) Watumishi wa Mungu hawalipi kisasi,Kisasi ni cha Mungu,Hiki kitu kwa ndugu yetu Gwajima hakipo kabisa,akiinza kuongea pale kanisani kwake kama wewe ni mtu usiyemfahamu unaweza dhani ni mtu tu wa duniani anatoa madukuduku yake...Kichambo heavy alichowahi kumpa Kardinali Pengo,Paul Makonda na Emmanuel Mbasha ni mfano hai wa tabia yake halisi.
ii)Watumishi wa Mungu Hawarushii watu MAPEPO Bali waganga na wachawi ndiyo hufanya hivyo,Nimesikitishwa sana na clip niliyoiona ikisambaa mtaani Gwajima akiyaamuru MAPEPO yaende kumuingia ndugu Paul Makonda,Hii ni kitu mbaya sana kuwahi kufanywa na mtu anayejidadavua mbele za watu kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu...Yesu alisema ndugu yako akikupiga upande wa kuume,mgeuzie na kushoto,maana yake ni kuwa SAMEHE SABA MARA SABINI,Je Ndugu Gwajima anatumia NENO Gani kutekeleza anayoyatekeleza?
iii) Neno la MUNGU linasema vita yetu si ya Damu na Nyama,kwa nini yeye anakubali kupigana vita hiyo?Je kuna haja ya mtumishi wa MUNGU kukaa nyumbani mwa BWANA huku BODYGUARDS wakiwa naye kila hatua anayopiga,je kuna kitu gani anakiogopa kinachomfanya aweke ulinzi mpaka kanisani.
Nmaliza kwa kusema,Yesu alisema siku za mwisho watatokea,manabii feki,makristo wa uongo,watumishi feki watakaotumia jina lake kuponya wagonjwa na kufanya miujiza mikubwa huku wakijua ya uwa ndani yao wanamtumikia baba wa uongo (Lucifer)Hivyo Mungu atusaidie tuweze kuchanganua kuwatambua watuishi feki kma Gwajimana wale wanaosimama katika kweli ya Mungu...Wafuasi wa Gwajima amkeni katika usingizi mzito msijeangamia kwa kukosa maarifa
NAWASILISHA