Maboso
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 5,164
- 5,762
Hivi kati ya watumishi wa Mungu, Gwajima naye ni mmojawapo? Hata kama kakosewa kama anavyodai, je yeye neno la kusamehe huwa linampita pembeni? Au akisoma Biblia vifungu vinavyohusu kusamehe huwa vinafutika? Huwa anawafundishaje waumini wake kuhusu somo la msamaha?
Mathayo 6:14-15 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba wenu wa mbinguni atawasamehe ninyi bali msipowasamehe watu makosa yao wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu."
Waefeso 4:32 "Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma ninyi mkasameheane kama na Mungu katika kristo alivyowasamehe ninyi."
Mathayo 18:21-22 "Kisha petero akamwendea akamwambia Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi nami ni msamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia sikwambii mara saba bali hata saba mara sabini."
1 Wakorintho 13:4, 5. “Upendo ni wenye ustahimilivu na wenye fadhili. Upendo hauna wivu, haujigambi, haujivuni, haujiendeshi bila adabu, hautafuti faida zake wenyewe, hauchokozeki. Hauweki hesabu ya ubaya. Haushangilii juu ya ukosefu wa uadilifu, bali hushangilia pamoja na kweli. Huhimili mambo yote, huamini mambo yote, hutumaini mambo yote, huvumilia mambo yote.”