Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Bila kujali kuwa Gwajima ni nabii wa uongo au ukweli...ukweli utabakia kuwa ukiwa unamtumikia MUNGU wewe ni zaidi ya raisi. Mungu anasema, yeye ni Mfalme wa Wafalme, ni Bwana wa Majeshi, ukiwa unamtumikia yeye unakuwa ni zaidi ya mkuu wa majeshi ya nchi.
anamtumikia mungu yupi
 
Bila kujali kuwa Gwajima ni nabii wa uongo au ukweli...ukweli utabakia kuwa ukiwa unamtumikia MUNGU wewe ni zaidi ya raisi. Mungu anasema, yeye ni Mfalme wa Wafalme, ni Bwana wa Majeshi, ukiwa unamtumikia yeye unakuwa ni zaidi ya mkuu wa majeshi ya nchi.
Gwajima kavunjiwa heshima na lazima ajitetee kwa alivyoona yeye inafaa
 
Kweli yeye ni zaidi ya Rais katika madhabahu/familia yake, kama wewe ulivyo zaidi kwa mkeo/mmeo.
 
Huyu mchungaji ni ajenti wa IBILISI, na kila anaemuamini na kumfuata, ataishia MOTONI, mwenye masikio na asikie !
Dogo jifunze kua na akiba ya maneno...
Unaingilia kazi ya Mungu kuhusu nani aende peponi na nani aingie MOTONI.
We ni mkristo I hope hebu fanya kupitia
James 3:3-6
Proverbs 18:21
Soma kitabu chenu you'll learn a lot.
Ni kweli vitabu vimetuonya kuhusu manabii wa uongo...Lakini yatupasa kua makini unapo mtuhumu mtumishi wa neno la Mungu.
Simemi Gwajima ni mtumishi wa Mungu au sio.
Ninacho emphasize hapa ni bora ujitenge na kukashifu hawa watu maana hata vitabu vinasema hivyo rejea
Psalms 105:15
 
Gwajima ni tapeli kama matapeli wengine.

Ukweli utabaki kuwa ukweli chuki na roho yake ya visasi si funzo kwa wakristu tunaofuata mafundisho ya Bwana YETU YESU KRISTU.
We nae ni wale wale tu
 
We nae ni wale wale tu
Wale wale wakina nani?

Kama wewe ni mpagani utaona sawa na kushabikia , kama wewe ni muislamu ni utashangila maneno yake huyu Gwajima , lakini kwa Mkristu aijuaye vema mafundisho ya Kristu Yesu ni dhahiri atapingana na baadhi ya maneno ya kichonganishi na ya kufitinisha anayoyatoa Huyu Mchungaji.
 
Wanabodi,
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.

Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.

Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, Makonda alipewa tuu list yenye majina na kazi yake ilikuwa ni kuwataja tuu, aliyemtaja Gwajims ni muumni wake mtiifu, koss ls Makonds ni lipi?!.

Jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa, kwa ubaya na kumsingizia uongo, ndivyo Bwana Yesu alivyofundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?!. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kuume mgeuzie na la kushoto. Adui mpende. Samehe saba mara sabini. Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo? .

Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.

Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.
Paskali
Jumatatu Njema.
Paskali
Mkuu kumbe kuna baadhi ya mada upo shallow sana, jitahidi kujikita zaidi kwenye mada ambazo una uelewa mpana. Hii ya kumwita gwajima nabii wa uwongo umepotoka na utaishia kushusha heshima yako.

Unadai gwaji kamwita 'huyu kiumbe'. Kumbuka Yesu alimwambia petro "rudi nyuma shetani".. huyo ni Yesu anamuita Mtume petro shetani kwa wakati huo. Leo gwaji kasema huyu kiumbe unashangaa nini.

Pia, kumbuka Martin Luther King alikuwa Askofu na bado alipambana dhidi ya uonevu, manyanyasa na ubaguzi na alishinda. Askofu Desmond Tutu wa afrika kusini naye alikuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanyonge.

Hakuna tatizo kwa gwajii kuumbua mtu mwenye cheti feki au anayetumia cheti cha mtu mwingine. angalia sasa anayoyafanya huyo Rc ya kuvamia wanahabari. Na bado unathubutu kumtetea. Ajabu sana.

Nakukumbusha, sio lazima uandike kila kitu. Dili na yale machache unayoyajua na kuyaweza. Ya kolomije waachie wengine.
 
Haiwezekani amuite Mkuu wa Mkoa kiumbe...ni kosa kubwa sana
Ni kiumbe ndio na wote sie ni viumbe! kumbe ni nani ndugu? tena likitumika makanisani ndo mahali pake, japo sina hakika kama lile la Gwajima ni kanisa! nahisi hao jamaa wanasali kwa Gwajima na sio kanisani
 
Back
Top Bottom