Nimevumilia sana lakini sasa nimechoka, yaan ni wiki ya tatu sasa kila nikienda kanisani kusikiliza neno la Mungu katika Kanisa la Ufufuo na uzima ila baada ya kusikiliza neno la Mungu nasikiliza majungu, umbeya na udaku wa mtu anayeitwa Bashite, halafu muda wa sadaka ukifika naambiwa tutoe sadaka, sitakubali tena jumapili hii kufanya hili swala, nitatoa sadaka kama nitasikiliza neno la Mungu mwanzo mwisho, sio majungu, yaan mtu anahubiri majungu tu kila jumapili? sasa, sijui neno la Mungu tutaanza kuhubiriwa lini?
Naomba sana mchungaji husika, jumapili uhubiri neno la Mungu, tunataka kusikiliza neno la Mungu, au basi ongelea Bashite huku ukihusianisha na neno la Mungu na biblia.