Wanabodi,
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.
Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.
Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, Makonda alipewa tuu list yenye majina na kazi yake ilikuwa ni kuwataja tuu, aliyemtaja Gwajima kuwa anajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, sio Mkuu wa Mkoa, Makonda, bali ni muumini wake mtiifu, ambaye nimemtaja hapa chini na alichokisema!, sasa kosa la Makonda ni lipi?!.
Jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ubaya na kumsingizia uongo, ndivyo Bwana wetu Yesu Kristo alivyotufundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?!. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kushoto, mgeuzie na la kuume!. Yesu ametufundisha "adui mpende". Yesu ametufundisha "samehe hata saba mara sabini". Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo?
Je, Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?.
Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?
Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.
Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.
Jumatatu Njema.
Paskali
Update
Wanabodi, kwenye siasa, hakuna rafiki wa kudumu, wala adui wa kudumu, kuna just common interest.
Japo katika bandiko hili, nilitofautiana na Gwajima, lakini kufuatia kwa sasa na mimi ni kada, wa Chama Cha Mapinduzi na mgombea aliyepitishwa na chama changu kugombea ubunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, ni Askofu Gwajima, then naomba kudeclare kuwa sasa namuunga mkono Askofu Gwajima 100% kwa 100% tukalikomboe jimbo la Kawe lilokuwa utumwani kwa kipindi cha miaka kumi, tulirejeshe CCM!.
Kwa Kawe ya Maendeleo, chagua CCM, Chagua Gwajima, na kwenye uRais ni Magufuli, Mbunge ni Gwajima na madiwani wa CCM.
Mimi na Gwaji Boy...dam dam!.
P