Mchungaji Gwajima ni nani? Tukianzia hapa Tutajua namna ya Kudeal na watu aina yake

Mchungaji Gwajima ni nani? Tukianzia hapa Tutajua namna ya Kudeal na watu aina yake

Mnachosha na vithread vyenu vya kijinga
We bwege nini?! Kuna aliyekuita humu?! Kuna mahali nimeku-mention kama sio kiherehere chako kilichokufanya uni-quote?! We jamaa sijui wa wapi wewe....
 
Katika orodha ya wana habari ambao hua nina waheshimu sana hapa Tanzania jina lako pia lipo (ni msimamo wangu, sio lazima wote mue sawa na mimi) but kwenye hili kaka umedandia kitu usicho kijua kabisa; Biblia unaifahamu kwa kiwango kidogo sana. Una haraka gani kaka ya kujua kama huyu askofu anavyo vyeti vya mhe au laa!? Amesema mwenyewe kwamba atavitoa muda ukifika, why can't we wait and see!? Hivi leaving certificate kwa Kiswahili c ni cheti pia? Mfano mtu aje aseme hivi; "Pascal hukufauru Secondary wewe, wewe ulipata 0 na cheti chako ninacho" and then akatoa hiyo leaving certificate kama ushahidi utambishia wapi ili hali wewe hutuoneshi hicho cheti chenye matokeo!? Well, nashawishika kuamini kwamba Gwajima anachosema ni kweli kwa mwenendo hu, mtuhumiwa badala ya kujielekeza kwenye kile anachotuhumiwa nacho yeye anabadiri viongozi wa dini ili wamuombee; mhe RC anasali kanisani kwa mchungaji Ndeki wa Living water, why can't he go and be prayed kwa mchungaji wake badala yake mara awaite Waislam mara Lutheran, anaogopa nini kwenda kanisani kwake ili aombewe? Mchungaji Ndeki na askofu Gwajima wote hawa ni Wapentekoste (haya ni madhehebu ya kikristo) kwanini aachane na wapentekoste wenzie na kujikita kwenye IMANI zingine? Pascal, hivi unafahamu kwamba Wapentekoste hawaamini kama Waislamu wana mwamini Mungu wa aina yao? Nafikiri ungejikita kwenye kutafiti mwenendo wa Bashite mara baada ya yeye kutupiwa dongo hata wewe ungeona kuna namna Fulani ya UKWELI ju ya shutuma anazo pewa.
Hivi mlitaka Gwajima baada ya kutuhumiwa anauza/anatumia madawa hayo ya kulevya akae tu kimya bila kusema chochote kwa watu anao waongoza!? Kaka, unafiki basi hauna kwao. Waingereza wanao msemo wao kwamba silence means Yes, so angekaa kimya hata mimi ninge amini kwamba askofu nae ni TEJA. Amejibu tena mnasema eti anyamaze kwakua yeye ni Mkristo, hiyo sio sawa
Nyie wote ni wasukuma, yaani Gwajima, mhe RC na wewe; kaani kikao chenu cha kifamilia sasa (joke of the day brother; heshima yangu kwako bado iko pale pale.)
Mkuu kwanza asante kwa kuniheshimu nami ningependa kuitunza heshima hiyo ila linapokuja suala la imani za watu, mimi ni mwepesi sana kukubaliana kutokukubaliana.
Nimeraise issues 3.
1. Jee Mchungaji Gwajima ni Nabii wa kweli au wa uwongo? . Nikatoa reference ya Yesu kuhusu jinsi ya kuwatambua manabii wa uwongo, utawatambua kwa maneno yao na matendo yao. Nikawawekea reference 2. Moja ya maneno alipomtukana Muadhama Poliycarp Cardinali Pengo. Referemce ya matendo nimeweka ushuhuda wa mwana JF aliyetendwa na kueleza humu jinsi alivyotendwa.
2. Hoja yangu ya pili ni kusema uongo kuhusu vyeti. Mchungaji ameeleza kuwa Bashite alipata sifuri na anavyo vyeti mezani kwake vinavyoonyesha hiyo sifuri!. Nikasema huu ni uongo. Cheti ni kitu kimoja na nakala ya cheti ni kitu kingine, nikasema Gwajima ana nakala na sio vyeti! . 2. Matokeo ya Div 0 hayana cheti, hivyo Mchungaji Gwajima hawezi kuwa na Cheti cha Bashite kuonyesha alipata 0 kwa sababu hakuna cheti kama hicho hapa duniani wala mbinguni. Kitu ambacho kipo ni matokeo. Matokeo sio cheti ni public document. Cheti cha Leaving certificates hakionyeshi matokeo yoyote.

Nikasema mimi ni Tomaso, siamini mpaka Gwajima atoe vyeti alivyodai anavyo vinginevyo ni muongo!.
3. Hoja yangu ya mwisho ni kuhusu Gwajima kuuza unga, nikasema hawezi kumlaumu Makonda kwa sababu kosa la Makonda ni kumtangaza tuu, nikasema Makonda yeye kapewa jina tuu. Mchungaji Gwajima anadai kuwa Makonda kamsingizia kwa ajili ya wivu wa helcopter na kutaka kugombea Misungwi. Ukweli wa tuhuma za Gwajima kuuza unga zililetwa humu JF kitambo na muumini wake mwenyewe na link niliwawekea kwenye bandiko langu hili

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais...
Paskali
 
Tuambie vizuri were mwenye ujuzi was manabii was uwongo. Tujuze katika Biblia wamesemaje? Ukilinganisha na karama alizonazo Gwajima.
 
Umekua muda sasa, mitandaoni majina mawili yamechukua nafasi Gastura na Bashite. Nadhani huu uwe muda sahihi kwa watanzania tuujue ukweli.

Ukitazama kwa umakini, Gastura ananafasi kubwa ya kutumia vyeti vya mtu compared to wanayemuita Bashite.

Kwa mujibu Wa Tapeli, Kibwetele Wa Tanzania Gwajima, Bashite anatokea Familia Duni sasa sijui alitumia pesa gani au ushawishi UPI kununua cheti. Ila kwa mkuu Gastura wote tunajua katokea familia bora hivyo Uwezo Wa kununua au kufoji alikua nao kuliko Bashite.

Ombi langu kwa Gastura, sisi Wanachama Wa vyama vya upinzani tunadhani ni sahihi kufahamu ukweli kuhusu yeye kwa maana yeye ni waziri mkuu wetu.

Kama kweli ana vyeti halali inakuaje ngumu kwa yeye kuviweka wazi tangu aanze itwa zero, mpaka leo Gastura.

Nanyi wana Chadema na wapinzani wenzangu inabidi tukumbuke ukimnyooshea mtu kidole ujue vitatu vinakutazama wewe.

Asanteni[emoji40] [emoji40] [emoji19]
 
Askofu na Mchungaji Gwajima amekuwa moja ya watu maarufu na gumzo kubwa sana nchini. aina hii ya watu wapo duniani kote kwa Dini au Imani zote. Mtu wa namna hii unapoanza naye vita unapaswa kwanza kujichunguza. kuchukua muda mrefu kujichunguza wewe kwanza kabla hujaanza kumchunguza yeye na kuangalia udhaifu wake.

Tumemuona mara kadhaa Gwajima akisimama kuzungumza anachoamini pasipo kuuma uma maneno. Tumwona akimsema Laiyekuwa Rais wa Awamu iliyopita, tulimwona akisema Serikali iyopita kwa Ujasiri na kupelekea kupata matatizo kadhaa. Hakuishia hapo tu. aliwasema hata Viongozi wengine ambao aliamini walikengeuka kwa sababu moja au nyingine pasipo hofu kuwa nao wana jamii kubwa na yenye nguvu nyuma yao. Miaka ya nyuma alikuwepo Mchungaji Mtikila. huyu alikuwa na Roho hii pia miaka hiyo. alizungumza alichoamini pasipo kujali jamii kubwa inayomzunguka ina aamini nini.

Kuna haja ya Kujua Mchungaji Gwajima ni nani? ametokea wapi, ameishi katika mazingira gani, anaamini nini, ana elimu gani na kwa nini anajiamini.

tukifaham historia ya gwajima tutajiuliza ni kwa nini alitajwa kwenye uhusika wa kuuza au kujihusisha na madawa ya kulevya? alijiamini nini kusema kuwa akipimwa hata akikutwa ana kemikali za sigara/tumbaku au pombe iitwe ni madawa ya kulevya? wakati wa kupimwa walikuwepo akina nani?

habari zote kuwahusu viongozi mbalimbali au data zao na ujasili alio nao anaupata wapi? watu wa namna hii huongea yale ambayo wengine hawawezi kuongea. huamini kuwa wao ni chachu katika jamii fulani kwa maana ya kuwa wana mchango mkubwa sana. Ukienda kanisani kwa Gwajiama ana waumini wasomi, wasio na elimu dunia kubwa, walio na elimu dunia kubwa,matajiri na maskini. ukiacha waumini wa kanisani kwake. kuna ambao si waumini wa imani yake ila ni watu wanaoamini msimamo wake. na msimamo wa gwajima ni msimamo wa nyundo. hii ni karba au hulka ya watu ambao wao huamini katika kugonga kila amabcho kitakuwa kimewekwa chini yao. gwajima ni nyundo.

Gwajima huwezi ku dela naye kwa vitisho. unahitaji ku deal naye kwa hekima sana na maarifa. unapomtisha yeye huongeza mapambano. huyu ni aina ya watu ambao unaweza ukadhani ni wadogo sana lakini wana ushawishi fulan katika jamii. penda usipende wapo watu wa namna hii.

  1. TUSIMPENDE AU KUMCHUKIA Gwajima kwa sababu Alipishana na Askofu Pengo. Kuna ambao wanaendeleza chuki/unazi kutokana na hili. Askofu Pengo ni binadamu kama mimi na wewe ukiniweka mimi na yeye mbele za Mungu tu binadamu wote sawa. Labda ambacho kitamwongezea Credit ya Kupata Zawadi kubwa au Adhabu kubwa ni Je aliokoa au kupotosha wangapi? ila kama alizini atahukumiwa, kama alisema uongo atahukumiwa, kama alikuwa mnafiki atahukumiwa. hivyo hivyo kwa Gwajima. naye akisimamishwa na mimi ataangaliwa Ameokoa au Kupoteza wangapi..
  2. Tunapomwangalia Gwajima kwa kusema aliwah mtukana Ask Pengo na kuanzia hapo tukamwona hafai kwa sababu "alimtukana" au aliongea alichoamini kuhusiana na Askofu Pengo tunakosea sana. Tuangalie hoja zake peke yake. dini, imani na itikadi zetu zisiathiri jambo hili.
  3. Swali kuu na neno la Imani katika Mfungo huu wa Kwarezima. JE ANACHONGEA GWAJIMA NI UONGO? THIBITISHA UONGO WAKE/ASHTAKIWE HARAKA KWA KUPOTOSHA UMMA WA WATANZANIA.

BASHITE ALETE VYETI TUTAJUA KAMA MTUMISHI NI MWONGO, TUMEKUELEWA, BASHITE LETA VYETI.
 
Mabashite bhana... ujibiwe mara ngapi? Kama huelewi that's your problem and not mine!!!
Fool. Unaandika hoja tofauti wakati akili imeshikwa na bashite! Rudi Facebook
 
We bwege nini?! Kuna aliyekuita humu?! Kuna mahali nimeku-mention kama sio kiherehere chako kilichokufanya uni-quote?! We jamaa sijui wa wapi wewe....
Lofa wewe. Mnajaza server tu. Mmegeuka makasuku kwa kukariri.
 
Dada weka na ushahidi basi. Maana unatokwa mate hata ushahidi hutak kuweka. Tunataka ushahidi wa madai mengine yote. Ila kama amechukua mke wa mtu huyo mtu naye analalamika? Mke wa mtu hachukiliwi.ukiona mke amechukuliwa kwa mtu ujue hakuwa mke wake.

Anyway.... Mi napenda tumfaham kiuhalisia gwajima.chuki tuweke pembeni kabisa.

Makonda tumjadili na kumhukumu kwa haki. Tusiwe na chuki tusiwe na hasira naye. Kwa upole tu tumwambie ndugu leta vyeti. Kama hana basi tunajua hana.

Gwajima ni mnafiki na mchukua wake za watu nan hasojua gwajima amemchukua flora mbasha? amevunja ndoa ya watu? mchungaj gan Tz au padre alovunja ndoa za mtu kama gwajima? Gwajima anajenga majumba ya kifahari kwa pesa za wahumin ambao n maskini wanatafuta pesa kwa shida.....Gwajima Ni mtu hasye na heshma wala staha.....pengo kumtukana amekosea sana lakn pengo ana hekma sana na busara wakat wa kikwete pengo alitajwa kuhusu dawa za kulevya mzee yule alinyamaza...alpotukanwa na gwajima alinyamaza pia....Naomba kukwambia hata rais kikwete sio kwamba ameshindwa kumfunga gwajima hakushindwa ila kikwete ana hekma na busara na uvumilvu sana....kikwete hasyetaka lawama.......Gwajima hana uwezo wa kushndana na rais wa nchi wala serikali kama ww unavotaka kutuamnsha....gwajima ni sawa na mkate mbele ya supu...gwajima ni sawa na tone la maji kwenye bahari....serikali wakimua kumfunga wanamfunga na mna msahau.....kwan wangap ktk nchi tafaut wamefungwa viongoz walokuwa wanasumbua serikali? wafuasi wamelalama weee mwisho wametulia.....hakuna anayemuogopa gwajima wala hana elimu ya kutsha unayotaka wewe kutuamnsha.....Tz ina viongoz wanaoheshma viongoz wa dini...lkn nafac walopewa hao viongoz wa dini wanaitumia vbaya .....kuingilia mambo yasiyowahusu.....nataman kuoneshwe mfano vp serikali ina nguvu zaidi ya waimba kwaya wa gwajima......Gwajima ni tapeli anayeamnsha watu kuwa yeye mfufuaji walokufa....huku katika ukoo wake wanakufa anashindwa kuwarejesha.......Gwajima ni nani? Gwajima n mjanja anayekula pesa za wajinga......Gwajima ni nani? Gwajima ni mtu hasokuwa na sifa ya kuww kiongoz wa dini.....Kwanza kiongoz gan wa dini ulindwe kiasi kile una nn?? Kama kulindwa angelindwa yesu.....Gwajima n mpiga deal......
 
Askofu na Mchungaji Gwajima amekuwa moja ya watu maarufu na gumzo kubwa sana nchini. aina hii ya watu wapo duniani kote kwa Dini au Imani zote. Mtu wa namna hii unapoanza naye vita unapaswa kwanza kujichunguza. kuchukua muda mrefu kujichunguza wewe kwanza kabla hujaanza kumchunguza yeye na kuangalia udhaifu wake.

Tumemuona mara kadhaa Gwajima akisimama kuzungumza anachoamini pasipo kuuma uma maneno. Tumwona akimsema Laiyekuwa Rais wa Awamu iliyopita, tulimwona akisema Serikali iyopita kwa Ujasiri na kupelekea kupata matatizo kadhaa. Hakuishia hapo tu. aliwasema hata Viongozi wengine ambao aliamini walikengeuka kwa sababu moja au nyingine pasipo hofu kuwa nao wana jamii kubwa na yenye nguvu nyuma yao. Miaka ya nyuma alikuwepo Mchungaji Mtikila. huyu alikuwa na Roho hii pia miaka hiyo. alizungumza alichoamini pasipo kujali jamii kubwa inayomzunguka ina aamini nini.

Kuna haja ya Kujua Mchungaji Gwajima ni nani? ametokea wapi, ameishi katika mazingira gani, anaamini nini, ana elimu gani na kwa nini anajiamini.

tukifaham historia ya gwajima tutajiuliza ni kwa nini alitajwa kwenye uhusika wa kuuza au kujihusisha na madawa ya kulevya? alijiamini nini kusema kuwa akipimwa hata akikutwa ana kemikali za sigara/tumbaku au pombe iitwe ni madawa ya kulevya? wakati wa kupimwa walikuwepo akina nani?

habari zote kuwahusu viongozi mbalimbali au data zao na ujasili alio nao anaupata wapi? watu wa namna hii huongea yale ambayo wengine hawawezi kuongea. huamini kuwa wao ni chachu katika jamii fulani kwa maana ya kuwa wana mchango mkubwa sana. Ukienda kanisani kwa Gwajiama ana waumini wasomi, wasio na elimu dunia kubwa, walio na elimu dunia kubwa,matajiri na maskini. ukiacha waumini wa kanisani kwake. kuna ambao si waumini wa imani yake ila ni watu wanaoamini msimamo wake. na msimamo wa gwajima ni msimamo wa nyundo. hii ni karba au hulka ya watu ambao wao huamini katika kugonga kila amabcho kitakuwa kimewekwa chini yao. gwajima ni nyundo.

Gwajima huwezi ku dela naye kwa vitisho. unahitaji ku deal naye kwa hekima sana na maarifa. unapomtisha yeye huongeza mapambano. huyu ni aina ya watu ambao unaweza ukadhani ni wadogo sana lakini wana ushawishi fulan katika jamii. penda usipende wapo watu wa namna hii.

  1. TUSIMPENDE AU KUMCHUKIA Gwajima kwa sababu Alipishana na Askofu Pengo. Kuna ambao wanaendeleza chuki/unazi kutokana na hili. Askofu Pengo ni binadamu kama mimi na wewe ukiniweka mimi na yeye mbele za Mungu tu binadamu wote sawa. Labda ambacho kitamwongezea Credit ya Kupata Zawadi kubwa au Adhabu kubwa ni Je aliokoa au kupotosha wangapi? ila kama alizini atahukumiwa, kama alisema uongo atahukumiwa, kama alikuwa mnafiki atahukumiwa. hivyo hivyo kwa Gwajima. naye akisimamishwa na mimi ataangaliwa Ameokoa au Kupoteza wangapi..
  2. Tunapomwangalia Gwajima kwa kusema aliwah mtukana Ask Pengo na kuanzia hapo tukamwona hafai kwa sababu "alimtukana" au aliongea alichoamini kuhusiana na Askofu Pengo tunakosea sana. Tuangalie hoja zake peke yake. dini, imani na itikadi zetu zisiathiri jambo hili.
  3. Swali kuu na neno la Imani katika Mfungo huu wa Kwarezima. JE ANACHONGEA GWAJIMA NI UONGO? THIBITISHA UONGO WAKE/ASHTAKIWE HARAKA KWA KUPOTOSHA UMMA WA WATANZANIA.
Yangu aliposhindwa kumfufua Amina Chifupa kama alivyoahidi simuamini kabisa.
 
Mchungaji gani anatembea na wake za watu na kuaribu ndoa? arafu eti wafuasi wake wanaenda kufunga pingu za maisha kwake,tafakalini!

Una uhakika na hili usemalo au ndo mwendo wa kuendesha maisha kwa taarifa za kuokoteza mabarabarani kama Bashite
 
Watanzania tuna safari ndefu sana kufika kama charlatans kama hata akina Gwajima wanapata ufuasi.
 
Tulikuwa tukisubiri kwa hamu kusoma hio historia ya Gwajima lakini naona mleta uzi katuacha hewani.
 
Back
Top Bottom