Mchungaji Hananja: Wachungaji KKKT wakihoji vitendo vya viongozi kuuza Mali za kanisa, wanafukuzwa, asema na yeye alisimamishwa mwaka mmoja

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112

Mchungaji Hananja akihojiwa na Bongo5 (ingia YouTube, kaongea nusu saa nzima) ameeleza uonevu mkubwa wanaofanyiwa na viongozi wakuu wa kanisa, na anasema yeye aliandikiwa barua na kiongozi mkuu wa kanisa kumsimamisha kazi bila mshahara kwa mwaka mzima, bila sababu yoyote ile.

Hananja anasema alikataa barua ya kiongozi mkuu wa kanisa kwa kuwa si muajiri wake,

Hananja ameeleza kwamba kanisa linapitia maumivu makubwa kwa sababu ya unyanyasaji na roho mbaya sana, na visasi walivyonavyo viongozi wakuu wa kanisa Hilo.

Hananja ameeleza kwamba viongozi wakuu wako katika wimbi kubwa la kuuza viwanja vya kanisa, na wachungaji wanapohoji, wanafukuzwa na kunyanyaswa sana.


=====

Kuna taarifa kwamba mchungaji Kimaro, kupitia Utumishi wake, kijitonyama imenunua viwanja vya mamia ya mamilioni, na kujenga majengo ya thamani kubwa, na kuna hisia kwamba wakuu wa kanisa wanataka kuviuza waweke Hela mfukoni.

Kanisa pia lilikuwa na hotel huko matema beach, hotel ambayo viongozi wakuu wa kanisa waliweka dhamana ili kupata mkopo wa mabilioni wa kujenga chuo kikuu, mkopo ulitolewa na fedha yote ikabebwa na wakuu wakanisa, benki walivyoanza kudai deni, wakuu wa kanisa harakaharaka wakatafuta mteja waiuze kwa bei ya kutupa. Mwaikali alipokataa hoteli isiuzwe, alitengenezewa zengwe na kufukuzwa kama mbwa, yaani askofu anafukuzwa kama mbwa na kulazwa rumande!

Pia yamekuwepo malalamiko kwamba shule za kanisa zinadorora, ada na fedha za wafadhili zimefanya wakuu wa kanisa wawe mabilionea wakiogelea kwenye fahari kuu. Na hata hospitali ya seliani Sasa ni mlango wa kuzimu, kwa kuwa haina huduma nzuri, na ukipelekwa pale, ni sawa na kusaini hati ya kifo

Zaidi soma: Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu
 
Watu kila mara kupigishwa viharambee na kupewa vibahasha vya michango/sadaka kumbe wajanja wanatia mifukoni tu! Sio poa
 
Kuna sehemu nimesema shoo na malasusa ni matahira wanaotembea
Acha kumtukana Askofu Shoo.
Hapo amehusikaje ?
Malasusa ndiye anayehusika na Dayosisi ya Mashariki na Pwani na ndiye anayemsimamia Dr. Kimaro.

Kanisa la KKKT Lina katiba mbovu sana na ndiyo inayosababisha migogoro na wizi mkubwa ndani ya kanisa Hillo. Kanisa la KKKT ni Mali ya Maaskofu. Kila mmoja ana sharubu. Yaani Dr. Kimaro ni WA Malasusa na sio wa Dr. Shoo. Dr. Shoo Hana maamuzi yoyote juu ya Dr. Kimaro.

Askofu mkuu alipaswa kuwa na mamlaka makubwa juu ya maaskaofu wote wa KKKT na kuweza hata kuwahamisha kwenye Dayosisi nyingine. Ndio maana Vitega uchumi vya KKKT vinakufa kila mahali Kwa sababu wengi sio waaminifu na hawana sifa za kusimamia miradi hiyo.
 
Mimi sijaenda KKKT miaka karibu 10 sasa.... Sadaka inapangwa kutoka juu, eti usharika huu mtoe kiasi fulani... basi hapo harambee za kijinga jinga tu.....ni wakati sasa wa maaskofu kutuachia kanisa
 
Wampe Bagonza hili kanisa litanyooka mbona?
 
Mim sijaenda KKKT miaka karibu 10 sasa....Sadaka inapangwa kutoka juu, eti usharika huu mtoe kiasi fulani...basi hapo harambee za kijinga jinga tu.....ni wakati sasa wa maaskofu kutuachia kanisa
Waumini nao ni makondoo. Kuna upumbavu flani wanaita uwiano mambo ya hivyo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…